Membe amshukia KITINE, amfananisha na "Kingwendu"

Membe amshukia KITINE, amfananisha na "Kingwendu"

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,896
Reaction score
1,866
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema mtu yeyote anayehitaji kugombea urais mwaka 2015 anahitaji kusikia sauti ikimwambia omba na si kukurupuka.

Membe alisema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari likiwemo la kutajwa kuwania urais 2015.

Katika mkutano huo uliolenga kuzungumzia msimamo wa Tanzania kuhusu Jamhuri ya Watu wa Sahara Magharibi na Morocco, Membe alisema hajaisikia sauti ikiniambia omba urais ila kwa ubunge aliisikia.

"Mtu yeyote anayetaka kuomba urais 2015 anahitaji kusikia sauti ikimwambia kila saa omba, yani akilala sauti hiyo anaisikia na hata akitembea … kama akikurupuka lazima awe ameteuliwa na chama chake na kukubalika.

"Kwa upande wangu mimi sijaisikia hiyo sauti ikiniambia omba urais ila kwa ubunge niliisikia, hivyo nikiisikia nitawaambia," alisema.

Akizungumzia tuhuma zilizoelekezwa na mmoja wa viongozi wastaafu nchini kwamba anajenga hoteli nje ya nchi, alisema kuwa aliyezitoa tuhuma hizo hana tofauti na mganga anayedaiwa kutoa uchawi mkoani Lindi aitwaye Kingwendu ambaye amekuwa akitoa habari za kutatanisha.

"Kingwendu amekuwa akipita katika baadhi ya vijiji na kukusanya wananchi na kuwaambia anayeua watoto wenu ni mama mmoja ana macho mekundu, anakaa upande wa kushoto.

"Wananchi huenda kumkamata mzee na kumjeruhi na wanapokamatwa wanadai ni Kingwendu kawaambia wakati yeye Kingwendu akiitwa anasema hajataja mtu jina.

"Katika ngazi ya Taifa tumeweza kuwa na vingwendu wengi, hivyo ni lazima tuwawajibishe watu kama hao vinginevyo wataleta matatizo, kama tunataka kuwa na taifa lenye ustawi lazima tuwabane watu kama hawa wazungumze ukweli," alisema.

Membe alitaka atafutwe aliyetoa tuhuma hizo na ahojiwe ili aeleze ukweli na endapo atamtaja yeye ndipo ahojiwe huku akisisitiza kwamba kuwepo na vingwendu kutawatesa wananchi hivyo wanapaswa kuwajibishwa

Sosi:
HabariLeo | Membe- Msikurupuke kuwania urais 2015
 
Mzee Kitine hajataja jina, au Membe anamjua mtu anayemzungumzia Mzee Kitine?

naamini ndio maana kawaomba waandishi warudi kwa "kingwendu" oops,
na wamuulize vizuri ili jina litajwe. yaani mpaka 2015 kazi ipo kweli kweli.
watu watapeana majina mapya, watatoana "macho", watakashfiana n.k.
 
Mimi nikiona hizi habari za CCM kushushuana kwenye vyombo vya habari....huwa najisikia njaa - lol.
Membe CCM, Kitine CCM, kwa nini hawayamalizi ndani ya chama chao, kuna haja gani "kumwaga kuku kwenye mtama?"
 
Membe ....bado yupo na senior wake ...kumuita kingwendu.....nadhani ,Kitine hakumpa majina ya kashfa wala kumtaja jina .....sasa kajihisi ...ukirusha jiwe gizani atakayelia limempata!!!! ...

Ikumbukwe kuwa kazi kubwa ya Membe "mzee wa fitina " mwaka 2000 kuelekea 2005 ,ilikuwa ni kuwachafua watu wote waliokuwa na nia ya urais ili kumsaidia KIkwete ...mhanga wa kwanza wa wanamtandao alikuwa..
Hassan ( hassy ) Kitine
iddi Simba
Frederick Sumaye
Salim Ahmed Salim

Hawa kwa wakati tofauti walichafuliwa vibaya na wana mtandao.......Huyu Membe urais ...hafai kabisa....eti anasema ...kuna watu ..wanataka agombeeee ...mbona hatuwaoni....au CCJ?
 
Huenda mkulu anmjua huyu mtu ndo maana ameamua kufanya yeye mwenyewe majukumu ya wizara yake.
 
Joka la mdimu lamsema Kingwendu.

Kusikia sauti ya kufikirika kila wakati ni dalili ya ugonjwa wa akili.

Siasa za bongo!
 
Membe ....bado yupo na senior wake ...kumuita kingwendu.....nadhani ,Kitine hakumpa majina ya kashfa wala kumtaja jina .....sasa kajihisi ...ukirusha jiwe gizani atakayelia limempata!!!! ...

Ikumbukwe kuwa kazi kubwa ya Membe "mzee wa fitina " mwaka 2000 kuelekea 2005 ,ilikuwa ni kuwachafua watu wote waliokuwa na nia ya urais ili kumsaidia KIkwete ...mhanga wa kwanza wa wanamtandao alikuwa..
Hassan ( hassy ) Kitine
iddi Simba
Frederick Sumaye
Salim Ahmed Salim

Hawa kwa wakati tofauti walichafuliwa vibaya na wana mtandao.......Huyu Membe urais ...hafai kabisa....eti anasema ...kuna watu ..wanataka agombeeee ...mbona hatuwaoni....au CCJ?
ukitaka mfahamu Membe vizuri waulize Watanzania waliokua Canada wakati huo Membe akifanya kazi ubalozi wetu Canada! Wengi hawataki kulisikia hata jina lake! Amejaliwa kuwafitini na kuwachonganisha watu!
 
Back
Top Bottom