Mema kwa mkulima wa Tanzania... Bashe na Rais Samia wanafanya kweli

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,889
109,220
Mkulima wa Tanzania sasa hivi ana kituo cha kisasa cha huduma kwa mtej (,Customer care).

Bashe kwa mara ya kwanza Tanzania, anaifanya Wizara ya kilimo kuwa ni watoa huduma wa kisasa kwa wakulima. Jionee:

Mengine tutaendelea kuwaletea.

Hongera Bashe, Hongera Rais Samia.

===
Waziri Hussein Bashe amezindua kituo cha kidigatali cha kuhudumia wakulima, ambao kituo hicho kitasaidia kuwa unganisha wakulima na maafisa ugani walioko katika maeneo yao.

Wakulima wanatakiwa watumie namba ya kituo ambao watumishi wa wizara ya Kilimo watawaunganisha na maafisa ugani. Aidha vituo vya huduma kwa wateja vitakuwa vinapokea malalamiko mengine yote na kuelezea hali ya soko.
 
Kituo cha huduma kwa wateja kinamsaidia nini mkulima anaetegemea mvua na mbolea isiyo na bei ya kueleweka?

Kituo cha huduma kwa wateja kina msaada gani kama mkulima analima kisha anapangiwa bei ya kuuza ama anazuiliwa asiuze mazao yake nje ya nchi?

Ama mkulima anakua anapiga simu anauliza kama shamba lake limejaa magugu, je ayapalilie ama anachome anapewa majibu wa desk officer farmers wa ofisi?
 
Mkulima wa Tanzania sasa hivi ana kituo cha kisasa cha huduma kwa mtej (,Customer care).

Bashe kwa mara ya kwanza Tanzania, anaifanya Wizara ya kilimo kuwa ni watoa huduma wa kisasa kwa wakulima. Jionee:

Mengine tutaendelea kuwaletea.

Hongera Bashe, Hongera Rais Samia.
Hizi ndio swagwa za kuwadanganya wajinga? Pitia pitia machapisho kule Misiri uonr nini maana ya Mapinduzi ya Kilimo, Bashe na Mama wanacheza na akili za wajinga
 
Subiri kijana, sasa hivi kuna zaidi y shamba darasa, ufundishwe kulima halafu usifunidishwe masoko? Usifundishwe wakulima wanavyoumizwa? Utakichukia kilimo. Bashe anafanya kweli, kionee darasa hilo:

Hao wali Dhulumu wako mtaani wana liona jua? Sarakasi za kijinga hizi
 
Hizi ndio swagwa za kuwadanganya wajinga? Pitia pitia machapisho kule Misiri uonr nini maana ya Mapinduzi ya Kilimo, Bashe na Mama wanacheza na akili za wajinga
Kwa mara ya kwanza Tanzania tunayaona anayoyafanya Bashe kwenye kilimo yakileta tija.

Misri walitowa ardhi kuwapa wakulima bure?
 
Back
Top Bottom