Meli ya MV Spice Islander, yazama ikelekea Pemba; wengi wahofiwa kupoteza maisha

SlidingRoof, asante kwa updates zako, but it looks true that you are shallow with the number 2000. Don't amplify the number, give us what you exactly know! Again thanks n keep on updates us, i still have trust on you.
 
ewe sliding roof, nakuuliza tena, una uhakika watu zaidi ya elfu 2000 wamefariki?? Kama huna uhakika usidanganye umma ili kupata umaarufu kupitia vifo,,,, kuna thread kule habari na hoja mchanganyiko jamaa kasema ana uhakika waliokua kwenye meli ni watu 610, coz ndo tiketz zilizokatwa,,, hawa 2000 wanatoka wapi jamani?????? Source yako ni nini??? Ama ni wapi??

Hizo taarifa kama nilivyosema hapo awali ni estimates..inaweza ikawa less au sitoshangaa ikawa more

kwa taarifa yako nimepewa habari baba yake rafiki yangu na mdogo wake wamo kwenye hiyo meli

sasa unaposema habari za kutaka umaarufu mie wa nini kwenye janga kama hili?
 
wwakuu mbona tunaangalia taarifa za habari hamna kitu kama hicho?
Kwa hiyo kama wewe kama uoni kwenye taarifa basi hamna ajali? Ulazimishwi kukubali endelea kusubili taarifa ya habari watu wote wanaochangia ni wajinga wewe ndio mjuaji?
Miafrica bana
 
hivi helcopter za police ziko wapi?mm huwa naona zikimtembeza mwema tu. Ilitakiwa zikaokoe watu.
Hili serikali bana hovyoooo.
 
Taarifa zimenijia hivi punde kuwa watu 2,000 (hakuna mwenye idadi kamili lakini namba hiyo ndio inayotajwa) wahofiwa kupoteza maisha yao baada ya Meli kuzama ikiwa inaelekea Pemba from Unguja kwenye mkondo wa Nungu.

Sasa wakati janga kama hili linatokea huwa kunakuwa na idadi mbali mbali zinatolewa lakini mimi nimeambiwa namba hiyo na watu wa 5 todauti toka sehemu mbali mbali kuanzia bandarini mpaka waliosindikiza jamaa zao ( ila kama namba kamili ikiletwa na serikali basi tutarekebisha tuu hivyo tunaomba coordination ya members)

Meli ilianza kuzama kiubavu na imechukua muda kuzama.

Inasemakana (from redio) sababu ilikuwa imejaa mizigo na abiria.

Kawaida Unguja meli huwa zinaondoka Gatini zikishapakia na kukaa nje huko karibu na kati ya bahari mpaka muda ndio safari zinaanza

Watu waliokolewa (sijajua na nani) hawafiki 25

watu wengi walikuwa watoto waliokwenda Unguja kula Iddi na walikuwa wanarejea kwani wiki ijayo baadhi ya skuli zafunguliwa

As I write kuna mmoja kati ya mabaharia kasimama juu ya meli ambayo inazama na anasema mawasiliano yanaweza kukatika at anytime kwani naye anaweza kuzama.

Kama ZANTEL au vyombo vya habari na wasiliano wanauwezo wawasiliane na idara za uokozi kama JWTZ ili wapeleke helicopeter zao za kuokoa.

Lakini mtu kama KETAN na wengineo anaweza kutoa helicopter zake atoe wakiokolewa hata watoto 20 si haba ni uhai

Inasemekana kuwa speed boats zingine zinaelekea eneo la tukio

Point of notice: Daftari la idadi ya abiria halipo so haijulikani wangapi wamo mle japo namba ni hiyo 2,000 sasa nadhani kwa mpango huo na kwa namna tunavyo operate Nyumbani nadhani itakuchukua siku kadhaa kujua namba halisi (kama daftari na copy za risiti hazitopotea)


Tunaomba updates coordination toka kwenye websites za:

JWTZ
JESHI LA POLISI
OFISI YA WAZIRI MKUU
OFISI YA USALAM WA TAIFA
WIZARA YA USAFIRISHAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI

mwenye habari zaidi tunaomba kama kutakuwa mwenye nafasi aanzishe facebook au social network pages atupe updates. Mwanakijiji hebu wacheki CNN, Invisible akiamka na wenzie watauleta updates zaidi

Kama kuna mwenye updates zingine anaweza kuzipost kwenye FACEBOOK PAGE hii
Zanzibar Ferry Accident - Wall | Facebook
najua haikatulia lakini nadhani anyone can post updates hapo
InshaAllah nitaendelea kuwahabarisha kadri muda unavyozidi kwenda


ngoja tusubiri nazi yetu kama itaahirisha safari ya kwenda kunywa kahawa na Bush Washington
 
SlidingRoof, asante kwa updates zako, but it looks true that you are shallow with the number 2000. Don't amplify the number, give us what you exactly know! Again thanks n keep on updates us, i still have trust on you.

Hakuna anayejua namba kamili lakini sources zangu including wafanyakazi wa pale bandarini, ndugu waliosindikiza jamaa zao na wengine wameirusia sana hiyo namba na kwenye matangazo ya redio yule baharia aliyekuwa anaongea alisema kuwa namba ndio hiyo

lakini nadhani bora tukafanya subra na kusikiliza kama kutakuwa na habari zaidi juu ya hili tukio
 
wwakuu mbona tunaangalia taarifa za habari hamna kitu kama hicho?

Vyombo vya habari vya TZ VIMELALA SAAANA. Breaking news za mwanzo nimesikia CLOUDS FM mida hii, na walitoa saa moja kamili ktk kipindi chao cha habari za asbh jumamosi....., maiti wanapelekwa viwanja vya maisara kwa utambuzi , hospitali imejaa...., na watu ni wengi...!
 
Kwa hiyo kama wewe kama uoni kwenye taarifa basi hamna ajali? Ulazimishwi kukubali endelea kusubili taarifa ya habari watu wote wanaochangia ni wajinga wewe ndio mjuaji?
Miafrica bana

mkuu unaniandama sana safari hii,kwwa nini??kumbuka usemi wa yule jamaa,tunajenga nyumba moja tusigombee fito
 
tz bado tunapigania utawala bora. Mambo kama ya kukabili na kujikinga na ajali yatakuja baadaye. Sidhani kama serikali ya magamba huwa inawaza ajali sababu wao na watoto zao na kampani zao wengi hutumia ndege kwenda huko zenj au pemba. Poleni wa zenj.
 
mmh huu utakuwa uzushi bwana mimi nimewahi panda hiyo meli haiwezi kubeba idadi hiyo lasivyo itazama hata kabla haijaondoka

Yaani watu ndani hakukaliki ni majonzi tuu kwa watu na wapo kwenye makundi makundi wakiwa wanasikitika na kufuatilia zaidi habari, nipo Pemba na nimepita Chake sio muda mrefu.
Tanzania uokozi wake ni wa zima moto na mimi binafsi sijaona usafiri ulio mbovu kama wa Pemba, ni balaa tupu. Kwanza sio wa kuaminika na ni mbovu mno.
Tanzania inahitaji kulitazama kwa upya hili suala la usafiri wa Pemba.
Mungu awaponye haraka walionusurika na RIP kwa waliofariki.
 
Haya! Mi nasubiria details za kushiba ili niweze kuongea lakini mpaka sasa moyo umesizi kabisa na inasikitisha sana. Na na wapawa pole ya moyo kwa waathirika wote!
 
Kweli ule mkondo wa nungwi ni balaa meli iliyokuwa inaweza kuuhimili ni marehemu mv mapinduzi lakini hizi meli za kuungunga tu ndio madhara yake. Mungu atupe subra kwani nami wamo jamaa zangu waliotoka kula skukuu.

nakumbuka sana nilivofika mahala nikashindwa kukaa kwenye kiti, ikabidi nikae chini. ghafla nikatapika.

mara tukatangaziwa hali ni mbaya "tuombe Mungu".

Injini moja ikazimimwa. (nafikiri kwa waliopanda Sepideh watakubaliana na mimi kwamba ni moja ya boti zenye nguvu na zinazoaminika, nafikiri ndicho kilichotuokoa. wala sipigii debe Sepideh, ni ukweli)

Ile sehemu haifai kwa meli zisizo na nguvu.
 
This is so depressing. 2 of my friends wako mle

jamani mtaniwia radhi. Endeleeni mimi natoka kidogo
 
Hizo taarifa kama nilivyosema hapo awali ni estimates..inaweza ikawa less au sitoshangaa ikawa more

kwa taarifa yako nimepewa habari baba yake rafiki yangu na mdogo wake wamo kwenye hiyo meli

sasa unaposema habari za kutaka umaarufu mie wa nini kwenye janga kama hili?
sawa mkuu,,, hakuna haja ya kubishana sana kwa sasa,,, kama great thinkers, lets wait kwa hiyo idadi kamili,, tuzidi kuwafariji ndugu zetu walioptwa na msiba huu,,, pole zangu za dhati pia kwa rafiki yako ambaye baba yake na mdogo wake pia walikuwepo kwenye meli hiyo
 
mkuu unaniandama sana safari hii,kwwa nini??kumbuka usemi wa yule jamaa,tunajenga nyumba moja tusigombee fito
Mkuu, Director1, tupo pamoja ndugu ya nimekupata sote tunajenga nyumba moja
 
Updates:

Zenji Radio kuna vyombo vya uokozi; boat, helkopa na watu hai zaidi ya 150 wameokolewa
 
Back
Top Bottom