Meli ya MV Spice Islander, yazama ikelekea Pemba; wengi wahofiwa kupoteza maisha

ALAANIWE MALARIA SUGU; PAMOJA NA UZAO WAKE, milele na milele ijayo,,,haiwezekani kwenye national tragedy kubwa kama hii unaongea ujinga,,,, mods piga ban,,,, anakera sana,,, watu wana majonzi na simanzi moyoni, wewe unaleta mambo ya ajabu??
 
na mpaka sasa inasemekana kua idadi ya abiria 610 ndio waliyokata tocket..mbali wale walodandia..
 
msiba mzito waikumba ZANZIBAR usiku wa kiamkia leo jumamosi, meli ya mv spice IMEZAMA katika mkondo wa nungwi ikielekea kisiwa cha pemba usiku wa kuamkia leo, katika abiria 610 waliopanda meli hiyo mpaka sasa wameokolewa 20 tu, huzuni na vilio ndivyo vilivyotawala katika mitaa ya ZANZIBAR, innalillahi waina ilayhi rajiun
 
Jukwaa la Siasa ni leading forum hapa JF Huu mchezo wa INVISSIBLE kuminya uhuru wa maoni umechelewesha habari hii muhimu na kuwavunja nguvu waliokuwa wanasaka details hizi za ajali kwa manufaa ya Umma. Sasa zimebaki kuwa habari zao binafsi. Forum imepoteza maana ya kuwa forum.UTATHIMINI UPYA UTARATIBU HUU MKUU
Mungu awalaze pema waliotangulia katika HAKI.
 
Poleni sana waathirika wa ajali hiyo mbaya.

Lakini niko makini sana kujua ya kwamba karibia miaka 15 tangu MV Bukoba iwauwe Wa-Tanzania wenzetu kibao kule kanda ya ziwa, je serikali yetu imewekeza kiasi gani katika shughuli zote za uokozi pindi ajali kama hii inapotokea??????

Au mambo ni yale yale ya tangu miaka ile????????????
 
ewe sliding roof, nakuuliza tena, una uhakika watu zaidi ya elfu 2000 wamefariki?? Kama huna uhakika usidanganye umma ili kupata umaarufu kupitia vifo,,,, kuna thread kule habari na hoja mchanganyiko jamaa kasema ana uhakika waliokua kwenye meli ni watu 610, coz ndo tiketz zilizokatwa,,, hawa 2000 wanatoka wapi jamani?????? Source yako ni nini??? Ama ni wapi??
 
Natamani kuona reaction ya serikali ktk hili, hasa kwa kuwa serikali yenyewe ni ya "umoja" na waziri ni wa "upinzani". Au ndo tutasikia hadithi zile zile "sitoki hadi anitoe aliyeniweka, kwanza mie sio nahodha". Ni haki kuliangalia suala hili ktk mapana yake. Yaani mizizi, shina, matawi hadi majani.
 
watu wamejazana hapa hospitali kuu ya mnazi mmoja lakini taarifa imetolewa watu wakasubiri viwanja vya mnazi mmoja maiti zitapelekwa hapo. Kwa kweli watu tuwe na subira msiba ni mzito.
 
Ni hofu, huzuni na majonzi, zimetanda huku pemba. Mimi naishi huku Pemba nimepata taarifa tangu saa tisa usiku za ,redio ZENJ FM, ESQUAMA Vimekuwa vikitoa taarifa hizo kweli ajali imetokea na asubuhi hii wanasema KMkM (jeshi la kujenga uchumi zanzibar) wapo ktk eneo kwa uokozi na baadhi ya miili imesha na hiyo meli sasa inasukumwa na mawimbi kuelekea Tanga. serikali lazima iwajibike kwani Pemba imesahaulika katika kila sekta kama vile hakuna watu.

MUNGU KTK CHRISTO YESU AWAFARIJI WENZENTU WALIOFIKWA NA MSIBA HUU MKUBWA
 
mmh huu utakuwa uzushi bwana mimi nimewahi panda hiyo meli haiwezi kubeba idadi hiyo lasivyo itazama hata kabla haijaondoka
 
Vyombo vya habari vya Tanzania bado vimelala, kuna jamaa yangu kaondoka asubuhi hii kwenda Unguja ameniambia mpaka saizi maiti zaidi ya 30 zimeishapatikana.
Na watoto wake wakiwemo walikuwa likizo unguja. Poleni sana Wazanzibar


kwanza ilibiruka kwa mbele. then watu waliokuwa juu na waojua kuogelea wakaa juu ya boti, then ikaanza kuzama taratibu......, more than 2000 pple have been confirmed to death. Ni msiba mkubwa kwa wazenj na Tanzania kwa ujumla.Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi.
 
mmh huu utakuwa uzushi bwana mimi nimewahi panda hiyo meli haiwezi kubeba idadi hiyo lasivyo itazama hata kabla haijaondoka
mkuu nakuunga mkono mia ya mia,,,, watu 2000 wataingiaje kwenye ile meli,,, huyu sliding roof ni muongo sana,, anabandika tu idadi yoyote hapa kama anavyojisikia,,,source of information anakwambia ndugu yake alieko zanzibar,,,??? Huu si uzandiki huu
 
Source RFA.

Ilikuwa ikisafiri kutoka Unguja kwenda Pemba.

Nilishawahi kupita pale na Sepideh.

Ni noma.

ukipita salama shukuru Mungu.

Kweli ule mkondo wa nungwi ni balaa meli iliyokuwa inaweza kuuhimili ni marehemu mv mapinduzi lakini hizi meli za kuungunga tu ndio madhara yake. Mungu atupe subra kwani nami wamo jamaa zangu waliotoka kula skukuu.
 
NImesikia Asubihi from Radio One kwamba watu 100 wamefariki and more info to come abt the sad story of sinking boat
 
Poleni sana wenzetu mliofiwa!utawaona hawa viongozi watakavyoshtuka usingizini nakuanza kupayuka!shame on them
 
Poleni sana ndugu zetu wa visiwani, hili ni pigo kubwa kwa familia zetu wote watanzania
 
Back
Top Bottom