Meli ya MV Spice Islander, yazama ikelekea Pemba; wengi wahofiwa kupoteza maisha

BinMgen

JF-Expert Member
Jun 18, 2008
1,844
245
kunataarifa meli ya abibiria (spice) itokayo Unguja kwenda Pemba imezama katika mkondo wa Nungwi mwenye taarifa kamili atuwekee.

spice.jpg

mv_spice_islander.jpg


Updated Posts:
_________

TAARIFA RASMI: Waliookolewa jumla yao ni 545 ambapo Sea Express iliokoa 292, Super Sea Bus iliokoa 198 na Boti ya KMKM iliokoa watu 55.


source Jussa
_________

Tunawashukuru sana kuwa kutupa mkono wa pole wana JF,tumepata pigo kubwa sana ambalo halijawahi kutokea,hivi hebu liangalieni hilo meli ni kweli la kupakia abiria ?

Hivi viongozi wetu wapo au wamelala,leo hii wametupa msiba mkubwa sana,tumepoteza vipenzi vyetu,ndugu zetu,watoto wetu,wazee wetu,inshallah allah atatulipia,mungu awalaze pema walifariki katika ajali hii ameen, na awape uzima wale walijeruhiwa ameen.
attachment.php


attachment.php


attachment.php


__________
Updated images by member:

attachment.php


attachment.php


attachment.php


attachment.php
__________

Mh. Kikwete katangaza siku3 za maombolezo na bendera zitapepea nusu mlingoti na amefuta ziara yake ya kwenda canada,pia dr. Shein katangaza maombolezo yasiku3 zenj kwamsiba huu mkubwa wazaidi ya watu 1000, Innalilahi waina lilahi raajiuun.

__________

hadi hivi sasa 620 wameokolewa, 189 wamefariki. uikoaji bado unaendelea.

__________

Kwa hisani ya ZANTEL Zanzibar Update

LIST OF SURVIVORS

Zantel offers its deepest condolences to the Nation and all those affected.

In the interest of the general public, Zantel will be constantly updating this page with the list of Survivors as soon as we have more information.

*Update as per Mnazi Mmoja Hospital

ORODHA YA WALIONUSURIKA
Zantel inatoa salaam za rambirambi kwa wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika janga hili.

Katika jitihada za kusaidia umma kwa ujumla, Zantel itakuwa ikitoa orodha ya majeruhi kadri ya majina yatakavyopatikana.

*Orodha hii ni kama inavyotolewa na Hospitali ya Mnazi Mmojas.

ORODHA YA WALIONUSURIKA HAPA!

_________

DKT BILAL, ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA MELI ZANZIBARMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Ally Amour wakati alipofika kumjulia hali mtoto Said Gerald (6) aliyenusurika katika ajali ya Meli eneo la Nungwi usiku wa kuamkia leo, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Aliyempakata ni mama yake mzazi, Mariam Hemed.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Baada ya hapo Makamu wa Rais alitembelea katika Viwanja vya Maisala na kutembelea shughuli za kiusaidia na kutambua maiti waliopatikana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


_________
 

Globu

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
8,376
1,792
Meli inayoitwa MV SPICE imezama ktk mkondo wa Nungwi. Ilikuwa inatokea Unguja kwenda Pemba. Tusubiri habari zaidi.
 

Derimto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
1,307
303
Jamani kama ni tetesi tuambieni ki mtindo unaofanana na ukweli mnaleta vipisi mno imetokea lini na saa ngapi na inakadiriwa kuwa na watu wangapi na labda chanzo cha ajali ni nini?
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,160
50,566
Mkuu vuta subira sio tetesi ni kweli kabisa nimepokea call kutoka kwa bizness partner kuna ajali nungwi,call zipo busy sana ngoja nizidi kumtafuta

Jamani kama ni tetesi tuambieni ki mtindo unaofanana na ukweli mnaleta vipisi mno imetokea lini na saa ngapi na inakadiriwa kuwa na watu wangapi na labda chanzo cha ajali ni nini?
 

BinMgen

JF-Expert Member
Jun 18, 2008
1,844
245
Jamani kama ni tetesi tuambieni ki mtindo unaofanana na ukweli mnaleta vipisi mno imetokea lini na saa ngapi na inakadiriwa kuwa na watu wangapi na labda chanzo cha ajali ni nini?
<br />
ni usiku huu, yaani hivi sasa 4.15 am watu wanaelekea bandarini. inasemekana imeshabiruka kunawatu wachache wako juu
 

Globu

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
8,376
1,792
Ni kweli meli imezama wala sio tetesi. Imezama sio mbali sana na mji wa Nungwi. Mpaka sasa watu 25 wameokolewa. Inasemekana ilikuwa na zaidi ya watu mia. Tusubiri taarifa zaidi.
 

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,547
776
watu wote Unguja wako macho sim zinacheza tuu. wametoa info kwenye redio kuwa sababu ni abiria walikuwa wengi na mizigo pia.

Meli inamalizika kuzama as I type , Speed boats ndio zinaenda sasa kujaribu kuokoa sijui itakuwaje

JWTZ kwa nini wasipeleke helicopter zao?

Pinda na ofisi wa Waziri Mkuu mko wapi?
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,160
50,566
Tusubirie wakubwa wa JF waamke,Zaidi ya Abiria 2000????? mmmhh hiyo meli imeeizidi Mv bukoba kweli????
 

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,547
776
Tusubirie wakubwa wa JF waamke,Zaidi ya Abiria 2000????? mmmhh hiyo meli imeeizidi Mv bukoba kweli????

Yani TV zote nafungua hapa sioni hata breaking news. najaribu kufungua radio nasikia miziki tu. halafu wanasema wamepiga hatua kwenye habari. hamna lolote uzembe tu.


Hamuwezi kuona kwa sababu vyombo vyetu vya habari na waandishi wetu wote ni uchwara

Last time I checked newsroom huwa hazifungwi lakini no onebothered even to update their website

Si IKULU
Si JWTZ
Si PM OFFICE
Si POLICE FORCE

JF ndio usisaeme. Invisible na hao watu wake wasiojulikama (mods) wame prove kuwa they are abunch on amateurs
kwa nini invisible asichague Mods From Australia, Tanzania, Middle East, Europe na USA ili waendane na time zones?

I'm just disgusted na news flow

sie wengine tuna jamaa zetu unguja na Pemba sasa hivi the only place watu wanaweza kupeana news ni kupitia social networks kama Facebook (kupitia simu) au sms

ZANTEL wamelala nao kwani this would have been the moment wakatoa specia numbers ili watu wapate kuwasiliana na jamaa zao at zero tariff etc
 

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Bahati mbaya sana Mkuu INVISSIBLE nae alikuwa amelala, lakini hatuwezi kulaumu MEDIA kwani hii pia ni Media kama zilivyo nyingine tena iliyo huru kuliko za wanasiasa licha ya Utaratibu huu kandamizi wa sasa wa kutaka kwanza bwana mkubwa ajiridhishe ndio apost (unaua forum yako)

Nimezungumza na Mkuu wa Kikosi cha Uokozi Zanzibar...Manusuara waliokuwa juu ya Meli wameokolewa na jitihada zinaendelea kuwatafuta manusura zaidi. Kama Post nyingine inavyosomeka hapo chini kabla ya KUEDIT Hii post, hali bado ni ya sintofahamu kubwa kwa sasa.

Tunasubiri details nyingine tuzipost hapa ili kujua hasa maafa ya Tukio hili la kusikitisha sana

Idadi ya Maiti so far wamefika 51 na waliokolewa 253, Inasadikiwa Meli ilikuwa na Abiria 610

Mungu zilaze pema peponi Roho za waliotangulia katika HAKI....Amen
 

BinMgen

JF-Expert Member
Jun 18, 2008
1,844
245
watu wote Unguja wako macho sim zinacheza tuu. wametoa info kwenye redio kuwa sababu ni abiria walikuwa wengi na mizigo pia.
Meli inamalizika kuzama as I type , Speed boats ndio zinaenda sasa kujaribu kuokoa sijui itakuwaje
JWTZ kwa nini wasipeleke helicopter zao?
Pinda na ofisi wa Waziri Mkuu mko wapi?
Ikowapi helicopter iliyotumika 2001 kuwauwa wapemba ktk maandamano, kwanini leo istumike kuwaokowa nduguzetu hawa jamani?
 

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
892
Vyombo vya habari vya Tanzania bado vimelala, kuna jamaa yangu kaondoka asubuhi hii kwenda Unguja ameniambia mpaka saizi maiti zaidi ya 30 zimeishapatikana.
Na watoto wake wakiwemo walikuwa likizo unguja. Poleni sana Wazanzibar
 

Nyota Ndogo

Senior Member
Aug 7, 2011
150
33
Source RFA.

Ilikuwa ikisafiri kutoka Unguja kwenda Pemba.

Nilishawahi kupita pale na Sepideh.

Ni noma.

ukipita salama shukuru Mungu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

9 Reactions
Reply
Top Bottom