Madereva Pemba wakerwa tabia ya Wanafunzi kupuuzia honi barabarani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Madereva wa vyombo vya moto Kisiwani Pemba, wamewataka wanafunzi kutodharau honi wanazowapigia au miungurumo maalum ya mashine, ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Wamesema, wanafunzi wengi wamekuwa na tabia ya kudharau honi au mivumo isiyokuwa na kawaida, wanayoifanya ili wakae pembeni, jambo ambalo linaweza kuleta madhara.

Wakizungumza na mwandishi wa habari eneo la Ngwachani, ambapo dereva mmoja aliyekataa kutaja jina lake, alipoteremka kwenye gari, kuwaelimisha wanafunzi waliodharau honi aliyowapigia mara tatu.

Alisema alilazimika kuweka gari pembeni na kuwapa maneno makali kundi la wanafunzi, baada ya kuwapigia honi na mivumo mikali ya mashine, bila ya kujali.

Dereva huyo alieleza alikuwa amebeba mzigo akitokea bandarini Mkoani, alipofika karibu na njia ya Tangaani, aliwapigia honi wanafunzi, ili wakae pembeni, ingawa hawakutii.

‘’Mbele yangu kuna gari mbili za abiria zinafukuzana zikitokezea mjini Chake chake, na upande wangu kuna kundi la wanafunzi kama 15, niliwapigia honi cha ajabu, hakuna hata mmoja aliyegeuka nyuma,” alisema.

Kwa upande wake dereva Ali Omar Ali wa gari ya Chake chake-Mkoani, alisema wanafunzi wenye tabia hiyo, hasa ni wa skuli zenye sekondari na zaidi wale wa kike, ndio ambao wamekuwa wakidharau honi.

‘’Wale skuli za msingi ukiwapigia honi au gari ukiibadilisha mvumo wanakaa pembeni haraka, lakini hawa wakubwa ni wajeuri na wakati mwengine, inatubidi sisi tuwakwepe wao,’’ alieleza.

Kwa upande wake dereva wa gari ya abiria, Hussein Kassim Omar alisema, kisheria wanafunzi wanapotembea iwe kwenda ama kurudi skuli, wavielekee vyombo vya moto na siku kuvipa mgongo.

Mwanafunzi mmoja Nassor Haji Ali, alisema kinachojitokeza ni kutokana na kukosekana kwa miundumbinu rafiki, ya watembea kwa miguu kwenye Barabara Chake chake - Mkoani.

Naye, mwanafunzi Aisha Khamis Adam, amesema sio kweli kuwa wao wamekuwa wakidharau honi, bali wakati mwingine madereva, wanakuwa wanawapigia karibu yao, pasi na dharura.

‘’Lakini madereva wengine hutupigia honi sisi wanafunzi wa kike, kama ishara ya kuanza kwa mahusiano ya kimapenzi na mmoja kati yetu, na hasa wanaemjua,” alieleza.

Hata mwanafunzi Mwajuma Daudi Mohamed alisema wamekuwa wakiziheshimu mno honi na mivumo ya gari, isiyo ya kawaida, ingawa shida ni madereva kutopunguza mwendo wanapowaona wanafunzi.

‘’Kama madereva wanafukuzana huko wanakotokea, hata wakikuta kundi la wanafunzi, hawapunguzi mwendo, sasa hili ni tatizo kwao na sio sisi,” alieleza.

Hivi karibuni Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Kusini Pemba kutoka Jeshi la Polisi, Shawali Abdallah alisema wameshazimaliza skuli zote za msingi na sekondari, kuwaelimisha wanafunzi, matumizi sahihi ya barabara.

‘’Tumeshapita skuli zote za mjini na vijijini, kwa zile ambazo wanafunzi wanapita kwenye barabara kuu, kuwa wanapokwenda ama kurudi gari, wawe wamezipa uso gari, hii inaweza kuwa rahisi chombo kikipata hitilafu, kukimbia,” alieleza.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amewakumbusha madereva, kuendelea kuheshimu sheria za usalama barabarani.

Katika kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2020 kikosi cha Usalama barabarani, kilifanikiwa kukamata makosa madogo ya Usalama barabarani 2,152,533 ikilinganishwa na makosa 2,311,538 yaliyokamatwa kwa mwaka 2019.

Kwa upande wa Zanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi uliongoza kwa matukio ya aina hiyo 7,031 na Mikoa iliyokuwa na idadi ndogo ya matukio ilikuwa ni Kaskazini Pemba 1,512 na Kusini Unguja 2,154.

Matukio ya usalama barabara kwa 2019, yaliripotiwa 104, yakisababisha majeruhi 290 na mwaka 2020, kulikuwa na watu 124 waliofariki, na majerehi 2092.

Ingawa pia ripoti hiyo ya Jeshi la Polisi Tanzania, ya mwaka 2020, iliripoti ajali 1,133 za piki piki, zilizosababisha vifo 744, sawa na majeruhi 948 kwa Tanzania yote.

Source: Pembatoday
 
Kiuendeshaji kistaarabu, honi ni kwa ajili ya kumstua mtu ambaye hajaona ujio wa chombo husika. Nje ya hapo honi inakuwa ni fujo tu.
 
Back
Top Bottom