watu wanajadili vitu vya maana kama ubovu wa meli we unatangaza eti nguo zimekauka nani ana nguo?
NI UJINGA! IWEJE BOTI ZA UOKOAJI ZIKAE BILA MAFUTA? Mbona magari ya maofisi hayaishiwi mafuta!
Na wewe na imani hizo bado tu.. haya Mumiani kataka kafara zake, Zanzibar haiwezi kuwa huru hadi hesabu ya vifo fulani itimie maana meli zote zinatoka Pemba kwenda Unguja..
Ndio watanzania wanazipenda hizo. Hawana time na unayowaza. Mbunge mmoja amewahi kutahadharisha hili kuwa "NCHI INAPOTEZA NGUVU KAZI KWA STAREHE, ANASA NA KUKAA VIJIWENI. Wengine wanaripoti bar tangu asbh..." Hawa ndio wateja wa hizo media.
Tuone tulichojifunza kutoka MV Spice Islander.
Asante kwa ufafanuzi wako japo kwa shingo upande. Kwa vile boti ilikuwa inatokea Dar mamlaka inayopaswa kuikagua ni sumatra, km ingekuwa inatokea Zenj bado hiyo ZMT ndiyo nayo ingefanyia ukaguzi boti au meli yoyote inayoondokea huko. Hivi ndivyo mimi huwa naona wanafanya kila nisafiripo kati ya zenj na bara.Mkuu taratibu najua katika hali kama hii watu huhamaki na matokeo yake unaweza kuelekeza SHUTUMA kusiko. SUMATRA jurisdication yao mwisho ni Chumbe (kama wapendavyo kusema wa-ZNZ).
SUMATRA hairuhusiwi ku-operate ZNZ. ZNZ kuna chombo kingine kabisa kinaitwa ZMT(?)
Haya bana sikujua kama nawe mwarabu wa Pemba! Tall yuko mjini...Mimi sina imani hizo, cacico anajuwa kwanini nimemwambia ani pm, waarabu wa pemba twajuana kwa vilemba.
Kweli serikali imejifunza kitu muhmu sana kwa ajali za Mv Bukoba na Spice Islander. ilichojifunza ni kuwa mel ikizama ni bora watu wazikwe humo humo ili kuondoa usumbufu wa kuwaopoa na kuwazika ardhini. Ngoja uone na hii, lazima waiache izame yote ili iwe kaburi la watu wengiSasa mbona mnatuchanganya, hapa mnasema MV Seagull, kule kwa Michuzi blogspot analipuka kivyake anasema MV Skaget. Tuamini lipi. Anyway, serikali ilijifunza chochote kutokana na ajali ya MV Bukoba na MV Spice Island??? MICHUZI: BREAKING NYUUZZZZZZZ........: MELI YA ABIRIA YA MV SKAGET ILIYOKUWA IKIELEKEA ZANZIBAR YAPINDIKA NA KUZAMA MUDA HUU
:A S-confused1: :banplease:Ni pm tutaongea zaidi, usijali.