Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wataongezewa posho ya shilingi elfu hamsini (50,000) ya nauli ili kuleta ufanisi katika kazi na kurahisisha masuala ya usafiri kwa ajili ya nauli za kwenda kazini na kurudi nyumbani ambapo tayari shilingi Bilioni 34 zimetengwa kwa ajili ya posho hiyo kwa Watumishi wote wanaostahili kupewa.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) zilizofanyika uwanja wa Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali imejipanga kutengeneza ajira laki tatu (300,000) kwa Wananchi wake kwa mujibu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ambapo amesema katika kipindi cha miaka mitatu Serikali kupitia shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ajira mpya zipatazo 187,651 zimepatikana sawa na asilimia 104 ya lengo la ajira 180,000 kwa miaka mitatu iliyopita.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha inaongeza fedha kwa ajili ya posho ya likizo ambapo zimetengwa shilingi bilioni 2.5 katika bajeti mpya ya mwaka.
Millard Ayo
===
Wabara tuendelee kusikilia mchongo..... ni huzuni kwakweli. Halafu kuna watu wanapiga mabilioni ya pesa wala hawachukuliwi hatua ndio kwanza wanahamishwa kwenye vitengo vingine, kwakweli job true true!
===
Pia soma:
Dkt. Mpango: Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake