tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,246
- 4,467
Mimi sio mtaalamu wa historia, ila kwa historia yangu ndogo niliyopata O-level ninaamini Tanganyika chini ya Ujerumani ingekuwa Taifa kubwa sana hapa Afrika zaidi ya hapa ilipo leo. Waliotuharibia walikuwa Waingereza waliokabidhiwa taifa leo. Hatukupaswa tuwe marafiki na waingereza. They were hopeless.
Nafikiria jinsi Ujerumani ilivyoendelea. Jinsi wajerumani wanavyofanya kazi kwa bidii. Nafikiria infrastructures walizojenga ambazo hadi sasa zinadumu. Hebu fikiria reli zetu. Hivi Tanganyika leo tungekuwa wapi tungeendelea kutawaliwa na waingereza. Naamini wangetunyorosha akili zetu - Tungekuwa mbali sana kifikra, kiuchumi na tusingekuwa wavivu kama sasa. Hofu yangu kubwa ni labda kukosa uwezo wa kumiliki ardhi. Lakini ardhi ya nini wakati mataifa yenye barafu kama Ukraine na Russia bado tunategemea toka kwao Chakula.
Tukumbuke tu kwamba kabla Ujerumani haijanyang'anywa eneo lake lililohusisha Tanganyika tarehe 7 Mei 1919, na kupewa Uingereza, eneo la maziwa makuu tulikuwa chini ya himaya iliyoitwa German East Africa (GEA) lilokuwa ni eneo linalohusisha nchi za sasa za Tanganyika, Burundi, Rwanda, na sehemu ndogo ya Msumbiji huku makao yake yakiwa Bagamoyo (1885–1890) kisha yakahamia Dar es Salaam (1890–1916) na kwa muda mfupi yakaenda Tabora (1916).
Mwingereza alituharibia sana.