Tatizo waislam wengi hawaelewi quran ndio maana kuna mikanganyiko mingi. Ukisoma suratil Baqara 2:62 inaeleza wazi kwamba wayahudi na Waksrito na Wasabai na yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu watalipwa kwa mazuri waliyoyafanya.
2: 62. Hakika Walio amini, na Wayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye
muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa
yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.
Tatizo hizi hadithi ambazo Mungu kazikataza kwenye Quran ndio tunazifua kuliko Quran . Kwa mfano hakuna sehemu kwenye Quran imesema watu wakienda hija wampige shetani mawe. Quran iko very clear tujiepusha na mawe au masanamu lakini kwasababu watu wameiacha Quran nakufuata hadith unaona wanaenda kubusu na kulishika lile jiwe jeusi. Ukisoma Quran Surat Baqara, Surat Maida na Surat Hajj inaelezea hija yote na mambo gani yakufanya ukiwa Hija. Na hilo la kumpiga shetani mawe sijui wamelitoa wapi sababu Quran inasema majini na mashetani wameubwa kwa moto kwa hiyo huwezi kuwadhuru kwa kutumia vitu kama mawe, silaha etc.