ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Hakika tunampenda sana binti yetu wa miaka mitatu(3). Karibia kila mtu akimuona ana msifie kuwa ni binti mzuri sanaaa wa sura (cutie) . Kwa kuwa rafiki yangu mmoja aliwahi kulieleza madhara ya kuweka sura/picha ya mtu kwenye mitandao ya jamii kama Facebook (FB), nilimuasa mke wangu asithubutu kufanya hivyo hata kidogo nami nimekuwa makini kuepuka kufanya jambo hilo kwa lengo la kumlinda mtoto ili akikuwa awe na ridhaa yake kuweka hadharani picha zake. Siku zote najaribu kumkumbusha "mai wifu" kuhusu ili na amekuwa akinijibu "yeye si mjinga wa kufanya mambo tunayoshaurina asifanye na kwamba yeye hata anwani ya barua pepe hana, na hataki kusikia kabisa vitu kama FB".
Lakini nasikitika sana, leo nimepokea mwaliko kutoka kwa rafiki mmoja katika familia yetu kupitia anwani yangu ya barua ya yahoo kunitaka nijiunge na Facebook. Baada ya kupokea mwaliko huo na kuingia kwenye FB, nakuta miongoni mwa marafiki zake ni mama watoto wangu na kwenye "wall" ya "mai wifu" na pia ya rafiki yangu huyo kuna picha kibao zikiwemo zangu na huyo mwanetu mpendwa ambazo nyingine sikumbuki hata zilipigwa lini.
Marafiki ambao wengine siwajui kabisa wameandika maoni meeengi (comments) kwenye "wall" ya "mai wife" wakimsifia yeye na mtoto jinsi walivyo wazuri wa sura na kufafana. Wengine wame "comment" kuhusu mimi wakisema labda si baba wa mtoto wanataka aweke picha halisi ya baba yake kwani mimi sifanani kabisa na mtoto na sina hadhi ya kuwa na mke kama huyo "maiwifu". Mbaya zaidi kuna mwengine ambao wana majina ya kiume (siwafahamu) wame comment mara kibao kuwa wanataka penzi la wifu na kuomba atoe namba yake kupitai email zao.....sijui kama ametoa au lah......
Nashindwa ni hatua gani nichukue kwa hasira nilizonazo leo!, sijamuuliza bado kuhusu ili.....