Ukiomba msaada humuoni mtu ila ukifa wanatoa michango ya maana!

Great YHC

Senior Member
Jan 1, 2024
167
596
_________________
Nyumba niliyo kuwa nikiishi ilifikia kipindi nilitaka kufukuzwa Ndani kwa kutokulipa kodi. Nikaamua kuwashirikisha marafiki hata na boss wangu pia, wote wakaanza kunikwepa. Nilivyoona hali hii nikaamua kushea na marafiki zangu Tatizo langu kwa kupost Facebook kutafuta msaada, lakini nilicho kipata ni likes 2 "na comment "0."
_
Nikaamua kutuma msg 250 kwa watu wangu wa karibu niliowasave kwenye simu, kuomba mkopo wa Tsh 600,000/=. Wakajibu watu 10 tu. Watu 6 kati ya hao waliniambia pole Sana, 10 walisema hawataweza kunisaidia. Mmoja aliamua kunisaidia kiasi kidogo sana na wengine 3 wakaniahidi, ila baadaye wakawa hawapokei hata simu zangu, mwisho nikafukuzwa kwenye nyumba.

Sikuwa na pakulala. Nikiwa nimechanganyikiwa natembea gizani mitaa ya Manzese, kibaka akanipora kibegi changu kidogo kilicho kuwa na vitambulisho vyangu, vyeti na simu. Akapotelea kwenye vichochoro sikumuona alipoishia. Kumbe huko alipokimbila alijaribu kuvuka barabara, akagongwa na kufa hapohapo.

Wapita njia wakaokota kibegi changu na kukuta vitambulisho na vyeti. Kale kasimu wajanja wakapita nako. Vyombo vya habari vikaripoti nimekufa, na ndugu zangu wakajulishwa kwenda kuchukua vitambulisho na vyeti vyangu.

Watu 300 wakaandika kwenye akaunti yangu ya Facebook jinsi walivyo nifahamu na jinsi nilivyokuwa mtu mzuri sana na mstaarabu. Kamati ya mazishi ikaundwa na rafiki zangu wakachanga Tsh 1,500,000 zakuweza kulisha watu kwenye msiba.

Wafanyakazi wenzangu wakachanga pesa za jeneza, viti na maturubai. Walipanga nizikwe kwenye Jeneza la Heshima la Tsh 3,000,000/=. Walipokwenda kununua, muuza Jeneza akawauzia kwa Tsh 2,800,000/=. Akatoa discount ya laki mbili kama mchango wake kwenye msiba wangu, kwa kuwa alikua rafiki yangu Facebook.

Familia wakakaa kupanga mazishi. Kikao cha kwanza tu wakachanga Tsh 3,000,000/=. Ndugu zangu kila mmoja alitaka kujionyesha kuwa yeye ni mchangiaji mzuri. Wakashindana kutoa mamilioni. Waka print T-shirts kwa Tsh 2,000,000/=.

Fikiria sasa picha iliyotokea nilipoamua kujitokeza siku ya mazishi yangu.

FUNZO:

Hivi ndivyo DUNIA ilivyo kwa sasa. Ni ukweli wa kusikitisha lakini ni moja ya maisha tunayoishi sasa hivi katika Jamii zetu kila siku. Wewe unaye soma hadithi hii badilika sasa na badili tabia yako.

Msaidie rafiki au ndugu yako wakati wa matatizo yake. Usisubirie kifo chake ndipo ukaonyeshe kujali. Haitasaidia kitu.

Mahatma Ghandi aliwahi kusema "The pain of caring is far less than the pain of regret" akimaanisha gharama za kuwajali wengine ni ndogo kuliko gharama za majuto kwa kushindwa kuwajali.

Yani kama mtu anahitaji dawa ya shilingi 5,000/= ili apone, na wewe unaweza kumsaidia lakini ukaacha kwa kuogopa gharama, utapata gharama kubwa zaidi za majuto ikiwa mtu huyo atakufa.!
 
Ila msiba wako pesa wanayo
Sasa mtu hulipi unamkopesha ya nini sasa ?
Huo si utakuwa ujuha ? huo msiba ni issue nyingine tu, ni kama mtu unamdai akaumwa na bado ukamchangia pesa ya matibabu.

Ila usipomkopesha mtu hatutarajii atakufa
 
Wakajibu watu 10 tu. Watu 6 kati ya hao waliniambia pole Sana, 10 walisema hawataweza kunisaidia. Mmoja aliamua kunisaidia kiasi kidogo sana na wengine 3 wakaniahidi, ila baadaye wakawa hawapokei hata simu zangu
Wamejibu kumi tu,

ila 10 walisema hawana msaada + 1 aliyesaidia + 3 walioahidi + 6 waliotoa pole = 20

Mtiririko wa visa ni mgumu sana kutokea kwenye maisha halisi, hii umetunga

Ila ni nzuri inafundisha
 
Kazini nimeshawapiga marufuku kuja kuniomba mchango wa Msiba na wananijua kabisa nilivyo mtata

Maana wakija kuniomba mchango wa msiba huwa nawauliza, "kwa nini hamkuchangisha wakati anaumwa mpaka mje mchangishe akiwa kishafariki?"

Sasa hivi hawaji, ila ikitokea mtu anaumwa ndo wanakuja kuniomba mchango

Na mimi huwa nawaambia tu, "mkisikia fulani anaumwa na zinahitajika pesa za matibabu njooni mi nitatoa, ila mkisubiri kishakufa ndo mjifanye kuja kuchangisha ntawazingua"

Binafsi huwa sipendi unafki
 
Yani ukiona mtu hukopeshwi pesa na marafiki wa kweli ni mawili tu

1. Kulipa mgumu
2. Hawana fedha muda huo


Tunapenda kutoa lawama tu lakini kama mtu unarudisha pesa kwa wakati, hamna mtu anaweza acha kukukopesha.
endelea kukua ngugu yangu.

japo kisa ni cha kutunga kwa lengo la elimu ila maisha yana tabia ya ajabu sana.

wakati unahisi unamfundisha asiye mrejeshaji yeye anatafsiri kama unafurahia shida zake,sasa uombe msijekutana mbele huko wewe ndiye mhitaji😂😂,na kwa vile nimekwambia maisha yana tabia ya ajabu...........
 
endelea kukua ngugu yangu.

japo kisa ni cha kutunga kwa lengo la elimu ila maisha yana tabia ya ajabu sana.

wakati unahisi unamfundisha asiye mrejeshaji yeye anatafsiri kama unafurahia shida zake,sasa uombe msijekutana mbele huko wewe ndiye mhitaji,na kwa vile nimekwambia maisha yana tabia ya ajabu...........
Yani mtu umemkopesha mfano 500k hajakulipa mwaka mzima, afu aje akuombe tena 100k utampa ?
 
Mimi nahitaji elfu 5 tu ili nipate chakula leo na ikiwezekana nauli nipate kurudi kijijini kwa wazazi wangu.
 
Back
Top Bottom