Me & daughter in fb | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Me & daughter in fb

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jan 9, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hakika tunampenda sana binti yetu wa miaka mitatu(3). Karibia kila mtu akimuona ana msifie kuwa ni binti mzuri sanaaa wa sura (cutie) . Kwa kuwa rafiki yangu mmoja aliwahi kulieleza madhara ya kuweka sura/picha ya mtu kwenye mitandao ya jamii kama Facebook (FB), nilimuasa mke wangu asithubutu kufanya hivyo hata kidogo nami nimekuwa makini kuepuka kufanya jambo hilo kwa lengo la kumlinda mtoto ili akikuwa awe na ridhaa yake kuweka hadharani picha zake. Siku zote najaribu kumkumbusha "mai wifu" kuhusu ili na amekuwa akinijibu "yeye si mjinga wa kufanya mambo tunayoshaurina asifanye na kwamba yeye hata anwani ya barua pepe hana, na hataki kusikia kabisa vitu kama FB".

  Lakini nasikitika sana, leo nimepokea mwaliko kutoka kwa rafiki mmoja katika familia yetu kupitia anwani yangu ya barua ya yahoo kunitaka nijiunge na Facebook. Baada ya kupokea mwaliko huo na kuingia kwenye FB, nakuta miongoni mwa marafiki zake ni mama watoto wangu na kwenye "wall" ya "mai wifu" na pia ya rafiki yangu huyo kuna picha kibao zikiwemo zangu na huyo mwanetu mpendwa ambazo nyingine sikumbuki hata zilipigwa lini.

  Marafiki ambao wengine siwajui kabisa wameandika maoni meeengi (comments) kwenye "wall" ya "mai wife" wakimsifia yeye na mtoto jinsi walivyo wazuri wa sura na kufafana. Wengine wame "comment" kuhusu mimi wakisema labda si baba wa mtoto wanataka aweke picha halisi ya baba yake kwani mimi sifanani kabisa na mtoto na sina hadhi ya kuwa na mke kama huyo "maiwifu". Mbaya zaidi kuna mwengine ambao wana majina ya kiume (siwafahamu) wame comment mara kibao kuwa wanataka penzi la wifu na kuomba atoe namba yake kupitai email zao.....sijui kama ametoa au lah......

  Nashindwa ni hatua gani nichukue kwa hasira nilizonazo leo!, sijamuuliza bado kuhusu ili.....
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  dah pole saana bro

  cha msingi usiwe na hasira, lipeleke taratibu, kwanza jaribu kukaa na mwenzio umchunguze ili ujue kiini cha yeye kukudanganya, from there kaeni chini wewe na yeye mtafute suluhisho. kweli hawawanawake mungu kawaumba lakini ni pasua kichwa kweli sijui kama tutaoa

  pole saana Ngoshwe
   
 3. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  pole sana. kabla ya kuchukua uamuzi vuta pumzi kisha itoe taaaratibu, chukua bilauri ya maji kisha unywe taaaratibuu.

  hata hivyo usione tabu mkeo kusifiwa hii ina maana umevuta chombo kwlei kweli lol na hata kama hasifiwe fb basi mtaani wanamsifu kwa saana tu.

  inabidi uzoe tuu
   
 4. American lady

  American lady Member

  #4
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana ngoshwe kwa yanayokusibu.cha msingi zaidi ni kumkalisha chini huyo waifu wako na kumuuliza hatima ya yote anayofanya itakuwa nn?maana yeye atakuwa anafurahia kusifiwa uzuri wake na binti wenu je hasikii vibaya mumewe kupondwa.thanx sn
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Nashukuru wote kwa ushauri, navuta pumzi.

  Kinachoniumiza kichwa sijui ni wangapi watakuwa wameona au ku-print pic za mtoto. Niliwahi kuelezwa kuwa kesi nyingi za watoto kuingiliwa/kubakwa au kulawitiwa kwenye nchi zilizoendelea zinahusishwa pia na watu wasio na nia nzuri kwa watoto kuwafuatilia watoto pengine kupitia mitandao ya kijamii kama hii.....au mashuleni na nyumbani kwao baada ya kuona picha zao na anwani za wazazi wao.....Mtoto amewekwa kwenye FB pasipo ridhaa yake wala hata mimi mzazi mwenzie, na sijui lengo la waifu ni nini kwa mtoto watu asiowajua wanapo msifia kwny FB kwa kumwita mtoto mdogo mchumba, love, "my wife to be" nk kwenye FB.....???
   
 6. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Pole kaka hii ndiyo tabu ya mitandao ya dizaini hii, lakini wife nae kachemka kwanini asikusikilize husband wake?, au alidhani siku ukijiunga hutojua kuwa yeye yumo pia, kweli kuuza sura kwenye fb kuna tabu yake, si mnakumbuka picha za watu zilikuwa zinatolewa huko na kuwekwa kwenye ze utamu, mueleweshe vizuri wife kwamba huo si utaratibu mzuri kwani kwa mke wa mtu kutumiwa msg za ajabu kwenye mtandao kama fb ambao all your friends wanaweza kusoma wall yako sio fresh, anajishusha hadhi na kukudhalilisha baba watoto.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Hamna uaminifu hapo, na kama hamna uaminifu katika hili, hujui kuna mengine yepi yaliyokosa uaminifu.

  Kama wewe mwanamme mkalishe chini na umueleze kwamba upumbavu wake umeugundua.

  Ningekuwa mimi hapo sababu tosha ya kuenda kufanya paternity test.Maana kama mkeo anakudanganya kuhusu picha na Facebook inawezekana linalosemekana kwamba amekubambikia mtoto nalo likawa kweli, si yote yanahusu kukosa uaminifu? Yote yanahusu kukufanya wewe mjinga usiyeweza kugundua.

  Hapo kitu cha muhimu kufanya paternity test huku ukiwa huna hofu ya kutaliki.

  Ndiyo maana wengine hatutaki kuoa, sasa wewe mazee uliyeoa na sie tusiooa hatuna tofauti maana ndoa inatakiwa ku guarantee trust, ukikosa trust what is the meaning of marriage? Si bora hata sie wasela tunaojua bado tuna circle the block looking for that parking spot.

  Marriage is overrated.
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Poa moto ndugu yangu,
  Jaribu kuwa mwelewa tu ili hata mama watoto akikupa sababu zake za msingi utamuelewa kwanini mwenzio yupo proud kuweka picha hadharani za binti yenu na wewe mumewe.

  Hizo comments za 'wapita' njia zichukulie tu kama "uhuru wa maoni", usikubali maneno yao yakuingie kichwani nawe eti ukaamini hufananii kuzaa kabinti ka cute kama hako!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jan 10, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Unaona sasa..ndio maana sisi wengine hatuna hiyo mi facebook. Ni ujinga mtupu kubandika mambo yako huko kwenye hilo litovuti. Halafu hii facebook imeanza kuharibu sana mahusiano ya watu (not that I care about relationships). Watu wana hook up na old flames wao n.k. Hakuna uaminifu kabisa kwenye haya mambo ya social networking. Kuyaendekeza ni kujilengesha kuvunjwa moyo bure pasipo na sababu ya msingi.

  Sasa kama kuna njemba inawasiliana na mkeo kwenye mail messages za facebook utajuaje? Daah...pole sana babu
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,640
  Trophy Points: 280
  Mtoto sio wako
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Namuuliza hana la kusema anajibu eti mtoto si wetu wote na yeye ndie aliyeumia kumzaa, na mimi sijua maumivu yake ya kumkamua huko hospitali??.....
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Dharau inaendelea.

  Yaani badala ya kujirudi na kukuomba msamaha anazidisha dharau.

  Mwanamme mwenye kufikiri lazima ujiulize, hii dharau inatoka wapi?

  Kuna uwezekano mkubwa sana mkeo unamegewa na wajanja, kuna uwezekano hata huyo mtoto unayeambiwa ni "wenu" si wenu.

  Piga DNA test hapo mazee.
   
 13. C

  Chief JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nakuunga mikono yote
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Majibu mabaya sana haya kwa mwanamke katika matrimonial
  house, ambapo mwanaume anatakiwa kuwa kichwa cha nyumba!

  Kuna kitu kinatakiwa kifanyike hapo ndani kwenu, mtu aonywe, na afunzwe adabu...
  Lakini isije ikawa na wewe unaogopa kumpoteza mkuu(kwa urembo alio nao), kwahiyo unasikilizia maumivu na kukomaa kiujanja!...du!
   
 15. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...of'coz atakuwa hana la kusema. Lugha gani unatumia kumhoji, ukali? kumbuka kwamba huyo ni mkeo, ulipompenda na hata kumuoa ulimpenda kwa mazuri yake, na mabaya yake ukayafumbia macho.

  Kumbuka, naye ana haki kujinadi mbele ya marafiki zake kwamba ana mume na mtoto mzuri kama huyo wenu. Kosa kubwa sana kumhoji uhalali wa mtoto wenu, Ikijagundulika ni wako utaombaje msamaha?

  Masikilizano ni muhimu ndani ya nyumba. lakini vile vile masikilizano hayo yasiwe "one way traffic" eti kwakuwa wewe ni mwanaume, eti 'Mfalme' wa Nyumba.

  "when you strengthen your self esteem, there is no room for jealousy!"

  Be brave my bother, najua inakuuma sana, lakini 'ufa hauzibwi kwa jazba na vishindo'
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hasira za nini sasa?
  au unahisi ukweli fulani?
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,486
  Trophy Points: 280
  .

  Ngoswe, Wanawake ni Mama zetu, dada zetu na wake zetu wanastahili heshima zao zote, lakini kuna baadhi yao, wee acha tuu.

  Ushauri wangu, take it easy, usichue uamuzi wowote wa hasira. Tena mambo ya DNA ndio achana nayo kabisa usije umia ukakosa mwana mke na maji ya moto.

  Kwa mliosoma kitabu sikumbuki nadhani Sidney Sheldon The Prodigal Daughter akiitwa Noela, baba mvuvi samaki wa Kitaliano na mama, wote ni brunette brown eyes wakazaa very beutiful daughter blonde blue eyes!.

  Sisi ngozi nyeusi hatuna mengi, 'mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba'
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  pasco...
  Hicho kitabu kinaiitwa
  memories of midnight
  cha sidney sheldon

  sikijui hiko cha prodigal daughter,
   
 19. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Mi yanawake ndivyo ilivyo.
   
 20. nyaunyau

  nyaunyau Senior Member

  #20
  Jan 10, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mwanamke huyo anajua wewe siyo baba mtoto huyo ndiyo maana hakutii maelekezo yako check DNA
   
Loading...