Mdunguaji wa Goma

Mdunguaji wa Goma

RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SIMU; 0758573660/0624155629.


HII NI SEHEMU YA SABA.


Wakati alipokuwa akisimama baada ya kuokota mchanga, masikio yake yalihisi sauti ya mkimbio wa kiumbe hai. Kiumbe ambae alikuwa anatumia ncha ya viatu vyake ili asitoe kishindo na, alipoinua uso wake, aliona kivuli cha mtu kikimfuata kwa kasi kubwa ambayo haikuitarajia na, kabla hajasimama vema, alijikuta akichezea mateke mawili ya kifua na kwenda chini bila kupenda.

Licha ya kuanguka, lakini hakufungua mdomo wake ili kutema mchanga wote, ambao aliufumbata chini ya ulimi na badala yake, aliinua ulimi kidogo na kutema mchanga mmoja tu na,mdomoni alisalia na vipande vitano vya mchanga.

Alipojaribu kuinuka, alijikuta akirudi chini huku ubavu wake wa kushoto ukipokea maumivu makali, kiasi alishindwa kuhimili na kujikuta akiguna kwa maumivu.

Kama kawaida kila aliposhindwa kupambana, alikuwa akitema chini kipande kimoja cha mchanga na kusalia na vipande vinne mdomoni mwake.

Alitulia chini na kumtazama adui yake ambae alikuwa akijiandaa kumshambulia tena, na kwa kasi ya ajabu alijiinua chini na kusimama wima, kisha alijipanga kwa mpambano huku maumivu, yakianza kuutafuna mkono wake wa kushoto, ambao ulikuwa umejeruhiwa na risasi.

Adui nae alikuwa amesimama bila kutetereka, alijipanga kukabiliana na Miguu ya kuku.

Adui alikuwa ni Tembe za chai, ambae alimfuatilia hadi alipofanikiwa kuyaona makazi ya Miguu ya Kuku, kisha akuachagua usiku kumtembelea kwa aina ile ya kushitukiza.
Miamba walikutana, huku mmoja akijisifu kumfuata nyumbani adui yake na mwingine akiona dharau kufuatwa nyumbani kwake.

Hakika ulikuwa ni mtihani usio na majibu rahisi.

*****

Miguu ya Kuku alikuwa amesalia na vipande vinne vya mchanga, mdomoni mwake huku kisu kidogo akiwa amekishika vema mkononi mwake. Hakutaka kuanza kumshambulia adui yake, badala yake alijisimamisha kivivu ili kumhadaa hasimu wake.

Hadaa yake ilizamaa matunda, kwani alifuatwa kwa mtindo wa zigizaga, huku mapigo kadhaa yakimpita mithili ya wacheza filamu za kichina.

Mapigo mengi yalipita patupu lakini pigo moja la mwisho, lilimwingia vema kwenye paji lake la uso na kumyumbisha kidogo, lakini alihimili na kusimama.

Kama kawaida yake, alitema kipande kimoja cha mchanga na, kufanya idadi ya vipande mdomoni vibaki vitatu.

Alijipanga tena na Tembe za chai nae alijipanga kwa mpambano mwingine.

Wakati huu miguu ya Kuku alianzisha yeye mapambano. Alimtisha kama anataka kumtandika teke na adui alipotishika, aliachia konde la mkono wa kulia lililoenda kutua kwenye mwamba wa pua, kabla mpigwaji hajajifikiria zaidi, ngumi nyingine ilitua kwenye kidevu(chembekidevu).

Ngumi aliopigwa Tembe za chai, ilimfanya ashindwe kuelewa mdomo wake umekutana na dhahama namna gani, badala yake alianza kuhisi ladha ya chumvi huku mate yakiwa mazito mdomoni mwake. Kabla hajajua ateme au ameze mate yake, alijikuta akikutana na dhahama ya kutandikwa teke la shingo, kiasi alishindwa kupumua vema huku akienda chini mzimamzima.

Wakati yeye akienda chini, Miguu ya Kuku yeye alikuwa anatema kipande cha mchanga, na kusalia na vipande viwili mdomoni mwake.

“Baboon!” Alisema kwa sauti huku akimsubiri adui yake ainuke, hakutaka kumpiga kwa kuvizia na mwishoni aonekane alimuonea. Alitaka wapigane wima wima, ili mshindi ahesabike kiuhalali.

Baada ya kusimama, mpambano ulianza upya, kila mmoja akijaribu kutumia ufundi wake, kumdhibiti mwenzake.

Dakika moja ilikatika bila mjuzi zaidi kupatikana. Kila mmoja alikuwa amepangua ngumi na teke nyingi, bila kuruhusu kuguswa na mpinzani wake.
Miguu ya Kuku alitema chini kipande cha tano cha mchanga na, kusaliwa na kipande kimoja mdomoni. Hakutaka kipande kile kimalizike mdomoni bila kumdhibiti adui yake.

Aliweka vema kisu chake, huku akiweka mkao aina ya FiuFui, mkao maarufu wa kutumia silaha ndogo, kwenye jamii za watu wa Lebanon. Mkao ule ulikuwa unamfanya mpambanaji kuchutama, huku akitandaza mikono na kisha kuanza kujongea, mithili ya nyani aliyeiba mahindi shambani.

Tembe za chai hakuwahi kuona mkao wa aina ile, hivyo hakujua mwenzake amedhamiria kufanya nini. Haraka alitaka kujaribu bahati yake, kwa kuushambulia mguu wa kushoto wa hasimu wake, akiwa na lengo la kumtegua na kumtupa chini.

Kitu kimoja hakuwahi kujua mchezo wa FiuFui huwa ni mchezo hatari kwa adui. Wakati alipojaribu kurusha teke, alishangaa mguu wake ukidakwa kwa ustadi mkubwa, kisha alihisi akichanwa nyuma ya paja na kitu chenye ncha kali. Alipojaribu kuruka ili ageuke kujua kilichomsibu, alishangaa akichomwa nyuma ya mgongo, huku hasimu wake akiwa mbele yake akinesanesa.
Tembe za chai alishindwa kuelewa imetumika kasi kiasi gani, kuchomwa na kisu mgongoni na aliemchoma kuwa mbele yake.

Hata!

Hofu ilianza kumuingia, hakuwahi kukutana na kiumbe mwenye kasi namna ile, hakuwahi kuona mapigo ya kutumia kasi namna ile.
Mapigo ambayo ndani ya sekunde tatu, tayari anamilikishwa majeraha mawili ya kuchanwa na kisu.
Akajaribu bahati yake kwa mara nyingine, lakini alijikuta akiloa mvua ya ngumi zisizohesabika. Hakikutumika kisu, bali ngumi ambazo ziligusa kila eneo lenye udhaifu.

Tembe za chai alienda chini huku akiwa amepiga magoti, mithili ya muumini mwovu kanisani. Alihema kwa tabu huku maumivu yakiutawala mwili wake na alipomtizama mwenzake, alishuhudia mnesoneso usio na mpangilio, ikiwa na maana, wakati wowote angekutana na pigo la kifo.

Akubali kufa? Hapana, hilo hakuona kama ni sahihi kwa wakati huo, kufa kizembe namna ile,hakika aliona mtihani.

Alipanga kuitumia nafasi ambayo aliona Miguu ya Kuku anaichezea, alipanga jambo.

Wakati akiwa kwenye mipango yake, masikio yake yalihisi sauti ya kutemwa kitu kutoka kwenye mdomo wa mpinzani wake. Akili yake ilicheza na kumbukumbu za kutema yule bwana na, kumbukumbu hazikudanganya. Alikumbuka vema kumuona jamaa kwenye jengo la mauzo, akitafuna karanga moja moja na, alipotafuna karanga ya tano, alimshuhudia akianzisha varangati lisilo na mfano, hadi yeye alipoingilia. Na sasa, anamsikia jamaa akitema kila baada ya muda na kwa idadi ilifika sita.

Hata! Nani haogopi kifo?

Kwa hali aliokuwa nayo aliamini hawezi kupambana na, kwa haraka alijua jamaa huwa anahesabu zake kila akitema kitu kutoka mdomoni, hivyo hakutaka kuingia kwenye hesabu hizo.

Haraka alisimama, kisha akajirusha na kuanguka upande mwingine, huku akimuacha Miguu ya Kuku amezubaa. Alitumia mshangao wa mwenzake kufanikisha adhima yake.

Kwa wepesi wa nyoka vichakani, aliudandia ukuta kama mzaha vile, kisha alijirusha na kuanguka nje ya uzio na kuanza kutimua mbio za Madenge na mpira.

Kitu kimoja ambacho hakujua ni kuwa, Miguu ya Kuku ni mtaalamu zaidi yake, ni mtaalamu wa kuruka kuta za kila aina na, kasi yake ya kukimbia ni zaidi ya swala. Anakimbia mita mia kwa sekunde nane tu, tena akiwa hatoi vishindo.

Tembe za chai alienda kuyavagaa asioyaweza.

****

Wakati akidhani amemkimbia Miguu ya Kuku, alishangaa akipigwa mweleka safi, huku akidakwa ili asianguke chini, kisha alizungushwa kwa mtindo wa ajabu kabisa na kubwagwa chini kama gunia la viazi vya Mbeya. Kabla hajajua kilichomzoa namna ile, alishangaa akitandikwa konde zito katikati ya kifua na kumfanya apoteze uelekeo wa kuvuta hewa safi.
Alitamani kuongea, lakini alishindwa. Alitamani kupiga kelele za kila namna, lakini sauti haikutoka katu na, badala yake alijikuta akitandikwa makofi ya uso kama mtoto mdogo, aliyedokoa maharage ya wenyewe.

Kamasi nyepesi pamoja na mate mazito, vilimtoka bila kupenda. Alipokuja kupata ufahamu, alijisikia akilia kama mtoto aliesuswa na *****.

Aibu jama!
Alijisikia aibu mbele ya mwanaume mwenzake; alimkimbia na sasa analia kama mtoto mdogo huku akiwa amepiga magoti.

Yaani kutoka kuwa mamluki wa kuogopwa, hadi kulia mbele ya mwanaume mwenzake. Hakika Tembe za chai alijuta kumfahamu Miguu ya Kuku.

“Naitwa Zuki Gadu alimaarufu Miguu ya Kuku” Alijitambulisha kisha aliendelea.

“Huwa siui bila sababu na hapa sijui tunapigana kwa sababu gani. Hata kule mjini yule boya nilimuua kwa sababu sikutaka kashikashi na polisi.” Zuki Gadu alitua.

“Hata mimi sijui kwa nini tunapigana, ila najua nilikufuata ili kufunza adabu..” Tembe za chai alijibu.

“Kwa hivyo bado unataka kunifunza adabu?”

“Umenishinda ndugu, na niache niendelee na….” Tembe za chai hakumaliza kauli yake, risasi ilifumua kichwa chake, huku Miguu ya Kuku akijirusha upande mwingine na kulala chini, asijue alieshambulia ni nani.

Hofu ikamvaa, moyo ukamdunda, mwili ukamsisimka, ngozi ikajikunyata.

Akiwa amelela chini, alishuhudia watu watatu wakimfuata kwa kasi, huku kila mmoja akiwa ameshika bastola yenye kiminya sauti.

Watu wale wote walikuwa wamevalia koti ndefu, huku nyuso zao zikiwa zimefunikwa na barakoa. Waliendana na giza la muda ule.
Miguu ya Kuku alihisi ni zamu yake kupiga magoti na kulia.

Hilo hakutaka limkute, akapanga kufa kiume na vita ni asili yake, akasimama wima, kisu mkononi, tayari kukabiliana na miamba mitatu inayotembea kizungu
.
.
.
.
.
.
ENDELEA KUWA NAMI.
Hatari sanaa
 
RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA NANE.



Kamasi nyepesi pamoja na mate mazito, vilimtoka bila kupenda. Alipokuja kupata ufahamu, alijisikia akilia kama mtoto aliesuswa na *****.

Aibu jama!
Alijisikia aibu mbele ya mwanaume mwenzake; alimkimbia na sasa analia kama mtoto mdogo huku akiwa amepiga magoti.

Yaani kutoka kuwa mamluki wa kuogopwa, hadi kulia mbele ya mwanaume mwenzake. Hakika Tembe za chai alijuta kumfahamu Miguu ya Kuku.

“Naitwa Zuki Gadu alimaarufu Miguu ya Kuku” Alijitambulisha kisha aliendelea.

“Huwa siui bila sababu na hapa sijui tunapigana kwa sababu gani. Hata kule mjini yule boya nilimuua kwa sababu sikutaka kashikashi na polisi.” Zuki Gadu alitua.

“Hata mimi sijui kwa nini tunapigana, ila najua nilikufuata ili kufunza adabu..” Tembe za chai alijibu.

“Kwa hivyo bado unataka kunifunza adabu?”

“Umenishinda ndugu, na niache niendelee na….” Tembe za chai hakumaliza kauli yake, risasi ilifumua kichwa chake, huku Miguu ya Kuku akijirusha upande mwingine na kulala chini, asijue alieshambulia ni nani.

Hofu ikamvaa, moyo ukamdunda, mwili ukamsisimka, ngozi ikajikunyata.

Akiwa amelela chini, alishuhudia watu watatu wakimfuata kwa kasi, huku kila mmoja akiwa ameshika bastola yenye kiminya sauti.

Watu wale wote walikuwa wamevalia koti ndefu, huku nyuso zao zikiwa zimefunikwa na barakoa. Waliendana na giza la muda ule.
Miguu ya Kuku alihisi ni zamu yake kupiga magoti na kulia.

Hilo hakutaka limkute, akapanga kufa kiume na vita ni asili yake, akasimama wima, kisu mkononi, tayari kukabiliana na miamba mitatu inayotembea kizungu.

****

Kitendo chake cha kusimama, kilifanya midomo mitatu ya bastola zenye viwambo vya kuzuia sauti, imwelekee yeye ikiwa na maana muda wowote angechakaa risasi.
Alishusha pumzi huku akiwaza mbinu mbadala kujikwamua, hakutaka kuingia kwenye mikono ya wale jamaa, ambao hakuwa amejua dhamira yao.

Watu wale walimfikia na kumzingira, huku wakiwa kimya bila kumsemesha. Nae hakuwasemesha, alitega masikio yake kama antena ya mnara wa kijerumani, akiwa tayari kuisikia sauti yoyote ya hatari kutoka kwa watu wale, ambao walivalia makoti marefu na barakoa nyusoni mwao.

“Maiti hii usishugulike nayo, tumemuua sisi, acha tuizike sisi” Mmoja wa wale watu alisema, huku akishusha silaha yake chini na kumfuata Tembe za chai, ambae alikuwa amesambaratika chini bila uhai.

“Hii siyo kesi yako tena, hukuua wewe hivyo tuachie sisi. Usijiulize lolote kuhusu sisi, huyu ni wa kwetu.” Alizungumza jamaa mwingine huku na yeye akishusha bastola yake na kupiga hatua kumfuata mwenzake, aliyekuwa ameanza kumbeba Tembe za chai.

Miguu ya Kuku alibaki akishangaa, hakujua wale ni kina nani na wamefuata nini pale na, kwa nini walimuua Tembe za chai, huku wakimwacha yeye. Pia ni kwa nini wamruhusu kilarahisi namna ile.

Hata!

Lipo jambo. Tena jambo kubwa ambalo hakujua ukubwa wake ni kiasi gani.

Alijifikiria mara kadhaa; aachane nao ama apambane kujua lengo lao?
Wazo kubwa lilikuwa ni kuachana nao, ili afanye mipango mingine na awatafute kukikuchwa, lakini wazo likapingwa na wazo lingine.
Aliwaza ni vipi kama muda wote walikuwa wanamfuatilia na wanajua, sakata la mengi yaliyotokea siku hiyo. Na vipi kama wanataka kutumia tukio la aina hiyo, kuja kumpelekesha watakavyo.

“mh!” Aliguna huku akilini akishindwa kuamua maamuzi sahihi ya kuchukua. Macho yake yaliendelea kuwaangalia wale jamaa, wakiuchukua mwili wa Tembe za chai na kusogea nao barabarani, kisha waliubwaga chini bila wasiwasi wowote na kusimama kando, kama si wao walioumwaga.

“Kina nani hawa? Mbona wanajiamini sana na kila kitu wanachokifanya?” Alijiuliza huku akipiga hatua kuelekea kwenye geti la nyumba yake.

Aliamua kuwaacha waende zao, kwa sababu aliamini; kujiamini mbele ya mgeni anaejiamini kwenye mazingira hatarishi, ni silaha ya kumrudisha nyuma mgeni huyo.

Aliona akifanya jambo lolote, atakuwa ni sawa na muoga anaeogopa mapambano yajayo na yeye hajawahi kuwa kunguru hata siku moja.

“Watajuta endapo wataingia kwenye anga zangu, ila kama walimfuata yule pimbi ni, jambo jema sana.” Alijisemea huku akisukuma geti, baada ya kulifungua kwa njia alizojua yeye, baada ya kuwa alishafunga kwa ndani kabla ya sekeseke na Tembe za chai.

Siku hiyo aliamua kulala kwenye chumba chake cha siri, huku masikio akiyaacha hai kwa ajili ya kunusa ugeni wowote, ambao ungelitokea.

Miguu ya Kuku alilala huku akiwa ni mshindi wa mapambano ya siku nzima.

****

Wakati Miguu ya Kuku akilala kwa uchovu mkubwa, kundi la watu watatu lilikuwa linaingia kwenye nyumba moja mitaa ya Mbezi. Kundi lile lilikuwa kwenye gari la wagonjwa, huku mmoja akiwa Dereva na wawili wakiwa wamevalia mavazi ya kitabibu. Ndani ya gari walikuwa na kiumbe kisicho na uhai, ambacho walitoka kukipokonya uhai huko Tegeta kwa Ndevu.

Walipoingia ndani ya nyumba ile, wale wawili haraka walishuka na kuutoa mwili, kisha waliubeba mzegamzega na kuupeleka kwenye kijumba kidogo, ambacho kilikuwa kimejengwa kando ya nyumba kubwa.

Walipofika mle ndani, mmoja aliwasha taa kisha mmoja alifungua pipa, lilokuwa na kimiminika kilichotulia.

“Tunalizamisha kwanza au tunamtumbukiza jamaa ndo tunalizamisha?” Jamaa aliyefungua pipa lile, alimhoji mwenzake.

“Tumtumbukize, kisha tulizamishe pipa lote.” Jamaa alijibu.

Haraka haraka walisaidiana kuibeba ile maiti na kuitumbukiza kwenye lile pipa, huku wao wakiruka kando wasiguswe na kimiminika kilichokuwa ndani ya lile pipa.
Walipohakikisha ule mwili umepotelea kwenye pipa, huku kimiminika kilichokuwamo kikianza kuchemka mithili ya maji ya pombe, mmoja alibonyeza kitufe chekundu ukutani na, taratibu lile pipa lilianza kwenda chini ya ardhi.

Dakika moja baadae, lile pipa lilipotelea chini na kisha ukafuatia mfuniko kufunika juu yake na wale jamaa walizima taa na kutoka ndani ya kijumba kile.

Walitoka wakiwa wameyeyusha mwili wa mtu kwenye tindi kali na kulikuwa hakuna ushahidi tena, kuhusu mtu aliyeuawa.

****

“Sasa nadhani kila mmoja ameona kazi ya Miguu ya Kuku” Jamaa mmoja alisema huku akikaa kwenye sofa na kuivua barakoa yake.

“Hakika ulisema bwana. Huyu jamaa anasifa zote za kutufanyia kazi yetu huko Congo” Jamaa mwingine alijibu huku akivua mavazi ya kitabibu aliyokuwa ameyavaa muda mfupi uliopita.

“Mimi sina neno, nimenyoosha mikono juu” Alijibu jamaa mwingine huku akivua viatu vyake.

“Licha ya kunyoosha mikono kwa kazi ya huyu bwana, lakini naamini kuna kosa tumelifanya.” Aliongea jamaa aliyekuwa amevaa barakoa, kabla ya kuivua na kuitupia pembeni.
“Alfa, kosa gani tena?” Jamaa mmoja aliuliza huku akikaa vema sofani.

“Kumuua Tembe za chai mbele ya macho ya Miguu ya Kuku” Alfa'one alimwambia.

“Lakini Omega ulikatazwa kufanya vile.” Jamaa mwingine nae alidakia.

“Rich, sidhani kama nilipotoka. Ilikuwa ni heri kumuu, kuliko tungeliwaacha waendelee kupiga soga. Wangekubaliana na kuelezana tumewachezea kamari, basi nina hakika tusingeendelea kukaa pamoja usiku huu. Wangelituwinda wanaizaya wale” Omega'one alijitetea baada ya kutuhumiwa na wenzake, kufanya kosa kumchapa risasi Tembe za Chai.

“Duhh! Ila uliwaza mbali sana aisee!” Rich'one alisema huku akibebanisha miguu yake.

“Unaweza kuwa ulikuwa sahihi, lakini kichwa changu kimejaa mashaka. Miguu ya Kuku namfahamu, atataka kujua kwa nini jamaa aliuawa na kina nani walimuua. Kumbukeni hadi tunaondoka pale, hatukujitambulisha kwake na alitumia busara sana kutuacha, ama pengine alichoka” Alfa aliendelea kuwatahadharisha wenzake.

Ukimya ulishika hatamu kwa sekunde kadhaa.

“Tuachane na hayo. Ila kiukweli yule jamaa alinifurahisha sana alipomuua Kiuno cha nyoka, katikati ya umati wa maofisa wa jeshi, tena wenye silaha za moto” Rich' alihamisha mada.

“Yule jamaa kweli ni miguu ya Kuku, yaani alifanya tukio ambalo hakuna aiyelitegemea bwana.” Omega aliunga hoja, huku akichekelea kivivu.
“Hayo ndo mambo yake huyu bwana. Anafanya tukio popote kwa ufanisi mkubwa na, sikukosea kumchagua. Hii kazi yetu inahitaji mtu mwenye uwezo kama wake” Alfa aliendelea kusifia.

“Unajicho kali sana bwana mkubwa. Hakika unastahili kubeba maono ya Boys Among Men. Upo vizuri”

“Sasa tujadili haya majina ya hawa watu wetu huko Goma. Aanze na nani na amalizie kwa nani”

“Tusimpangie wa kuanza nae, bali tumpe orodha ya watu wote sita, kisha tumpe pesa afanye kazi yake.”

“Hakika, maana tukimpangia, tutakuwa ni kama tunamchuuza tena. Yule ni mamluki, anazombinu zake na kikubwa akamilishe kazi yetu kwa ufasaha.”

“Lakini si mnajua Papaa Deo bado anaendesha vita? Si mnajua sehemu anayopeleka mali?”

“Ndiyo tunaelewa. Lakini sisi lengo letu wafe tu ili walipe ubaya wao.”

“Mi naona wasife bila na sisi kuwatia hasara kidogo. Inabidi mali iliyoko kwa Papaa Deo iingie mkononi mwetu, angalau turudishe mzigo waliotudhulumu watoto haramu wale”

“ Sasa hiyo ni kazi nyingine bwana. Hapa naona kabisa zinaibuka kazi mbili; wizi na uuaji. Lakini ni rahisi kuua kuliko kuiba kwa Papaa Deo”

“Kama mnazo milioni mia sita za kumlipa Miguu ya Kuku, basi kazi zote atafanya” Alfa aliingilia mjadala, baada ya kuwa amekaa kimya muda mrefu.

“Milioni mia sita!” Waliuliza mshangao kwa pamoja.

“Ndiyo. Bila hiyo pesa, tafuteni mtu mwingine wa kuwafanyia hiyo kazi. Kumbukeni Papaa Deo ni Kanali wa jeshi na anaulinzi kila pahali.” Alfa alisisitiza hoja yake.

“Milioni mia sita ni pesa ndefu sana, lakini kama akifanikiwa kuiba mali kwa Papaa Deo, nitamuongezea na nyingine ifike bilioni” Rich'one alisema kwa majivuno.

“Pesa ndefu sana aisee!” Omega bado walikuwa anashangaa.

“Ulishazoea majambazi wa bei rahisi eeh. Huyu ni classic killer” Alfa alizodoa.

“Lakini naomba asiembiwe wadhifa wa hawa watu tunaomtuma. Endapo akijua wadhifa wao, anaweza kuahirisha zoezi. Maana ni rahisi sana kumuua kiongozi mmoja wa kijeshi, lakini ni ngumu kuua viongozi sita ndani ya muda mfupi.” Rich alishauri.

“Upo sahihi. Lakini Miguu ya Kuku hawezi kwenda sehemu bila kujua anafuata watu wa aina gani.” Alfa alichomekea.

“Kwa hiyo unamaanisha anaweza kutuuliza kabla ya kukubali?”

“Ndiyo au hapana. Kwa sababu inategemeana na mzuka alioamka nao siku hiyo.”

“Aisee!”

“Eeh! Miguu ya Kuku ni mwanajeshi asie na namba ya ajira. Anaakili kuliko udhaniavyo.”
“Hii bado ngumu, adhima yetu inaweza isifanikiwe na wale jamaa wakaendelea kutafuana mali walizotudhulumu.” Omega alianza kuonesha wasiwasi wake.


Wakati wale wazee wakijadili kuhusu Miguu ya Kuku na kazi wanayotarajia kumpa, yeye alikuwa anajigeuza upande kitandani, huku akiwaza namna ya kuingia jengo la mauzo na kuuchukua mkoba mweusi.

Alitarajia kukutana na upinzani mwingine tena, hivyo alianza kupiga hesabu zake upya huku akingoja mapambazuko.

Mambo yakawa mambo na akilini hakuwa na wazo lolote kuhusu safari ya nje ya nchi na laiti angelijua, hakika asingeliwaza kufuata mkoba mweusi.

Kwa maana ni heri vita ya Tanzania, kuliko vita ya Congo, tena kwenye jimbo la Kivu ya kaskazini.
.
.
.
.
.
ENDELEA KUWA NAMI.
 
Back
Top Bottom