Mdunguaji wa Goma

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,768
2,000
NA; BAHATI K MWAMBA
-----1------

Kikao cha watu watatu kiliendelea na kila Mjumbe, tayari alishatoa wazo lake aliloona ni sahihi kwa wakati huo. Makubaliano ya hapa na pale yalifikiwa, lakini ukaibuka utata kwenye hitaji lao la mwisho, na lilowafanya wakutane siku hiyo.

Maongezi yao yalihama kuwa ya kibiashara, yakaelekea kuwa ya kibabe na kila mmoja akitaka hoja yake ipite bila kupingwa.

Wazee hawa wenye umri sawa, walivimbiana huku kila mmoja akijinasibu kwa sifa zake, achilia mbali uwezo wa fedha na, mali walizomiliki ambapo; Mali zote hazikupatikana kwa njia halali na hilo ndilo, lilifanya uibuke mzozo, kwa kuwa kila mmoja alikuwa na aina ya watu ambao, aliwatumia ili kutimiza ujazo wa mifuko yake.

Ukiachilia mbali wazee hawa kuibuka kuwa wenye ukwasi wa kutisha, pia walikuwa ni wasitaafu wa jeshi, wakiwa na vyeo vya chini kabisa.

Kila aliyewafahamu, alijiuliza ukwasi huo waliupata vipi ikiwa, mafao yao yalikuwa hayawezi kuwafikisha kwenye kilele cha ubilionea. Wengine walidhani watakuwa walienda kuroga ili wasife masikini, huku wengine wakidhani walikopa bank ili waziishi ndoto zao.

Mengi yalisemwa, lakini ni wao waliofahamu ukwasi huo waliupata vipi.

Wakati watu wakishangaa utajiri huo wa baada ya kustaafu, lakini wao walianza kuuishi miaka mingi hata wingali kazini. Waliufanya kuwa siri, huku wakiendelea kufanya unyama wa hapa na pale, ili kutunisha hazina zao.

Lakini waliendelea kujivika mwamvuli wa kazi, huku kazi zao zikifanywa na watu maalumu wa kukodi. Watu hawa maalumu ndiyo waliozua zogo kwenye kikao chao hicho, kila mmoja aliamini mtu wake ni sahihi kuifanya kazi waliokusudia kuifanya.

Si kwamba watu hao wa kununua hawakuwafahamu kwa ujumla wao; la hasha, waliwafahamu vema lakini, kila mmoja alimwamini yule alieyefanya nae kazi kwa muda mrefu na kwa uaminifu mkubwa.

“Jamani eeh, hebu tusigombane. Sisi sote ni BoysAmongMen, ni lazima tukubaliane kwa sauti moja bila kukwazana” Alizungumza Mzee mmoja ambae hupenda kujiita Rich'one.

Ukapita ukimya mfupi huku kila mmoja akijaribu kushusha morali yake.

“Mimi bado naona hii kazi tumpe Kiuno cha nyoka, huyu bwana anaijua kazi yake vilivyo na mazingira yoyote anaweza kufanya kazi yake.” Alizungumza mzee mwingine, ambae alipenda kujiita Omega'one.

“Lakini nabaki na msimamo wangu, Kiuono cha nyoka hawezi kuifanya kazi hii. Kwanza anatamaa sana, pia ni mtu asie na msimamo kabisa. Akipata dili lenye pesa kubwa, ni rahisi kuitosa kazi yetu.” Alizungumza Rich'one huku akiwatizama wenzake kwa umakini, kuona kama hoja yake inawaingia.

“Tukisema kila mmoja ampambe mtu wake, hakuna mbabe kati yao, maana, kila mmoja atakuwa na sifa sawa na zile za mwenzake kwa kuwa, sifa zote zitakuwa ni za weledi wa kufanya kazi kwa usahihi” Omega aliongea huku akiwatizama wenzake kwa utulivu mkubwa na kufanya umakini, uongezeke miongoni mwao.

Alipohakikisha wenzake wametulia na wanamsikiliza, aliendelea.

“Sifa zote tumezisikia na sasa ni wakati wa kuweka majina yote mezani, kisha tuchambue sifa zao zote kwa umakini na, tutoke na jina moja lenye nguvu.”

Mzee aliyependa kujiita Omega'one alikaa vema kwenye kiti, huku akisubiri wenzake watekeleze wazo lake.

“Mm-mh-mh-...” Mzee mwingine ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu, alirekebisha koo na kujiweka vema ili aongee jambo lake.

Wenzake walikaa kimya na kumsikiliza.

“Mawazo yenu yako sawa kabisa. Boys among men, daima huwa hatogombani kirejareja namna hii, bali huwa tunaamua wazo moja lenye tija.” Alinyamaza kidogo na kuwatazama wenzake, kisha alipoona wanamsikiliza, aliendelea..

“Mmewataja watu wenu na sifa zao; mmemtaja Kiuno cha nyoka na
Tembe za chai, kama ni watu makini na hatari kwenye kufanikisha matukio makubwa na yenye kuogofya.” Alinyamaza na kuwatizama tena wenzake, ambao walikuwa wamekaa kimya wakimsikiliza.
Aliendelea..

“Lakini pengine hamjapima uzito wa Nazi hii tunayowapa. Kazi hii inaugumu kwa kiasi kikubwa na inahitaji mtu makini sana na mwenye kutumia akili, kuliko nguvu na uchawi. Mtu huyu pia awe ni mwenye ujuzi wa mapigano na mwenye kujua kuitumia vema silaha yoyote, awe ni mwenye kuendesha chombo chochote cha moto, awe ni mtu ambae amefunga mkataba na kifo, wakati wowote kikimuita yuko tayari kukipokea. Mtu huyu awe zaidi ya komando wa jeshi la uzunguni.” Mzee yule alimaliza kuongea na kuegemea mwenye kiti alichokalia, huku macho yake yakihama; kutoka kushoto kwenda kulia na kulia kwenda kushoto. Aliwatizama wenzake ambao walikuwa kimya wakitafakari uzito wa hoja ya Alfa'one, ambae mara nyingi walimheshimu kwa busara zake miongoni mwao.

“Kwa hiyo unashauri tuachane na hawa jamaa?” Rich'one alimuuliza.

“Hapana! Hawa hawa wanatosha, lakini tuchague mmoja ambae anaweza kupiga vita peke yake kwenye nchi ngeni” Alijibu.

“Unahisi ni yupi anaefaa kuibeba kazi hii?” Omega'one aliuliza.

“Wote wanafaa kuibeba kazi hii, lakini nampendekeza zaidi huyu jamaa anaeitwa Miguu ya Kuku.”

Ukapita ukimya mfupi kila mmoja akitafakari la kwake kisha, ukimya ule ukavunjwa kabla ya dakika haijaisha.

“Unahisi huyu jamaa anasifa gani kubwa, kuliko wenzake tuliowataja?” Rich'one aliuliza.

“Huyu jamaa anapiga kila aina ya mapigo unayoyajua, anapiga hadi suplex lakini kubwa zaidi, huyu jamaa ni mdunguaji aliyekamilika”

Wenzake walitumbua macho kwa kutomuelewa, nae akaamua kuwaelewesha.

“Hii ni kazi ya nje ya nchi na hatuwezi jua ataenda kukabiliana na magumu gani huko aendako na atatumia mbinu gani, kuhakikisha kila kitu kinaenda vile ilivyopangwa. Ni vema kumpeleka mtu ambae anajua kila aina ya mapambano ili lengo letu litimie” Alinyamaza tena na kuwatizama wenzake, kisha akaendelea kumpamba Miguu ya Kuku.

“Huyu jamaa angelikuwa mwanajeshi basi, angelikuwa anashikilia rekodi ya mdunguaji bora duniani. Anaweza kudungua kitu chenye unene wa kidole, akiwa umbali wa mita mia tano. Pia anaweza kubapata shabaha yake ndani ya sekunde mbili tu, baada ya kufyatua risasi ya kwanza. Anakimbia mita mia moja kwa sekunde nane tu, pia aliitwa Miguu ya Kuku kwa sababu hatoi kishindo na mguu wake mmoja una vidole vinne tu. Sasa kwa sifa hizo kuna mdunguaji gani hapa duniani anaweza kumfikia? Nani anaweza kupambana nae ikiwa anapiga kila aina ya mipigo pia, anatumia akili nyingi kupata windo lake kuliko nguvu.” Alfa’one akatua maelezo yake.

“Duh, huyu kweli kiboko!” Omega’one akaongea kwa mshangao huku akijiweka sawa kwenye kiti.

“Hata mimi ameanza kuniingia hivi” Rich’one nae akaunga hoja.

“Lakini nisingependa nichukue mawazo yenu, nataka tujiridhishe na uwezo wa watu hawa wote, kabla hatujatuma mtu huko Goma.” Alfa'one aliwambia wenzake.

“Unataka kusema nini tena?” Omega’one aliuliza.

“Nataka tuwachambue kwanza” Alijibiwa.

“Uchambuzi tena wa nini ikiwa sifa zote umempa? Haina haja bwana, kuendelea kumjadili ni kupoteza rasilimali muda.”

“Hapana Boy. Lengo langu nataka tupate mtu miongoni mwa watu. Mtu wa kazi, mtu anaweza kuwakalisha watu wengine wenye sifa kama zake”

“Eleza lengo lako, pengine tunaweza kuelewana.”

“Namaanisha hawa watu wote watatu tuwapambanishe hapa mjini, kisha mshindi apewe kazi ya kwenda huko Goma”

“Lakini unajua hawa watu huwa hawatoi jasho bila kulipwa?”

“Hilo nalijua, lakini tusiogope garama kama tunahitaji kupata mali zetu zenye ukwasi wa kutosha. Wapewe kazi ya kutafutana wao kwa wao, kisha mbabe anapewa tenda”

“Lakini unajua hawa mamluki mara nyingi huwa hayapendi kushindwa, inaweza kutoke mmoja akashindwa lakini akaenda kuanzisha vita itakayochafua mji wote wa Dar es laam”

“Hapa sheria itakayotumika si kumuacha aliyeshindwa akiwa hai. Hapa inabidi ipigwe DOA mzee.”
“DOA! Unamaana gani?”

“Namaanisha Dead or Alive”

“Hii ni hatari sasa na wakigundua tunawachezeshea kamari na wakatugeuka itakuwaje?”

“Usisahau wewe ni mstaafu ambae umepigana vita ndani ya Katanga, Kivu yote ukiwa chini ya amri ya walinda amani na, kumbuka; once a soldier always remain a soldier na, mwenye akili ndiye mshindi”

Ukapita ukimya kila mmoja akiwaza lake.

“Alfa yupo sahihi, lazima tuchuje pumba na mchele ili tusije kimbilia tui, tukidhani ni maziwa.” Rich’one alikubaliana na hoja.

“Tuko pamoja Boys” Omega’one alikubaliana na wenzake, kisha akauliza.

“Hatua gani zinafuata?”

“Kila mtu ampe taarifa mtu wake, kisha wote wakutane jengo la mauzo, gorofa namba tano kwenye duka la simu na wachukue mkoba mweusi watakoukuta humo” Alfa alitoa mkakati wake.

“Sasa itakuwaje mmoja akiwahi kuuchukua mkoba na kuufikisha sehemu husika kabla ya wenzake?” Rich’one alitoa wasiwasi wake.

“Mamluki hawako hivyo, huwa hawana haraka ya kioga hivyo na kazi yoyote mezani kwao, huwa ni kiashiria cha hatari hata kama kapewa kazi ya kumchamba mtoto, ni lazima atie wasiwasi” Alfa alifafanua.

“Basi waingie mzigoni kesho”

“Yeah, Kesho mji utachafuka si kitoto”

“Hahaa! Sisi ndo wazee vijana, Boys among men…” Alfa alicheka kifedhuli huku akiichukua simu yake ya garama kubwa na kulitafuta jina la Miguu ya Kuku.

Wakati yeye akiwasiliana na Miguu ya Kuku, Omega yeye alikuwa anawasiliana na Kiuno cha nyoka na Rich’one aliwasiliana na Tembe za chai.

Walikuwa wanatengeneza bomu la kulipua nyoyo za wakazi wa jiji la Dar es laamu na viunga vyake.
Lakini kitu ambacho hawakujua ni kuwa, chatu hafugwi ndani ya nyumba, kwa kuwa ipo siku atakugeuka.

Dar ikawa ya moto.

*****
Endelea kuwa nami hadi mwisho wa kazi hii
 
Nelly

JF-Expert Member
Jan 25, 2020
1,433
2,000
RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA

SIMU; 0758573660/062155629

shusha vitu mkuu☝☝☝
 
Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,768
2,000
RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SIMU; 0758573660.

SEHEMU YA PILI.

Walikuwa wanatengeneza bomu la kulipua nyoyo za wakazi wa jiji la Dar es laamu na viunga vyake.
Lakini kitu ambacho hawakujua ni kuwa, chatu hafugwi ndani ya nyumba, kwa kuwa ipo siku atakugeuka.

Dar ikawa ya moto.

*****

Zuki Gado alimaarufu kwa jina la Miguu ya Kuku, alikuwa ni mkazi wa Tegeta kwa ndevu. Mara nyingi Zuki alipenda kukaa vijiweni akipiga soga na watu wa rika tofauti, hakujali umri wao, yeye alipenda kuwa mtu wa watu; alisaidia palipohitajika na alishiriki kila aina ya tukio kwenye mitaa yake. Zuki Gado p.a.k Miguu ya Kuku, alifahamika hadi na kuku wa mtaani. Watu walimsifu na kumuona ni mwema na asie na majivuni, kipato chake alikitumia kugawana na masikini mtaani kwake.

Licha ya kusaidia kila mara, lakini hakuna aliyefahamu kipato chake alikitoa wapi kwa maana, hakuwa mtu wa kazi wala kuonekana akisimamia biashara. Yeye alikuwa ni mtu wa kupotea na kuonekana baada ya siku au miezi kadhaa.
Kila alipoonekana baada ya kupotea machoni mwa wenyeji wake, alikuwa akija na gari jipya ama pikipiki mpya na yenye thamani kubwa. Nyumbani kwake kulikuwa ni sawa na uwanja wa maonesho ya magari, kulikuwa na gari nyingi zilizotosha kuutambulisha ukwasi wake.

Licha ya kuwa na gari nyingi, lakini hakuna gari ambayo ilifikisha thamani ya tsh milioni themanini, zote zilikuwa ni chini ya hapo.

Zuki Gado siku hiyo ya ajabu kwake, ilimkuta akiwa amekaa kwenye kijiwe cha kahawa, huku akipiga soga za hapa na pale.

Ilianza kuita simu na hakuhangaika kuipokea. Ulikuwa ni utaratibu wake wa kila siku, kupokea muito wa pili wa simu. Alifanya hivyo ili kujiepusha kupokea simu zisizokuwa na manufaa kwake.

Simu yake haikuita tena na badala yake, saa yake ya mkononi ilitoa mlio fulani mara mbili na kunyamaza.

Alikuwa anakaribia kuweka kikombe cha kahawa mdomoni, akasita na kukirejesha mezani, kisha haraka alisimama na kuaga pale kijiweni, huku akijichekesha kirafiki na muuza kahawa.

Hakudaiwa pesa kwa kuwa ilikuwa ni utaratibu wake, kunywa na kulipa pesa bila kudai chenji, hivyo basi, hata akinywa bila kulipa hakuna ambae alijali.

Uharaka wake wa kutoka kijiweni ulichangiwa na muito wa saa yake. Kwa mtu mwingine angelidhani ni muito wa taarifa, kutoka saa moja kwenda saa nyingine, lakini kwake ilikuwa ni zaidi ya muito.
Ilikuwa ni muito wa wito, nae hakutaka kuupuza wito huo.

Kijiwe cha kahawa hakikuwa mbali na nyumbani kwake, hivyo alitumia dakika chache kufika ndani kwake na kuelekea chumbani kwake.

Huko alikaa kitandani na kuivua saa yake, kisha aliuvuta ufunguo wa saa na kuifanya saa yake itoe mlio mara tatu mfululizo.
Mlio ulipokoma, kulifuatia utokaji wa karatasi nyembamba pembeni kidogo ya sehemu ya ufunguo wa kurekebishia majira ya saa ile.
Aliivuta karatasi ile iliokuwa imetumwa kwa njia ya fax. Alipohakikisha imetoka yote, aliweka saa yake pembeni na kukisoma kikaratasi kile.

“Email” Ujumbe ulisomeka vile.

Haraka alikiweka mdomoni kikaratasi kile na kuanza kukitafuna huku mikono yake, ikidaka simu yake aliyokuwa ameiweka kwenye meza ndogo iliokuwa pale chumbani.

Haraka aliwasha data na kuelekea moja kwa moja, upande wa faili la barua pepe, huko alikutana na ujumbe kutoka kwa mtu aliyejiita Boy1. Ujumbe ule ulisomeka hivi….

‘Jengo la mauzo,F5. Mweusi mkoba.’ Aliusoma kwa umakini, kisha akaamua kuujibu ujumbe ule.

“Nitanunua gari ama pikipiki?” Alisubiri kidogo na punde aliona ujumbe wake umesomwa, nae alikaa mkao wa kungoja majibu.

“Gari mpya kabisa” Alijibiwa.

“Nipe gari na pikipiki nikuletee utakacho” Alituma tena ujumbe huo na kungoja majibu.

“Ondoa shaka, natanguliza gari sasa hivi kisha ukileta nitakacho, nitakupa pikipiki” Alijibiwa.

Akafikiria kidogo huku akitaka kufuta jumbe zote, mara akakumbuka kitu na haraka akaandika..

“Ni lazima iwe kesho?” akatuma ujumbe huo.

“Wahi nikuwahi, lazima iwe kesho” Alijibiwa.

Aliishia kutabasamu kivivu, huku akifuta jumbe zote kwenye kikasha cha simu cha kuhifadhia barua pepe.

Siku zote hakutaka kuwa mtu wa kuingia mtegoni kizembe. Alihakikisha anapata taarifa sahihi kutoka kwa mtu yeyote ambae angelimpa kazi. Alitumia ujanja wa hali ya juu kupata uzito wa kazi kupitia ukubwa wa malipo. Mara nyingi alipenda kuulizia gari ama pikipiki na, kama tajiri angelisema atamnunulia pikipiki, ilikuwa na maana kazi ni ndogo na nyepesi na pengine isingeligusisha umwagikaji damu. Lakini kama tajiri angelitamka gari kama malipo, basi alijua kazi ni kubwa na itagarimu uhai wa mtu. Pia kama tajiri angelikubali kulipa pikipiki na gari, ilimaanisha kazi ni ya ufundi wenye kunuka damu.

Hivyo wakati anawasiliana na mtu aliyejiita Boy, alitumia njia zake za kila siku ili kujua ukubwa wa kazi. Mbinu hiyo ilimsaidia sana kwa kuwa, tajiri yake alijua jamaa ni mpenda magari hivyo garama za kazi, ilikuwa ni lazima zivuke thamani ya gari au pikipiki za bei kubwa na hapo ilikuwa ni zaidi ya milioni mia moja.

Matajiri wake hawakuwahi kujua ile ilikuwa ni njia yake ya kujua ukubwa wa kazi, pia hawakujua yeye alinunua magari kila alipotoka kumwaga damu kwenye kazi au hununua pikipiki kila anapotoka kufanya kazi bila kumwaga damu.

Miguu ya kuku alijua kuwatega bila wao kujua.

*****

Baada ya kupata taarifa za kazi aliotakiwa kuifanya, Miguu ya kuku alikaa kitandani na kutafakari uzito wa kazi iliokuwa mbele yake. Akiwa katikati ya mawazo, simu yake iliingiza ujumbe mfupi na alipousoma, uso wake ulichanua kwa tabasamu maridhawa.

Ulikuwa ni ujumbe kutoka bank, uliomtaarifu kufanyika kwa malipo ya milioni mia na hamsini,kutoka kwenye kampuni ya uuzaji magari.

Aliufuta ujumbe ule ambao alijua ulimaanisha ni pesa ya awali kwenye dili alilopewa.
“Wahi nikuwahi..” Alijisemea baada ya kukumbuka ujumbe wa mwisho kutoka kwa Boy.

“Ina maana kuna mtu mwingine anauhitaji huo mzigo na huyo mtu ndiye hatari bila shaka hadi nimepewa pesa ya kutakata” Alijiwazia huku akivua nguo alizokuwa amevaa, kisha alitungua kanzu yake safi kutoka kwenye henga.

Aliivaa na kisha alichukua baraghashia yake na kuiweka kichwani. Alijitizama kwenye kioo na kuridhika na mwonekano wake, kisha alifungua kabati lake na kutoka sanduku dogo la chuma.

Alilifungua sanduku lile na macho yake yalikaribishwa na silaha kadhaa zenye ubora aliouhitaji. Mkono wake wa kulia ulianza kudaka kisu, kisha ukadaka bastola yenye kiwambo.

Alipohakikisha kila kitu kipo sawa, alifunga lile sanduku na kulirejesha kwenye kabati.

Alifunga kabati vizuri, kisha alichukua silaha zake na kuzihifadhi mwilini mwake na kuhakikisha hazionwi na mtu na anazifikia kwa wepesi zaidi atakapozihitaji.

Zuki Gado p.a.k Miguu ya kuku alitoka nje na kuufunga mlango wake vizuri, kisha aligeuka upande wake wa mashariki na kutazama upande wake maegesho ya magari yake.

Kwa harakaharaka macho yake yalikutana na gari zaidi ya thelathini. Aliyatazama magari yale kama anaeyashangaa, kisha aligeuka upande wake wa magharibi na kukutana na maegesho ya pikipiki za bei mbaya, zaidi ya hamsini na mbili.
Alitikisa kichwa na kutabasamu huku akijipongeza kwa kazi kubwa alioifanya na kupata idadi ile ya pikipiki na gari.

Kwake aliona ni ushindi kuwa na pikipiki nyingi kuliko gari, kwa sababu, kwake alichukia sana kuua mtu kwenye kazi yake yoyote, hivyo kuwa na gari chache ilimaanisha, aliua watu wachache. Pia kuwa na pikipiki nyingi, ilimaanisha alifanikisha kazi nyingi bila kumwaga damu.

Aliipongeza akili yake kwa kuwa na uwezo wa kufanya kazi bila kuua watu wengi, tofauti na mamluki wengine.
Licha ya kuwa na gari nyingi na pikipiki kwenye uwanja wa nyumba yake, lakini aliamua kutozitumia na badala yake, aliamua kuelekea katikati ya jiji kwa kutumia daladala.

Siku zote Miguu ya kuku hakupenda purukushani na serikali, hivyo aliamini akitumia moja ya gari zake, ingelikuwa ni kujichokonoa mwenyewe.

*****

Alipanda daladala zilizokuwa zinaelekea moja kwa moja katikati ya mji, zikitokea Boko. Alipanda na kukaa kwenye kiti kama abiria wengine kisha alitulia na kuanza kutafakari mawili matatu.

Miguu ya kuku aliiheshimu kazi yake vilivyo, hivyo badala ya kwenda kesho yake kama alivyokuwa ameelekezwa, yeye aliamua kwenda siku hiyo hiyo. Aliamua kwenda si kwa lengo la kuuchukua huo mzigo, bali aliamua kwenda kulichunguza jengo la mauzo lilivyo, ili endapo lingejitokeza jambo katikati ya misheni yake, ajue ni wapi angelitakiwa kukimbilia na kujiokoa.

Wakati yeye akidhani ni yeye mwenye akili za kukagua mazingira kabla ya kazi, alijidanganya.

Kulikuwa na mtu mwingine nae alikuwa na kazi kama yake na, yeye alipenda kukagua mazingira kabla ya kazi na, jioni hiyo na yeye alikuwa anaenda kwenye jengo la mauzo kuweka mambo yake sawa.

Wote wawili walijikuta wakianza kazi kabla ya siku iliotakiwa. Walianza mtafutano kabla ya wakati.

Mtu huyo alikuwa ni mtaalamu wa mapigano na kuruka viunzi. Kujikunja na kujikunjua kwa kasi, kulifanya apachikwe jina la Kiuno cha nyoka, badala ya jina lake Said Magabe.

Jengo la mauzo lilijuta kuwafahamu viumbe wale kwa siku hiyo.

Moto ukawaka!...
 
Man the one

Senior Member
Jan 12, 2018
155
225

Mbona kimbembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MoseRose

JF-Expert Member
Sep 5, 2017
276
1,000

Simulizi nzuri.Inavutia sana.Hongera mtoa post.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MoseRose

JF-Expert Member
Sep 5, 2017
276
1,000
RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA

SIMU; 0758573660/062155629

-----1------

Kikao cha watu watatu kiliendelea na kila Mjumbe, tayari alishatoa wazo lake aliloona ni sahihi kwa wakati huo. Makubaliano ya hapa na pale yalifikiwa, lakini ukaibuka utata kwenye hitaji lao la mwisho, na lilowafanya wakutane siku hiyo.

Maongezi yao yalihama kuwa ya kibiashara, yakaelekea kuwa ya kibabe na kila mmoja akitaka hoja yake ipite bila kupingwa.

Wazee hawa wenye umri sawa, walivimbiana huku kila mmoja akijinasibu kwa sifa zake, achilia mbali uwezo wa fedha na, mali walizomiliki ambapo; Mali zote hazikupatikana kwa njia halali na hilo ndilo, lilifanya uibuke mzozo, kwa kuwa kila mmoja alikuwa na aina ya watu ambao, aliwatumia ili kutimiza ujazo wa mifuko yake.

Ukiachilia mbali wazee hawa kuibuka kuwa wenye ukwasi wa kutisha, pia walikuwa ni wasitaafu wa jeshi, wakiwa na vyeo vya chini kabisa.

Kila aliyewafahamu, alijiuliza ukwasi huo waliupata vipi ikiwa, mafao yao yalikuwa hayawezi kuwafikisha kwenye kilele cha ubilionea. Wengine walidhani watakuwa walienda kuroga ili wasife masikini, huku wengine wakidhani walikopa bank ili waziishi ndoto zao.

Mengi yalisemwa, lakini ni wao waliofahamu ukwasi huo waliupata vipi.

Wakati watu wakishangaa utajiri huo wa baada ya kustaafu, lakini wao walianza kuuishi miaka mingi hata wingali kazini. Waliufanya kuwa siri, huku wakiendelea kufanya unyama wa hapa na pale, ili kutunisha hazina zao.

Lakini waliendelea kujivika mwamvuli wa kazi, huku kazi zao zikifanywa na watu maalumu wa kukodi. Watu hawa maalumu ndiyo waliozua zogo kwenye kikao chao hicho, kila mmoja aliamini mtu wake ni sahihi kuifanya kazi waliokusudia kuifanya.

Si kwamba watu hao wa kununua hawakuwafahamu kwa ujumla wao; la hasha, waliwafahamu vema lakini, kila mmoja alimwamini yule alieyefanya nae kazi kwa muda mrefu na kwa uaminifu mkubwa.

“Jamani eeh, hebu tusigombane. Sisi sote ni BoysAmongMen, ni lazima tukubaliane kwa sauti moja bila kukwazana” Alizungumza Mzee mmoja ambae hupenda kujiita Rich'one.

Ukapita ukimya mfupi huku kila mmoja akijaribu kushusha morali yake.

“Mimi bado naona hii kazi tumpe Kiuno cha nyoka, huyu bwana anaijua kazi yake vilivyo na mazingira yoyote anaweza kufanya kazi yake.” Alizungumza mzee mwingine, ambae alipenda kujiita Omega'one.

“Lakini nabaki na msimamo wangu, Kiuono cha nyoka hawezi kuifanya kazi hii. Kwanza anatamaa sana, pia ni mtu asie na msimamo kabisa. Akipata dili lenye pesa kubwa, ni rahisi kuitosa kazi yetu.” Alizungumza Rich'one huku akiwatizama wenzake kwa umakini, kuona kama hoja yake inawaingia.

“Tukisema kila mmoja ampambe mtu wake, hakuna mbabe kati yao, maana, kila mmoja atakuwa na sifa sawa na zile za mwenzake kwa kuwa, sifa zote zitakuwa ni za weledi wa kufanya kazi kwa usahihi” Omega aliongea huku akiwatizama wenzake kwa utulivu mkubwa na kufanya umakini, uongezeke miongoni mwao.

Alipohakikisha wenzake wametulia na wanamsikiliza, aliendelea.

“Sifa zote tumezisikia na sasa ni wakati wa kuweka majina yote mezani, kisha tuchambue sifa zao zote kwa umakini na, tutoke na jina moja lenye nguvu.”

Mzee aliyependa kujiita Omega'one alikaa vema kwenye kiti, huku akisubiri wenzake watekeleze wazo lake.

“Mm-mh-mh-...” Mzee mwingine ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu, alirekebisha koo na kujiweka vema ili aongee jambo lake.

Wenzake walikaa kimya na kumsikiliza.

“Mawazo yenu yako sawa kabisa. Boys among men, daima huwa hatogombani kirejareja namna hii, bali huwa tunaamua wazo moja lenye tija.” Alinyamaza kidogo na kuwatazama wenzake, kisha alipoona wanamsikiliza, aliendelea..

“Mmewataja watu wenu na sifa zao; mmemtaja Kiuno cha nyoka na
Tembe za chai, kama ni watu makini na hatari kwenye kufanikisha matukio makubwa na yenye kuogofya.” Alinyamaza na kuwatizama tena wenzake, ambao walikuwa wamekaa kimya wakimsikiliza.
Aliendelea..

“Lakini pengine hamjapima uzito wa Nazi hii tunayowapa. Kazi hii inaugumu kwa kiasi kikubwa na inahitaji mtu makini sana na mwenye kutumia akili, kuliko nguvu na uchawi. Mtu huyu pia awe ni mwenye ujuzi wa mapigano na mwenye kujua kuitumia vema silaha yoyote, awe ni mwenye kuendesha chombo chochote cha moto, awe ni mtu ambae amefunga mkataba na kifo, wakati wowote kikimuita yuko tayari kukipokea. Mtu huyu awe zaidi ya komando wa jeshi la uzunguni.” Mzee yule alimaliza kuongea na kuegemea mwenye kiti alichokalia, huku macho yake yakihama; kutoka kushoto kwenda kulia na kulia kwenda kushoto. Aliwatizama wenzake ambao walikuwa kimya wakitafakari uzito wa hoja ya Alfa'one, ambae mara nyingi walimheshimu kwa busara zake miongoni mwao.

“Kwa hiyo unashauri tuachane na hawa jamaa?” Rich'one alimuuliza.

“Hapana! Hawa hawa wanatosha, lakini tuchague mmoja ambae anaweza kupiga vita peke yake kwenye nchi ngeni” Alijibu.

“Unahisi ni yupi anaefaa kuibeba kazi hii?” Omega'one aliuliza.

“Wote wanafaa kuibeba kazi hii, lakini nampendekeza zaidi huyu jamaa anaeitwa Miguu ya Kuku.”

Ukapita ukimya mfupi kila mmoja akitafakari la kwake kisha, ukimya ule ukavunjwa kabla ya dakika haijaisha.

“Unahisi huyu jamaa anasifa gani kubwa, kuliko wenzake tuliowataja?” Rich'one aliuliza.

“Huyu jamaa anapiga kila aina ya mapigo unayoyajua, anapiga hadi suplex lakini kubwa zaidi, huyu jamaa ni mdunguaji aliyekamilika”

Wenzake walitumbua macho kwa kutomuelewa, nae akaamua kuwaelewesha.

“Hii ni kazi ya nje ya nchi na hatuwezi jua ataenda kukabiliana na magumu gani huko aendako na atatumia mbinu gani, kuhakikisha kila kitu kinaenda vile ilivyopangwa. Ni vema kumpeleka mtu ambae anajua kila aina ya mapambano ili lengo letu litimie” Alinyamaza tena na kuwatizama wenzake, kisha akaendelea kumpamba Miguu ya Kuku.

“Huyu jamaa angelikuwa mwanajeshi basi, angelikuwa anashikilia rekodi ya mdunguaji bora duniani. Anaweza kudungua kitu chenye unene wa kidole, akiwa umbali wa mita mia tano. Pia anaweza kubapata shabaha yake ndani ya sekunde mbili tu, baada ya kufyatua risasi ya kwanza. Anakimbia mita mia moja kwa sekunde nane tu, pia aliitwa Miguu ya Kuku kwa sababu hatoi kishindo na mguu wake mmoja una vidole vinne tu. Sasa kwa sifa hizo kuna mdunguaji gani hapa duniani anaweza kumfikia? Nani anaweza kupambana nae ikiwa anapiga kila aina ya mipigo pia, anatumia akili nyingi kupata windo lake kuliko nguvu.” Alfa’one akatua maelezo yake.

“Duh, huyu kweli kiboko!” Omega’one akaongea kwa mshangao huku akijiweka sawa kwenye kiti.

“Hata mimi ameanza kuniingia hivi” Rich’one nae akaunga hoja.

“Lakini nisingependa nichukue mawazo yenu, nataka tujiridhishe na uwezo wa watu hawa wote, kabla hatujatuma mtu huko Goma.” Alfa'one aliwambia wenzake.

“Unataka kusema nini tena?” Omega’one aliuliza.

“Nataka tuwachambue kwanza” Alijibiwa.

“Uchambuzi tena wa nini ikiwa sifa zote umempa? Haina haja bwana, kuendelea kumjadili ni kupoteza rasilimali muda.”

“Hapana Boy. Lengo langu nataka tupate mtu miongoni mwa watu. Mtu wa kazi, mtu anaweza kuwakalisha watu wengine wenye sifa kama zake”

“Eleza lengo lako, pengine tunaweza kuelewana.”

“Namaanisha hawa watu wote watatu tuwapambanishe hapa mjini, kisha mshindi apewe kazi ya kwenda huko Goma”

“Lakini unajua hawa watu huwa hawatoi jasho bila kulipwa?”

“Hilo nalijua, lakini tusiogope garama kama tunahitaji kupata mali zetu zenye ukwasi wa kutosha. Wapewe kazi ya kutafutana wao kwa wao, kisha mbabe anapewa tenda”

“Lakini unajua hawa mamluki mara nyingi huwa hayapendi kushindwa, inaweza kutoke mmoja akashindwa lakini akaenda kuanzisha vita itakayochafua mji wote wa Dar es laam”

“Hapa sheria itakayotumika si kumuacha aliyeshindwa akiwa hai. Hapa inabidi ipigwe DOA mzee.”
“DOA! Unamaana gani?”

“Namaanisha Dead or Alive”

“Hii ni hatari sasa na wakigundua tunawachezeshea kamari na wakatugeuka itakuwaje?”

“Usisahau wewe ni mstaafu ambae umepigana vita ndani ya Katanga, Kivu yote ukiwa chini ya amri ya walinda amani na, kumbuka; once a soldier always remain a soldier na, mwenye akili ndiye mshindi”

Ukapita ukimya kila mmoja akiwaza lake.

“Alfa yupo sahihi, lazima tuchuje pumba na mchele ili tusije kimbilia tui, tukidhani ni maziwa.” Rich’one alikubaliana na hoja.

“Tuko pamoja Boys” Omega’one alikubaliana na wenzake, kisha akauliza.

“Hatua gani zinafuata?”

“Kila mtu ampe taarifa mtu wake, kisha wote wakutane jengo la mauzo, gorofa namba tano kwenye duka la simu na wachukue mkoba mweusi watakoukuta humo” Alfa alitoa mkakati wake.

“Sasa itakuwaje mmoja akiwahi kuuchukua mkoba na kuufikisha sehemu husika kabla ya wenzake?” Rich’one alitoa wasiwasi wake.

“Mamluki hawako hivyo, huwa hawana haraka ya kioga hivyo na kazi yoyote mezani kwao, huwa ni kiashiria cha hatari hata kama kapewa kazi ya kumchamba mtoto, ni lazima atie wasiwasi” Alfa alifafanua.

“Basi waingie mzigoni kesho”

“Yeah, Kesho mji utachafuka si kitoto”

“Hahaa! Sisi ndo wazee vijana, Boys among men…” Alfa alicheka kifedhuli huku akiichukua simu yake ya garama kubwa na kulitafuta jina la Miguu ya Kuku.

Wakati yeye akiwasiliana na Miguu ya Kuku, Omega yeye alikuwa anawasiliana na Kiuno cha nyoka na Rich’one aliwasiliana na Tembe za chai.

Walikuwa wanatengeneza bomu la kulipua nyoyo za wakazi wa jiji la Dar es laamu na viunga vyake.
Lakini kitu ambacho hawakujua ni kuwa, chatu hafugwi ndani ya nyumba, kwa kuwa ipo siku atakugeuka.

Dar ikawa ya moto.

*****
Endelea kuwa nami hadi mwisho wa kazi hii
Kudos #Kudo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom