Mdunguaji wa Goma

Mdunguaji wa Goma

RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA SITA.

Wakati Miguu ya kukua anafanya yaliondani ya uwezo wake, Tembe za chai alikuwa amepigwa na butwaa huku akiwa na pikipiki yake, akiwa hajui cha kufanya.

Ni kweli alikuwa na nia ya kumuua kiuno cha nyoka, lakini uwepo wa polisi ilikuwa kikwazo na, tena polisi walikuwa na silaha na yeye hakutaka kujeruhiwa kizembe.

Yeye akiwa anafikiria, ndipo alipomuana Miguu ya kuku akifanya vitu vyake kwa uwezo mkubwa, huku akitumia pikipiki aina ya boxer. Pikipiki ambayo haikuwa na uwezo mkubwa, kama aliokuwa nayo yeye.

Ilimshangaza. Tena ilimshangaza zaidi alipoona jamaa akiondoka, bila risasi za polisi kumwangusha bali, ni yeye ambae alimwacha kiuno cha nyoka akiwa hana uhai, kwenye mikono ya polisi.

“Duh!!” Alishangaa huku akiwasha pikipiki yake na kuanza kumfuatilia Miguu ya Kuku.

Tembe za chai aliamini siku zote ni yeye aliestahili kupambana na watu wa aina ile. Aliamua kumfuatilia Miguu ya Kuku.

Kitu ambacho hakujua ni kuwa, Miguu ya Kuku nyayo zake hazifuatwi abadani.

Aliufuata moto.

****

Majira ya saa mbili za usiku, yalimkuta Miguu ya Kuku akiwa ndani ya nyumba yake, huku maji ya moto yakiwa mbele yake.
Maji yale aliyatumia kusafishia jeraha lake kwenye mkono wa kushoto. Jeraha lile lililokuwa limetokana na kashikashi alioifanya katikati ya jiji.

Pembeni yake kulikuwa na; mkasi, kisu kidogo pamoja na pamba. Juu kidogo ya kiwiko chake, mkono wa kushoto, alikuwa amefunga na kamba kando ya jeraha. Alifanya vile kwa kuwa alitaka kuichomoa risasi iliokuwa imekwama kwenye nyama.
Alipohakikisha kila kitu kipo kama alivyotaka, aliikaza vema kamba aliokuwa amejifunga, kisha alichukua kijiti na kukiweka mdomoni. Alichukua mkasi na kuuingiza kwenye jeraha, kisha alivuta risasi iliokuwa imekwama huku akigugumia kwa maumivu makali. Alijichomoa risasi bila kutumia ganzi, alitumia kung'ata kijiti kama njia ya kujipunguzia maumivu.

Aliweka pembeni mkasi uliokuwa na risasi, kisha alichukua pamba iliokuwa na dawa ya kukata maumivu na kuzuia kuvuja damu, aliipitisha kwenye jeraha huku akiugulia maumivu yalioongezewa na dawa. Alipohakikisha dawa imegusa pahala pake, alitupa kila kitu pembeni na kujilaza kwenye kiti chake mithili ya mzee anaevuta mtemba.

Macho yake yaliangalia juu huku akitafakari mawili matatu.

“Kazi hii itanilazimu niiache, japo nimrudie Mungu wa kweli, kabla sijakutana na kiama” Alijiwazia huku akikumbuka namna alivyokuwa akikwepa risasi na aina nyingine za silaha, awapo kwenye mapambano.

“Nina kila kitu, lakini sina familia. Natakamani kuwa nayo, lakini matendo yangu hayaniruhusu. Naogopa wanangu kurithi kazi kama hii” Aliwaza tena huku akikaa vizuri kwenye kiti na kuchukua kitambaa kisafi na kukiloweka kwenye maji ya moto. Alipohakikisha kimepata unyevunyevu aliouhitaji, alikitoa na kukikamua kidogo kisha, alikitumia kujifuta damu zilizokuwa zimegandia.

Alilisafisha vema jeraha lake na kujifungua kamba, aliweka vifaa tiba vyake pamoja na kusimama kwa nia ya kutoka, kwenye chumba chake cha siri kilichokuwa ndani ya nyumba yake.

Kabla hata hajapiga hatua yoyote, umeme ulikatika na nyumba nzima ilimilikiwa na giza la kutisha.

Alisonya huku akitulia ili macho yake yapate kuzoea giza.

“Tanesco huwa wanaota kukata umeme tu, bila kujali adha wanazowapa wateja wao…” Alimalizia na sonyo kubwa huku mkono ukirejesha vifaa tiba vyake.

Akilini mwake alijua dakika moja iliofuata, jenereta la pale nyumbani kwake lingejiwasha. Lakini hadi hiyo dakika inakatika, hakuona mwanga wowote ukirejea.

Wasiwasi ukamvaa, mwili ukamwingia ubaridi wa kutisha. Alihisi tayari amehujumiwa akiwa nyumbani kwake.

Mawazo yake yalisafiri haraka na kukumbuka songombingo, lililotokea saa chache zilizopita na, akili yake ikamkumbuka vema mtu wa tatu aliyeingilia ule mchezo, kwenye jengo la mauzo. Licha ya kumuona hata wakati akilishambulia gari la kiuno cha nyoka, ajabu alijikuta akimsahau na kurejea nyumbani bila kujua hatima ya yule mtu.

“Kwani naelekea kuzeeka!? Mbona naanza kuwa mzembe?” Alishangaa na kujiuliza peke yake, huku akipekua vifaa vyake na kukiokota kisu.

“Lakini binaadamu wanadharau sana. Yaani unamfuata mtu kwake na kumzimia umeme!” Alijisemea huku akipapasa ukuta. Alikuwa anatafuta sehemu ya kumtoa ndani ya kile chumba chake.

Mkono wake wa kulia ulipata sehemu alioihitaji, haraka alivuta kamba alioishika na nafasi ndogo mithili ya dirisha za kizuizini ilipatikana. Kwa wepesi wa aina yake, Miguu ya Kuku alijipinda na kuwa kama mtoto mdogo aliekaa kwenye tairi bovu, kisha alijiachia na kupita kwenye kinafasi hicho mithili ya nyoka pangoni.

Kidirisha kile kilimfikisha kwenye njia nyembamba, ambayo alikuwa ameijengea ukuta mwembamba ambao kamwe, hakuna mtu angelidhani kuna njia ya kupitisha kiumbe mwenye miguu miwili. Kama ungelifanikiwa kuuona ukuta ule, basi ungelidhani ni njia ya kupitishia bomba la maji taka ama uchafu wowote, kutokea jikoni.

Njia ile ambayo ni yeye alijua uwepo wake, ilimfikisha kwenye kijumba kidogo ambacho, kilijengwa kama vijumba vya kuchomea taka, kwenye maabara za hospitali.

Kijumba kile nacho hakikuwa na mlango, bali kilikuwa na vidirisha vidogo ambavyo kamwe, usingelidhani vinaweza kupitisha kiumbe hai mwenye mikono miwili na miguu miwili.

Lakini Miguu ya Kuku ile ilikuwa ni sehemu yake ya kutokea na, aliijenga maalumu kwa kazi hiyo, huku kila mara akipiga mazoezi namna ya kupita kwenye vidirisha vidogo namna ile.

Hivyo alikuwa anapita sehemu ambazo alijua zinapitika vipi, wala hakupata kazi kupita kwenye kidirisha kimojawapo na kutoka nje, huku akiwa na kisu chake mkononi.

Alipoigusa ardhi yenye nyasi, ndipo alipogundua umeme ulikuwa umekatika nyumbani kwake, huku sehemu nyingine kukiwa na mwangaza wa kutosha.

“siku zote huwa naamini hisia zangu.” Alijisemea huku akipiga hatua taratibu bila kutoa vishindo, umakini ukiwa upo nae sambamba. Hakutaka kufanya kosa ambalo lingekuja kumgarimu, ukizingatia, hakujua ni nani amemvamia nyumbani kwake na alikuwa na lengo gani.

Alitembea taratibu hadi alipolifikia geti la nyumba yake na, alipolikagua aligundua halikuwa wazi. Hiyo ilimaanisha mvamizi alikuwa ameruka ukuta na kuingia ndani ya nyumba yake, kisha kumkatia umeme.

“Baboon!” Neno lilimtoka bila kupenda. Neno hilo lilimaanisha aina ya nyani waishio bara Amerika. Alipenda kulitumia kila alipohisi hatari ya kiwango cha juu kabisa.

“Huyu jamaa anadharau sana. Kunifuata kwangu ni dharau kubwa sana aisee.” Alijisemea huku akiokota mchanga chini, kisha aliuhesabu kwa idadi na, alipopata idadi ya vipande sita vya mchanga, alivitia mdomoni.

Wakati alipokuwa akisimama baada ya kuokota mchanga, masikio yake yalihisi sauti ya mkimbio wa kiumbe hai. Kiumbe ambae alikuwa anatumia ncha ya viatu vyake ili asitoe kishindo na, alipoinua uso wake, aliona kivuli cha mtu kikimfuata kwa kasi kubwa ambayo haikuitarajia na, kabla hajasimama vema, alijikuta akichezea mateke mawili ya kifua na kwenda chini bila kupenda.

Licha ya kuanguka, lakini hakufungua mdomo wake ili kutema mchanga wote, ambao aliufumbata chini ya ulimi na badala yake, aliinua ulimi kidogo na kutema mchanga mmoja tu na,mdomoni alisalia na vipande vitano vya mchanga.

Alipojaribu kuinuka, alijikuta akirudi chini huku ubavu wake wa kushoto ukipokea maumivu makali, kiasi alishindwa kuhimili na kujikuta akiguna kwa maumivu.

Kama kawaida kila aliposhindwa kupambana, alikuwa akitema chini kipande kimoja cha mchanga na kusalia na vipande vinne mdomoni mwake.

Alitulia chini na kumtazama adui yake ambae alikuwa akijiandaa kumshambulia tena, na kwa kasi ya ajabu alijiinua chini na kusimama wima, kisha alijipanga kwa mpambano huku maumivu, yakianza kuutafuna mkono wake wa kushoto, ambao ulikuwa umejeruhiwa na risasi.

Adui nae alikuwa amesimama bila kutetereka, alijipanga kukabiliana na Miguu ya kuku.

Adui alikuwa ni Tembe za chai, ambae alimfuatilia hadi alipofanikiwa kuyaona makazi ya Miguu ya Kuku, kisha akuachagua usiku kumtembelea kwa aina ile ya kushitukiza.
Miamba walikutana, huku mmoja akijisifu kumfuata nyumbani adui yake na mwingine akiona dharau kufuatwa na nyumbani kwake.

Hakika ulikuwa ni mtihani usio na majibu rahisi

.
.
.
.
ENDELEA KUWA NAMI.
 
RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SIMU; 0758573660/0624155629.

HII NI SEHEMU YA SABA.

Wakati alipokuwa akisimama baada ya kuokota mchanga, masikio yake yalihisi sauti ya mkimbio wa kiumbe hai. Kiumbe ambae alikuwa anatumia ncha ya viatu vyake ili asitoe kishindo na, alipoinua uso wake, aliona kivuli cha mtu kikimfuata kwa kasi kubwa ambayo haikuitarajia na, kabla hajasimama vema, alijikuta akichezea mateke mawili ya kifua na kwenda chini bila kupenda.

Licha ya kuanguka, lakini hakufungua mdomo wake ili kutema mchanga wote, ambao aliufumbata chini ya ulimi na badala yake, aliinua ulimi kidogo na kutema mchanga mmoja tu na,mdomoni alisalia na vipande vitano vya mchanga.

Alipojaribu kuinuka, alijikuta akirudi chini huku ubavu wake wa kushoto ukipokea maumivu makali, kiasi alishindwa kuhimili na kujikuta akiguna kwa maumivu.

Kama kawaida kila aliposhindwa kupambana, alikuwa akitema chini kipande kimoja cha mchanga na kusalia na vipande vinne mdomoni mwake.

Alitulia chini na kumtazama adui yake ambae alikuwa akijiandaa kumshambulia tena, na kwa kasi ya ajabu alijiinua chini na kusimama wima, kisha alijipanga kwa mpambano huku maumivu, yakianza kuutafuna mkono wake wa kushoto, ambao ulikuwa umejeruhiwa na risasi.

Adui nae alikuwa amesimama bila kutetereka, alijipanga kukabiliana na Miguu ya kuku.

Adui alikuwa ni Tembe za chai, ambae alimfuatilia hadi alipofanikiwa kuyaona makazi ya Miguu ya Kuku, kisha akuachagua usiku kumtembelea kwa aina ile ya kushitukiza.
Miamba walikutana, huku mmoja akijisifu kumfuata nyumbani adui yake na mwingine akiona dharau kufuatwa nyumbani kwake.

Hakika ulikuwa ni mtihani usio na majibu rahisi.

*****

Miguu ya Kuku alikuwa amesalia na vipande vinne vya mchanga, mdomoni mwake huku kisu kidogo akiwa amekishika vema mkononi mwake. Hakutaka kuanza kumshambulia adui yake, badala yake alijisimamisha kivivu ili kumhadaa hasimu wake.

Hadaa yake ilizamaa matunda, kwani alifuatwa kwa mtindo wa zigizaga, huku mapigo kadhaa yakimpita mithili ya wacheza filamu za kichina.

Mapigo mengi yalipita patupu lakini pigo moja la mwisho, lilimwingia vema kwenye paji lake la uso na kumyumbisha kidogo, lakini alihimili na kusimama.

Kama kawaida yake, alitema kipande kimoja cha mchanga na, kufanya idadi ya vipande mdomoni vibaki vitatu.

Alijipanga tena na Tembe za chai nae alijipanga kwa mpambano mwingine.

Wakati huu miguu ya Kuku alianzisha yeye mapambano. Alimtisha kama anataka kumtandika teke na adui alipotishika, aliachia konde la mkono wa kulia lililoenda kutua kwenye mwamba wa pua, kabla mpigwaji hajajifikiria zaidi, ngumi nyingine ilitua kwenye kidevu(chembekidevu).

Ngumi aliopigwa Tembe za chai, ilimfanya ashindwe kuelewa mdomo wake umekutana na dhahama namna gani, badala yake alianza kuhisi ladha ya chumvi huku mate yakiwa mazito mdomoni mwake. Kabla hajajua ateme au ameze mate yake, alijikuta akikutana na dhahama ya kutandikwa teke la shingo, kiasi alishindwa kupumua vema huku akienda chini mzimamzima.

Wakati yeye akienda chini, Miguu ya Kuku yeye alikuwa anatema kipande cha mchanga, na kusalia na vipande viwili mdomoni mwake.

“Baboon!” Alisema kwa sauti huku akimsubiri adui yake ainuke, hakutaka kumpiga kwa kuvizia na mwishoni aonekane alimuonea. Alitaka wapigane wima wima, ili mshindi ahesabike kiuhalali.

Baada ya kusimama, mpambano ulianza upya, kila mmoja akijaribu kutumia ufundi wake, kumdhibiti mwenzake.

Dakika moja ilikatika bila mjuzi zaidi kupatikana. Kila mmoja alikuwa amepangua ngumi na teke nyingi, bila kuruhusu kuguswa na mpinzani wake.
Miguu ya Kuku alitema chini kipande cha tano cha mchanga na, kusaliwa na kipande kimoja mdomoni. Hakutaka kipande kile kimalizike mdomoni bila kumdhibiti adui yake.

Aliweka vema kisu chake, huku akiweka mkao aina ya FiuFui, mkao maarufu wa kutumia silaha ndogo, kwenye jamii za watu wa Lebanon. Mkao ule ulikuwa unamfanya mpambanaji kuchutama, huku akitandaza mikono na kisha kuanza kujongea, mithili ya nyani aliyeiba mahindi shambani.

Tembe za chai hakuwahi kuona mkao wa aina ile, hivyo hakujua mwenzake amedhamiria kufanya nini. Haraka alitaka kujaribu bahati yake, kwa kuushambulia mguu wa kushoto wa hasimu wake, akiwa na lengo la kumtegua na kumtupa chini.

Kitu kimoja hakuwahi kujua mchezo wa FiuFui huwa ni mchezo hatari kwa adui. Wakati alipojaribu kurusha teke, alishangaa mguu wake ukidakwa kwa ustadi mkubwa, kisha alihisi akichanwa nyuma ya paja na kitu chenye ncha kali. Alipojaribu kuruka ili ageuke kujua kilichomsibu, alishangaa akichomwa nyuma ya mgongo, huku hasimu wake akiwa mbele yake akinesanesa.
Tembe za chai alishindwa kuelewa imetumika kasi kiasi gani, kuchomwa na kisu mgongoni na aliemchoma kuwa mbele yake.

Hata!

Hofu ilianza kumuingia, hakuwahi kukutana na kiumbe mwenye kasi namna ile, hakuwahi kuona mapigo ya kutumia kasi namna ile.
Mapigo ambayo ndani ya sekunde tatu, tayari anamilikishwa majeraha mawili ya kuchanwa na kisu.
Akajaribu bahati yake kwa mara nyingine, lakini alijikuta akiloa mvua ya ngumi zisizohesabika. Hakikutumika kisu, bali ngumi ambazo ziligusa kila eneo lenye udhaifu.

Tembe za chai alienda chini huku akiwa amepiga magoti, mithili ya muumini mwovu kanisani. Alihema kwa tabu huku maumivu yakiutawala mwili wake na alipomtizama mwenzake, alishuhudia mnesoneso usio na mpangilio, ikiwa na maana, wakati wowote angekutana na pigo la kifo.

Akubali kufa? Hapana, hilo hakuona kama ni sahihi kwa wakati huo, kufa kizembe namna ile,hakika aliona mtihani.

Alipanga kuitumia nafasi ambayo aliona Miguu ya Kuku anaichezea, alipanga jambo.

Wakati akiwa kwenye mipango yake, masikio yake yalihisi sauti ya kutemwa kitu kutoka kwenye mdomo wa mpinzani wake. Akili yake ilicheza na kumbukumbu za kutema yule bwana na, kumbukumbu hazikudanganya. Alikumbuka vema kumuona jamaa kwenye jengo la mauzo, akitafuna karanga moja moja na, alipotafuna karanga ya tano, alimshuhudia akianzisha varangati lisilo na mfano, hadi yeye alipoingilia. Na sasa, anamsikia jamaa akitema kila baada ya muda na kwa idadi ilifika sita.

Hata! Nani haogopi kifo?

Kwa hali aliokuwa nayo aliamini hawezi kupambana na, kwa haraka alijua jamaa huwa anahesabu zake kila akitema kitu kutoka mdomoni, hivyo hakutaka kuingia kwenye hesabu hizo.

Haraka alisimama, kisha akajirusha na kuanguka upande mwingine, huku akimuacha Miguu ya Kuku amezubaa. Alitumia mshangao wa mwenzake kufanikisha adhima yake.

Kwa wepesi wa nyoka vichakani, aliudandia ukuta kama mzaha vile, kisha alijirusha na kuanguka nje ya uzio na kuanza kutimua mbio za Madenge na mpira.

Kitu kimoja ambacho hakujua ni kuwa, Miguu ya Kuku ni mtaalamu zaidi yake, ni mtaalamu wa kuruka kuta za kila aina na, kasi yake ya kukimbia ni zaidi ya swala. Anakimbia mita mia kwa sekunde nane tu, tena akiwa hatoi vishindo.

Tembe za chai alienda kuyavagaa asioyaweza.

****

Wakati akidhani amemkimbia Miguu ya Kuku, alishangaa akipigwa mweleka safi, huku akidakwa ili asianguke chini, kisha alizungushwa kwa mtindo wa ajabu kabisa na kubwagwa chini kama gunia la viazi vya Mbeya. Kabla hajajua kilichomzoa namna ile, alishangaa akitandikwa konde zito katikati ya kifua na kumfanya apoteze uelekeo wa kuvuta hewa safi.
Alitamani kuongea, lakini alishindwa. Alitamani kupiga kelele za kila namna, lakini sauti haikutoka katu na, badala yake alijikuta akitandikwa makofi ya uso kama mtoto mdogo, aliyedokoa maharage ya wenyewe.

Kamasi nyepesi pamoja na mate mazito, vilimtoka bila kupenda. Alipokuja kupata ufahamu, alijisikia akilia kama mtoto aliesuswa na *****.

Aibu jama!
Alijisikia aibu mbele ya mwanaume mwenzake; alimkimbia na sasa analia kama mtoto mdogo huku akiwa amepiga magoti.

Yaani kutoka kuwa mamluki wa kuogopwa, hadi kulia mbele ya mwanaume mwenzake. Hakika Tembe za chai alijuta kumfahamu Miguu ya Kuku.

“Naitwa Zuki Gadu alimaarufu Miguu ya Kuku” Alijitambulisha kisha aliendelea.

“Huwa siui bila sababu na hapa sijui tunapigana kwa sababu gani. Hata kule mjini yule boya nilimuua kwa sababu sikutaka kashikashi na polisi.” Zuki Gadu alitua.

“Hata mimi sijui kwa nini tunapigana, ila najua nilikufuata ili kufunza adabu..” Tembe za chai alijibu.

“Kwa hivyo bado unataka kunifunza adabu?”

“Umenishinda ndugu, na niache niendelee na….” Tembe za chai hakumaliza kauli yake, risasi ilifumua kichwa chake, huku Miguu ya Kuku akijirusha upande mwingine na kulala chini, asijue alieshambulia ni nani.

Hofu ikamvaa, moyo ukamdunda, mwili ukamsisimka, ngozi ikajikunyata.

Akiwa amelela chini, alishuhudia watu watatu wakimfuata kwa kasi, huku kila mmoja akiwa ameshika bastola yenye kiminya sauti.

Watu wale wote walikuwa wamevalia koti ndefu, huku nyuso zao zikiwa zimefunikwa na barakoa. Waliendana na giza la muda ule.
Miguu ya Kuku alihisi ni zamu yake kupiga magoti na kulia.

Hilo hakutaka limkute, akapanga kufa kiume na vita ni asili yake, akasimama wima, kisu mkononi, tayari kukabiliana na miamba mitatu inayotembea kizungu

Hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom