Mdunguaji wa Goma

Mdunguaji wa Goma

RIWAYA; MDUNGUAJI WA GOMA.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA TISA.

“Milioni mia sita!” Waliuliza mshangao kwa pamoja.

“Ndiyo. Bila hiyo pesa, tafuteni mtu mwingine wa kuwafanyia hiyo kazi. Kumbukeni Papaa Deo ni Kanali wa jeshi na anaulinzi kila pahali.” Alfa alisisitiza hoja yake.

“Milioni mia sita ni pesa ndefu sana, lakini kama akifanikiwa kuiba mali kwa Papaa Deo, nitamuongezea na nyingine ifike bilioni” Rich'one alisema kwa majivuno.

“Pesa ndefu sana aisee!” Omega bado walikuwa anashangaa.

“Ulishazoea majambazi wa bei rahisi eeh. Huyu ni classic killer” Alfa alizodoa.

“Lakini naomba asiembiwe wadhifa wa hawa watu tunaomtuma. Endapo akijua wadhifa wao, anaweza kuahirisha zoezi. Maana ni rahisi sana kumuua kiongozi mmoja wa kijeshi, lakini ni ngumu kuua viongozi sita ndani ya muda mfupi.” Rich alishauri.

“Upo sahihi. Lakini Miguu ya Kuku hawezi kwenda sehemu bila kujua anafuata watu wa aina gani.” Alfa alichomekea.

“Kwa hiyo unamaanisha anaweza kutuuliza kabla ya kukubali?”

“Ndiyo au hapana. Kwa sababu inategemeana na mzuka alioamka nao siku hiyo.”

“Aisee!”

“Eeh! Miguu ya Kuku ni mwanajeshi asie na namba ya ajira. Anaakili kuliko udhaniavyo.”
“Hii bado ngumu, adhima yetu inaweza isifanikiwe na wale jamaa wakaendelea kutafuana mali walizotudhulumu.” Omega alianza kuonesha wasiwasi wake.

Wakati wale wazee wakijadili kuhusu Miguu ya Kuku na kazi wanayotarajia kumpa, yeye alikuwa anajigeuza upande kitandani, huku akiwaza namna ya kuingia jengo la mauzo na kuuchukua mkoba mweusi.

Alitarajia kukutana na upinzani mwingine tena, hivyo alianza kupiga hesabu zake upya huku akingoja mapambazuko.

Mambo yakawa mambo na akilini hakuwa na wazo lolote kuhusu safari ya nje ya nchi na laiti angelijua, hakika asingeliwaza kufuata mkoba mweusi.

Kwa maana ni heri vita ya Tanzania, kuliko vita ya Congo, tena kwenye jimbo la Kivu ya kaskazini.

******

Mapambazuko yalimkuta akiwa kwenye chumba cha mazoezi. Jasho limeujaa mwili, huku kifua kikipiga mithili ya ngoma za tembe. Mdomo wake ulifumba na kufumbua kila alipohitaji kufanya hivyo, kisha alivuta pumzi nyingi na kuendelea na zoezi lake la kufumba na kufumbua mdomo.

Mkono wake wa kushoto uliokuwa na jeraha la risasi, haukumpa taabu kwenye mazoezi yake hayo, kwa kuwa alishajichoma sindano ya kuzuia maumivu huku akiwa amefunga kidonda kwa kitambaa safi na laini.

Alitumia zaidi ya dakika tisini kufanya mazoezi makali, huku akiwa hajachukua lau dakika maja ya mapumziko.

Macho yake yalitizama saa iliyokuwa ukutani, kisha alisimama na kuvua vitambaa alivyokuwa amefunga vidoleni mwake na, kisha aliingia maliwatoni kujiswafi.

Dakika saba zilitosha kumpa usafi aliotaka, kisha alitoka maliwatoni na kuelekea jikoni. Huko alichemsha maji na kuweka kijiko kimoja cha sukari na unga wa kitunguu saumu, kisha aliyanywa yale maji yakiwa na moto wa kutosha. Alipohakikisha maji ya moto yametosha kiasi chake, alichukua mayai matano ya kuku wa kienyeji na, kuyapusulia kwenye kikombe kisha akayanywa bila kutia chumvi.

Alibeua baada ya kunya mayai mabichi. Alitoka jikoni na kwenda sebuleni, huko alikaa na kuegemeza kichwa chake kwenye sofa huku mikono yake ikifanya kazi ya kuyavuta masikio yake,kwenda chini.
Alikuwa anaweka sawa misuli ya kichwa na masikio, ili asipige miayo au kupata kichechefu na kuvurugwa tumbo, baada ya kunywa mchanganyiko wa mayai na maji ya moto ahsubuhi ile.

Alipohisi masikio yake yameacha kuvuta, alisimama na kuliendea jokofu kisha alivuta mlango na kutoa chupa ya maji ya baridi sana. Ilikuwa kiasi cha Lita moja na nusu. Akanywa maji yote yaliokuwa kwenye chupa, kisha akabeua tena huku miguu yake ikianza kuchanganya, kuelekea jikoni.

Alipofika jikoni, aliwasha jiko na kubandika supu ya utumbo. Ilipochemka aliipua na kuanza kushugulika na chapati za maji, idadi yake ikiwa ni chapati kumi.

Alipohakikisha chapati zimeiva, alichukua na sufuria la supu na kuelekea sebuleni. Bila kuweka kwenye bakuli, yeye alianza kushugulikia ikiwa kwenye sufuria huku akikamulia limao na pilipili kichaa tano.

Dakika kumi na tano zilitosha kumaliza supu na chapati za maji, kisha alisimama na kwenda kuchukua maji kwenye jagi, kisha alibugia yote bila kubakiza.

Alipomaliza mlo wake huo wa ahsubuhi, alirejesha vyombo na kivitupia kwenye beseni la vyombo vichafu, huku akishika tumbo lake kwa shine ya ahsubuhi hiyo.

Dakika moja baadae, alikuwa chumbani kwake akichagua mavazi ya kuvaa siku hiyo ambapo; alichagua suti nyeusi na viatu vyeusi, ambavyo alijua vitamrahisishia kwenye timbwili lolote huko aendako. Hakusahau kujipachika silaha kadhaa, huku bastola akiiweka kwenye soksi za viatu vyake. Alipomaliza, alichukua saa yake ya gharama na kutoka chumbani kwake, bila kubeba kitu chochote mkononi mwake.

Alipofika nje ya nyumba yake, alitola simu yake mfukoni na kuita usafiri wa Taxi, kisha alisubiri getini kwake huku akipiga muluzi wa Dunia mapito, wimbo wake Matonya.

Mara nyingi hakuwa akipenda kutumia usafiri wake, licha ya kuwa na utitiri wa magari mengi na mazuri, ambayo huyatumia kwa nadra sana.

Alipenda kusafiri kwa kutumia usafiri wa kawaida, kwa kuwa hakutaka kuacha ushahidi sehemu yoyote, endapo angeacha varangati lenye kuwasogeza maofisa wa jeshi la polisi.

Dakika kadhaa za kusubiri, zilimkutanisha na taxi aliyokuwa ameihitaji kupitia mtandao wa Uber. Alipanda na kuomba kupelekwa Ilala Boma.

Mwendo ulianza huku yeye akijilaza kwenye kiti akiwa na maana, hahitaji soga ya aina yoyote na dereva. Usingizi mwepesi ukamchukua, huku sikio likibaki wazi kama sungura.

****

Baada ya foleni za hapa na pale, hatimae dereva alimuamsha abiria wake, ikiwa mshale wa saa ulisoma saa tano na nusu ahsubuhi.

“Mmh, wapi hapa?” Miguu ya Kuku aliuliza huku akifumbua macho na kutizama nje kupitia kioo cha gari.

“Hapa ni Boma boss, tupo kando ya ofisi za mkuu wa mkoa.” Dereva alijibu.

Bila kuuliza zaidi, aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti mbili za elfu kumi kumi, kisha alishuka bila kusubiri kuambiwa lolote na dereva.

Alishika njia iliyokuwa upande wake wa kushoto na, kuambaa nayo huku akipishana na makundi ya watu ambao walikuwa wakichasakua nguo za wamachinga. Alitembea bila tahadhari yoyote, kwa kuwa hakutaka kuingia kwenye jicho la mdadisi yeyote ambae angelikuwa mitaa ile.
Alitembea bila kujali macho ya warembo ambao walimtizama na mvuto wake, ambao ulichangiwa na suti maridadi iliyomkaa vema mwilini mwake.
Hakujali pia macho ya baadhi ya watu, ambao walimuona ni kama amekosea kuivaa suti ile na kukatiza nayo mtaani kwa miguu, ikiwa alifaa kukaa kwenye gari la gharama na kuingia nalo mjini.

Yote hakujali, akili ilikuwa inajaribu kulikumbuka jengo la mauzo kama ambavyo, aliliona siku moja nyuma. Alipanga na kupangua mikakati yake ya namna ya kuingia na kutoka ndani ya jengo lile. Kikubwa akili yake ilikuwa inajaribu kukubaliana na hali yoyote ambayo angelikutana nayo, huku hesabu zake zikiishia kwenye makao makuu ya jeshi la polisi, ambapo hakutaka wamkute eneo lile, endapo kungelizuka jambo lolote.

Joto lilimpa adha mwilini mwake, lakini halikumfanya asiendelee na safari yake, huku kila mara akiangaza kiujanja janja ili kuona kama kuna mtu alikuwa akimfuatilia.

Alipoona hakuna aliyehangaika nae, alichepuka na kuingia kwenye viwanja vya jengo la mauzo. Tofauti na alivyodhania kukutana na ulinzi mkali, baada ya wao kuwa wameanzisha varangati siku ya nyuma yake, badala yake alikuta kila kitu kipo kama alivyoingia jana yake. Ulinzi ilikuwa uleule, kwa maana; walinzi wawili na gobole lao, huku ulinzi mkubwa wakiwa wameuweka kwenye pango la kuegeshea magali.

Alipita kama watu wengine walivyokuwa wakipita, kisha akaifuata kambalau na kupanda kuelekea ghorofa ya sita.
Nusu dakika alikuwa anakutana na ofisi za ghorofa ya sita, zikiendeleza kazi kama vile hakukuwa na kitu kilichokuwa kimetokea kwenye ofisi hizo.

Hakuhangaika kuingia kwenye ofisi hizo, badala yake aliifuata njia ya ngazi na kushuka chini ghorofa ya tano.
Alikutana na ukimya ambao aliutarajia kwenye ofisi zilizokuwa pale, kwa sababu yoyote ambayo kunatarajiwa kashikashi, lazima kuwe na maandalizi ya namna ile.

Alipiga moyo konde na kuufuata mlango ambao uliandika neno la kiingereza (Push). Aliusukuma mlango na kuingia ndani. Alipokelewa na viti tupu vya mapokezi, kumaanisha ofisi ilikuwa wazi na hakukuwa na wahudumu.
Alitulia akiwa amesimama huku macho yake yakizurura kwenye ofisi ile kwa kasi kubwa na, harakaharaka aligundua ilikuwa ni ofisi ya uuzaji wa madini na Vito, huku kukiwa na kibanda kidogo ndani yake, ambacho kilionekana kutumiwa kuuza simu za gharama kubwa. Pengine waliweka duka la simu ili wanunuaji na wauzaji wa madini, waweze kuzinunua kwa kuwa ziliwafaa zaidi wao, maana kajamba nani, hohehahe wa Buza, katu asingeliweza kununua.

Macho yake yaliendelea kutalii na kunakili kichwani kila kilichoonekana na hatimae, macho yake yaliangukia kwenye mlango mwingine ambao uliandika neno la kiswahili ‘Sukuma’.

Miguu ya Kuku alitabasamu kivivu, huku akishindwa kuelewa wahusika wa ofisi ile waliwaza nini kuweka kachumbari ya maelekezo, kwa lugha mbili, kiswahili ndani na kingereza nje.

Hakuwa na namna, alipiga hatua na kuufuata mlango huo, ambapo alifuata maelekezo kama yalivyokuwa, aliusukuma.

Alikaribishwa na ofisi safi na nadhifu sana, huku kiyoyozi kikiwa kimebeba umiliki wa kugawa hewa safi.

Macho yake yalikuwa yameganda nyuma ya meza iliyokuwa mbele yake. Yaliganda kwa watu watatu ambao walikuwa wamekaa nyuma ya meza ile, wakiwa kimya wakimtizama.

Kilichofanya agande ni, kuona mkoba mweusi ukiwa juu ya meza, huku aliyempa kazi ya kuufuata akiwa amekaa katikati ya watu wengine wawili.

Kwa harakaharaka alishindwa kuelewa; ni kwa nini mtu aliyempa kazi na kumlia pesa nyingi, awe pale tena na mkoba aliouhitaji ukiwa mezani bila kuonekana ukimilikiwa na yeyote miongoni mwa wale watu watatu.

Je, mtu huyo katekwa na wale watu wawili waliomuweka pembeni, ama kuna kitu gani kilikuwa kikiendelea.

Haraka alitaka kufahamu kinachoendelea kupitia lugha ya hisia. Macho yake aliyapeleka usoni kwa mtu aliyempa ile kazi, akiwa na nia ya kuyasoma mawazo yake, iwe ya hofu ama shari.

Alipoona hakuna hisia za hofu kwa mtu yule, haraka alipeleka macho yake kwa mtu aliyekuwa kushoto kwa mwajiri wake, akiwa na lengo la kuona hisia za ubabe na utabe. Hakuishia hapo, alimtizama pia mtu wa mwisho ambae hakuwa amemzingatia tangu awali; napo hakuona hisia alizotarajia wala hakuona lugha ya picha kutoka kwao wote watatu.

Kiufupi, alikutana na watu ambao walimtizama kawaida, ikiwa na maana hakuna baya miongoni mwao.

Ilimshangaza na alibaki wakiwa amesimama na, asijue cha kufanya.

Mkoba mbele yake na mwajiri wake mbele yake.
Je, achukue mkoba ambao ndo ulimpeleka pale, au amchomoe mwajiri wake na kuuacha mkoba? Kipi ni kipi na je, hakuelewa alipoambiwa kuufuata mkoba? Ilikuwa ni mkoba kama mkoba, au ni mkoba ikimaanishwa mtu.

Mawazo lukuki yalipita huku ofisi ikiwa kimya, kama vile hakukuwa na watu ndani yake

Miguu ya Kuku aliamua kufuata utaratibu kama alivyolipwa. Mkono wake ukaufuata mkoba na kuunyanyua, kisha aligeuka na kuanza kutoka ndani ya ofisi ile.

Lakini kabla hajaufikia mlango, sauti ya chuma ikasikika na hakuwa mgeni wa sauti kama zile, alijua ni sauti ya bastola imeondolewa usalama.

Moyo ukamdunda kimdundiko.

‘Tuku..tuku…tuku' Ukazidi kudunda.
.
.
.
.
.ENDELEA KUWA NAMI.
 
daah mlo wa miguu ya kuku umeniacha kinywa wazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom