Mdau: Baada ya baba kupotea, rafiki yake ametuma watu wenye silaha kuvamia nyumba yetu akitaka tuhame

"No research no right to speak".
By Mao, a former Chairman and the founder of CPC, China.

Not only that, but also, "He who alleges must prove".

Kwa muktadha huo, mleta hoja hajathibitisha madai yake, kwa sababu madai au hoja yake inaibua na inaacha maswali mengi zaidi bila majibu.
Kwa mantiki hiyo, kwa sasa ni vigumu sana kumtuhumu kwa utapeli huyo mtu wanayemtaja kuwa ni Kilumile. Mleta hoja kwanza anapaswa kuthibitisha madai yake kwanza kabla ya kumgeukia huyo Kilumile.
Kwa mazingira hayo, mahakama ndio itakayotoa majibu
 
You are completely wrong and out of point. Je, hiyo Mahakama majibu itayatoa wapi ikiwa wewe mwenyewe Mlalamikaji au mdai hujawasilisha ufafanuzi wa kina au maelezo ya kina kuhusu madai/malalamiko yako???? Ikiwa wewe mwenyewe mdai au mlalamikaji huyajui madai/malalamiko yako, Je, Mahakama itayajuaje???

Kumbuka, Kazi ya Mahakama siyo Kupiga Ramli.
 
Niliwahi mwambia mke wangu haya mambo ya mikopo bora nkalime kwenu tarime ngiba nije adi wangu mmoja sio kuanza kufunga nyumba jamaa wakija kudai kha
mtaani kuna watu wa kighoma wanakopesha vyakula vyombo madaftari wanakusanya buku kwa siku ama buku mbili sasa wanapokuja wanagawana posn ingilia huku we elekea kule sasa wamama wanavyokimbia kujificha vichochoron utacheka sasa hii ya crdb ningekufa kabla ya wakt kha
 
Kwamba wamama wakishawasikia waha tu Wanatoka nduki
 
Andiko la Mdau wa kutoka Goba kuhusu watu wanaotaka kupora nyumba yao baada ya baba yao kupotea:

Usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 6, 2023 kuna watu wamevamia katika nyumba yetu iliyopo Goba, Mtaa wa Kiburuni, Dar es Salaam na kuanza kuvunja sehemu ya nyumba, ikiwemo madirisha na milango, baada ya hapo wakamjeruhi ndugu yetu mmoja na kusema kuwa kama hatutahama kwenye nyumba hiyo watarejea kesho yake ambayo ni usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 7, 2023.

Wahalifu hao walifika wakiwa makundi, wanne wakaingia ndani na wengine ambao sijui idadi yao walibaki nje, majirani wanasema kuwa walikuwa na silaha za moto ndio maana hata wao walisita kutoa msaada kwa haraka.

Walikuwa wanamtaka kiongozi wa familia ambaye alikuwa katika chumba kingine, wakati akifanya uharibifu huo wakamchukua ndugu yetu mmoja na kuanza kumpiga huku wakimtaka aseme alipo ndugu yetu ambaye ni mtoto wa kwanza wa mzee.

Alikataa kutii kile walichotaka na wakaendelea kumpiga hadi alipopata nafasi ya kuwatoroka na kwenda kuripoti Polisi.

Polisi walikuja baadaye wakakuta wahalifu wale ambao tunaamini wametumwa na aliyekuwa rafiki wa baba yetu kwa kuwa ndiye ambaye tuna mgogoro naye wa nyumba tunayoishi.

Kwa nini rafiki wa baba anahusishwa?
Anahusishwa kwa kuwa mshukiwa anayefahamka kwa jina la Thomas Daniel Kilumile, mzaliwa wa Iringa ambaye kwa sasa anaishi Mwanza, alikuwa ni kama ndugu kwetu wakati baba alipokuwa nasi.

Wawili hao walikuwa marafiki na hata kufikia hatua ya huyo rafiki yake kuwa anakuja kwenye nyumba yetu analala na kwa pamoja walikuwa wakimiliki kampuni.

Walikuwa wafanyabiashara walioshirikiana muda mrefu, ghafla Mwaka 2018 baba akiwa ametoka na gari kwenda kwenye mizunguko yake ya kawaida hakurudi tena mpaka leo.

Hatujui kama ni mzima au ameshakufa na hata gari lake pia halikuwahi kuonekana.

Rafiki wa baba aanza kudai nyumba
Baada ya baba kupotea, ndugu tukaanza kufuatilia madeni na biashara zake alizokuwa anafanya, hapo ndipo sokomoko likaanza, huyo Thimos akaja kudai kuwa nyumba tunayoishi ni mali yake na tunatakiwa kuhama.

Mgogoro ukaanzia hapo, tukamtaka aende Mahakamani ili haki ipatikane, hakufanya hivyo, aliishia kwenda Polisi na suala letu lilifika hadi Serikali za mtaa lakini hakukuwa na utatuzi uliopatikana.

Nyaraka za nyumba zinaonesha zina jina la baba yetu aliyepoteza lakini Kilumile alikuja na nyaraka anazodai ni za kiwanja na kuwa kile ni kiwanja chake.

Kinachoshangaza ni kuwa rafiki huyo wa baba hakuwahi kusema chochote kuhusu umiliki wake wa nyumba hiyo, na kwa kinachoendelea tunapata mashaka kupotea kwa baba na hiki kinachoendelea.

Vitisho
Mzee Kilumile alianza kutupa vitisho yeye na mwanaye ambaye ni Daniel Kilumile wakitutaka tuhame, shauri lilifika Kituo cha Polisi Goba, kwa kuwa alikosa ushahidi akawa ni kama ameshindwa kuendelea.

Nyumba hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 na ikakamilika Mwaka 2014 ambapo ndipo familia ikahamia.

Mama yetu hayupo hapa anaishi Mwanza, aliwahi kusema rafiki wa baba anataka kutupora nyumba yetu kinyume cha sheria.

Kwa kuwa rafiki huyo wa baba mtoto wake ni mwanajeshi, amekuwa akidai kuwa lazima atatuhamisha na kwa mazingira yanayoonekana sasa inaonekana kuna vitu ambavyo anaweza kuhusika kwa kupotea kwa baba.

Tulitegemea pia baada ya baba kupotea angekuja kutuambia kuhusu biashara aliyokuwa akishirikiana na baba, tulipomuuliza hakuwa na majibu.
Kama ni kweli ulichokiandika ni sahihi,

Basi , Muuaji au mhusika WA kupotea Kwa baba yenu ni huyo Kilumile.Nashangaa kwanini yupo nje Hadi Sasa?

Polis siyo Kila kitu lazima ichukue Rushwa hii kesi mbona ipo wazi?

Kwa mwendo huu polis ndo chanzo Cha wananchi KUCHUKUA sheria MKONONI,. POLISI IMKAMATE HARAKA SANA HUYO MZEE NA MWANAYE HUYO MWANAJESHI MWENYE CHEO KIKUBWA JESHINI WAONESHE ALIPO MZEE ISHENGOMA.

Watoto WA Mzee ISHENGOMA wapewe ulinzi WA polis na wapewe silaha za moto za kujilinda.

UKIUA KWA UPANGA NAWE IPO SIKU UTAKUFA KIFO KIBAYA.
 
Watu huwa mmasumbuka buree wakati mnaweza tatua shida zenu. Nendeni kwa waganga konki hapo malawi mtamjua mbaya wenu ni yupi na mzee yupo wapi. Mnaweza chukua hatua kali za kumlarua mbaya wenu either yeye binafsi au na wanae/mkewe maana mchuma janga hula na wakwao. Amkeni nendeni malawi au nendeni kongo hapo biashara mtamaliza jua la saa nne, mkirudi watu hawapo hai tena. Zaidi ya hapo mtageuka makaini mchini.
🤣🤣🤣
malawi mbali
babati kuna mzee wa kipare ni hatari sijui ka yupo hai yule mzee. nlmsindikza bosi wangu oya niliyoyaona nikasema kurareki hii teknolojia kabisa
 
Mikopo hiyo. Hakuna watu wanakuja na Silaha. Mchana mda wote huo wawe wahalifu.

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD.....................................1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT

Baba yako hayupo hapo? Inawezekana baada ya Baba yako kupotea, jamaa akalipa deni lote, na labda hiyo Nyumba ndo ilikuwa bond, ninaamini ana haki of some sort
duh umetisha kamanda mkuu.
kwa hiyo hapo huyo mzee buberwa kaona achimbe aitelekeze familia akatese na dogodogo aiachie familia msala.
 
Andiko la Mdau wa kutoka Goba kuhusu watu wanaotaka kupora nyumba yao baada ya baba yao kupotea:

Usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 6, 2023 kuna watu wamevamia katika nyumba yetu iliyopo Goba, Mtaa wa Kiburuni, Dar es Salaam na kuanza kuvunja sehemu ya nyumba, ikiwemo madirisha na milango, baada ya hapo wakamjeruhi ndugu yetu mmoja na kusema kuwa kama hatutahama kwenye nyumba hiyo watarejea kesho yake ambayo ni usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 7, 2023.

Wahalifu hao walifika wakiwa makundi, wanne wakaingia ndani na wengine ambao sijui idadi yao walibaki nje, majirani wanasema kuwa walikuwa na silaha za moto ndio maana hata wao walisita kutoa msaada kwa haraka.

Walikuwa wanamtaka kiongozi wa familia ambaye alikuwa katika chumba kingine, wakati akifanya uharibifu huo wakamchukua ndugu yetu mmoja na kuanza kumpiga huku wakimtaka aseme alipo ndugu yetu ambaye ni mtoto wa kwanza wa mzee.

Alikataa kutii kile walichotaka na wakaendelea kumpiga hadi alipopata nafasi ya kuwatoroka na kwenda kuripoti Polisi.

Polisi walikuja baadaye wakakuta wahalifu wale ambao tunaamini wametumwa na aliyekuwa rafiki wa baba yetu kwa kuwa ndiye ambaye tuna mgogoro naye wa nyumba tunayoishi.

Kwa nini rafiki wa baba anahusishwa?
Anahusishwa kwa kuwa mshukiwa anayefahamka kwa jina la Thomas Daniel Kilumile, mzaliwa wa Iringa ambaye kwa sasa anaishi Mwanza, alikuwa ni kama ndugu kwetu wakati baba alipokuwa nasi.

Wawili hao walikuwa marafiki na hata kufikia hatua ya huyo rafiki yake kuwa anakuja kwenye nyumba yetu analala na kwa pamoja walikuwa wakimiliki kampuni.

Walikuwa wafanyabiashara walioshirikiana muda mrefu, ghafla Mwaka 2018 baba akiwa ametoka na gari kwenda kwenye mizunguko yake ya kawaida hakurudi tena mpaka leo.

Hatujui kama ni mzima au ameshakufa na hata gari lake pia halikuwahi kuonekana.

Rafiki wa baba aanza kudai nyumba
Baada ya baba kupotea, ndugu tukaanza kufuatilia madeni na biashara zake alizokuwa anafanya, hapo ndipo sokomoko likaanza, huyo Thimos akaja kudai kuwa nyumba tunayoishi ni mali yake na tunatakiwa kuhama.

Mgogoro ukaanzia hapo, tukamtaka aende Mahakamani ili haki ipatikane, hakufanya hivyo, aliishia kwenda Polisi na suala letu lilifika hadi Serikali za mtaa lakini hakukuwa na utatuzi uliopatikana.

Nyaraka za nyumba zinaonesha zina jina la baba yetu aliyepoteza lakini Kilumile alikuja na nyaraka anazodai ni za kiwanja na kuwa kile ni kiwanja chake.

Kinachoshangaza ni kuwa rafiki huyo wa baba hakuwahi kusema chochote kuhusu umiliki wake wa nyumba hiyo, na kwa kinachoendelea tunapata mashaka kupotea kwa baba na hiki kinachoendelea.

Vitisho
Mzee Kilumile alianza kutupa vitisho yeye na mwanaye ambaye ni Daniel Kilumile wakitutaka tuhame, shauri lilifika Kituo cha Polisi Goba, kwa kuwa alikosa ushahidi akawa ni kama ameshindwa kuendelea.

Nyumba hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 na ikakamilika Mwaka 2014 ambapo ndipo familia ikahamia.

Mama yetu hayupo hapa anaishi Mwanza, aliwahi kusema rafiki wa baba anataka kutupora nyumba yetu kinyume cha sheria.

Kwa kuwa rafiki huyo wa baba mtoto wake ni mwanajeshi, amekuwa akidai kuwa lazima atatuhamisha na kwa mazingira yanayoonekana sasa inaonekana kuna vitu ambavyo anaweza kuhusika kwa kupotea kwa baba.

Tulitegemea pia baada ya baba kupotea angekuja kutuambia kuhusu biashara aliyokuwa akishirikiana na baba, tulipomuuliza hakuwa na majibu.
Kamrogeni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom