Kero: EATV, Star tv na Star times badilikeni mnatukera watazamaji

Dec 13, 2019
79
150
Mimi ni mpenzi wa vipindi vya mijadala ya kisiasa na michezo, kwenye mijadara ya siasa nawaangalia sana ITV hata taarifa ya habari sijaona yenye mvuto kama ITV, na kwenye michezo nimeapa kumfata kokote atakapoenda maulidi kitenge kwahiyo nawaangalia wasafi na kuwasikiliza.

Naomba Nikiri tu kwamba local channels zimepoteza mvuto kwa watazamaji, hususani hii ya EATV, vipindi vyenu havina mvuto. hata hizi Swahili movies za weekend mnaweka za hovyohovyo. sitawaongelea sana Star tv pengine kwa sababu ubora wao wa vipindi ni duni kwakua wana content za kimwanza mwanza sana (japokua Aloyce Nyanda ananifanya nichungulie kwa muda, anatendea haki kipindi cha mjadara 2020).

Uchaguzi wa 2015 ndipo nilimjua rasmi kijana Samson Charles, alikua anaandaa mijadara ya moto pale EATV, alikuwa taswira ya vijana wengi wanaotamani kuwa wachambuzi wa siasa kwenye tv, sijajua imekuaje na amepatwa na nini miaka hii ila amepotea mazima.

Ilikuwa ni kipindi pekee napendelea kuangalia. Nje ya hapo sijaona kipindi kingine chochote kizuri mpaka leo.

Kwenye vipindi vya michezo ndo zero kabisa sijajua tatizo nini, huyu salama jabir hafit kwenye utangazi wa sports, anaongelea sana timu zake. Kuna huyu
Bili Sepenga hivi nini majukumu yake pale EATV?

Kule Star tv kuna kipindi cha Medani za Siasa sijui mtangazaji nani ila abadilike namna ya utangazaji wake, hauvutii hata kidogo. Sijui anamuiga nani ila anapuyanga sana.

Kwa upande wa Star times, jitahidi muongeze ubunifu kwa kuongeza channels za maana. Halafu wale jamaa wa matangazo pale Star Swahili hamuwalipi mshahara? Sijawaona wakibadili mavazi, shida nini?
 

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
2,835
2,000
Nina mashaka kama kweli huwa unaangalia TV na huwa unaangalia bar gani maana sidhani kama uliwahi kununua hata tv hahahhhhh
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom