ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
tunashukuru kwa taarifa mkuu ila CUF ni CCM-B kwa hiyo ni wa kuwa nao makini sana
Angalia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/91376-chadema-walikuwa-ccm-b-kabla-ya-cuf.html
tunashukuru kwa taarifa mkuu ila CUF ni CCM-B kwa hiyo ni wa kuwa nao makini sana
Duh, mkuu wangu lugha inakupiga chenga au ndio makusudi kwa sababu nimewazungumza CUF...Chadema wao siku zote wanalia hawana Udini nakama kweli hawana basi ni jukumu lao wenyewe kutuonyesha hawana Udini kwa sababu najua fika CUF ni chama cha aina gani. CUF ni wabaguzi toka maswala ya kimuungano kuzungumzia zaidi ya Zanzibar na Waislaam kiasi kwamba hata Ufisadi haikuwa kero kwenu.Labda utusaidie ni ipi RANGI Halisi ya Chadema?...maana nawe umechukua madai yaliyokuwa yanatumiwa na CCM kuwapaka CUF...ila nyinyi Chadema mkipakwa na rangi waliopakwa CUF "mnaruka"
Wewe ulitaka CUF mwaka huu ZNZ wafanye nini? watu wamefanya kura ya maoni, wewe ulitaka watu wauwane...?
.
Binafsi, siwapendi CUF na wala siwaamini kama kweli ni chama kinachowakilisha wananchi, ni chama kinachotumia kero za wananchi hasa waislaam ili kujiweka katika nafasi nzuri ya Upinzani. Na ushahidi wa malalamiko yangu umeonekana mwaka huu wakati Seif Sharrif Hamad alipokubali kuchukua makamu wa rais wa Zanzibar, cheo ambacho hakiwezi kuboresha sera za CUF kwa aina yeyote ile. Wizara walizopewa zote hazina maana hata kidogo na kwa miaka mitano mingine Wazanzibar watatawaliwa na serikali isiyokuwa na Upinzani - viongozi wake walichounda ni nasaba ya Usultan.
Chadema wanachotakiwa kufanya ni kukijenga chama pale kinapopwaya na kwa maelezo haya nadhani wanafahamu fika Ujinga ulokwisha jengwa na wananchi kiasi kwamba kura nyingi walizopoteza zimetokana na tuhuma hizo..Ni muhimu waweke mkazo kuwavuta wananchi (wapigakura) na sio ushirika wa vyama.
- Ni mtazamo wangu
Mkuu wangu labda hukunielewa...Mara nyingi hutazama mbele zaidi ya hivi vinavyoelea. Kama unakumbuka nilisema CUF sii chama cha Visiwani tu kipo bara na kina sehemu ambazo wananchi wengi wamekipigia kura. Chadema kkama chama kinachotazama ushindi mwaka 2015 ni lazima kitumie akili zaidi kujihusisha na wananchi haswa wapenzi wa CUF kwa kuwaonyesha mapenzi yasiyokuwa na ubaguzi kwa sababu tu CUF Zanzibar imekubaliana na CCM..Mzee Mkandara, (Sorry kukuita mzee ni kwa sababu ya busara yako nyingi:teeth
Kilichonifurahisha katika post yako hii ni kuona sasa umefungua macho na kuona kitu kilichokuwa kinatuletea utofauti siku kidogo zilizopita. Nacho ni muungano wa vyama hivi viwili. Nakumbuka ulikuwa msitari wa mbele kuhakikisha vinaungana kwa namna yoyote ile, mbali na kilio chetu kwamba si vema waungane. Nakumbuka hata ule mfano wako kwamba CUF ni kama mke wa ndoa wa CCM.
Lakini nimefurahi ku note kuwa sasa na wewe umeliona hilo la ndoa batili ambayo Chadema wanataka kujifunga nayo na CUF. Sioni sababu tena hata kwa nini kuwe na mdahalo. Wakati wa mdahalo nadhani umekwisha na Chadema need to work for wananchi na sio midahalo isiyo na tija hii ya kutupotezea muda.
Mkuu labda nisome tena.. CUF watafanya nini tofauti na CCM ikiwa sera zinazotumika ni za CCM. Kuna tija gani zaidi ambayo wewe unaiona toka wizara ambayo haizalishi isipokuwa mzigo kwa serikali na wananchi hivyo CCM wamekupeni mzigo huo kuubeba.Mkandara,
Hata kama huwapendi CUF lakini jaribu kuwa objective, angalau kidogo. Hivi wizara ya afya haina maana?
Sure!!!Ndani ya CUF kuna wapenzi wa madaraka na kuna watu hawawezi kukaa bila ya madaraka .Watu wote tegemeo la mageuzi ndani ya CUF wao ni madaraka kwanza ndiyo mfano Hamad Rashid naona hawezi kuishi Bungeni bila ya madaraka au anatimiza ahadi zao na makubaliano ya CCM ndiyo maana vurugu zote hizi .Maalimu kesha pata Ulaji kesha tulia na CUF kwisha kazi maana anatekeleza sera za CCM hawezi kupinga lolote na huku bara wanataka Chadema kuwa kama CUF hapana watuache wao waendelee na kusaka madaraka na kuingia makubaliano na CCM.Tutasikia hiyo weekend wao wana agenda gani .
Nimekupa heshima kubwa kwa bandiko hiliMkuu labda nisome tena.. CUF watafanya nini tofauti na CCM ikiwa sera zinazotumika ni za CCM. Kuna tija gani zaidi ambayo wewe unaiona toka wizara ambayo haizalishi isipokuwa mzigo kwa serikali na wananchi hivyo CCM wamekupeni mzigo huo kuubeba.
Elimu na Afya ni muhimu sana lakini kama CCM leo wakiwapa Chadema wizara hizo chini ya utawala wa CCM itakuwa vichekesho vitupu..
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.
Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.
Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.
Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.
CUF wanataka wawemo kwenye kambi ya upinzani. CADEMA wamebana. Sasa CUF wnakuja na vigezo vya kwanini wao nao wasiwemo kwenye kambi hiyo na CHADEMA wanakuja vigezo kwanini wawe wao peke yao. It will be very Intresting.
Hapa upinzani uko hatarini,haileti maana yoyote kuwa na such debate!
Duh, mkuu wangu lugha inakupiga chenga au ndio makusudi kwa sababu nimewazungumza CUF...Chadema wao siku zote wanalia hawana Udini nakama kweli hawana basi ni jukumu lao wenyewe kutuonyesha hawana Udini kwa sababu najua fika CUF ni chama cha aina gani. CUF ni wabaguzi toka maswala ya kimuungano kuzungumzia zaidi ya Zanzibar na Waislaam kiasi kwamba hata Ufisadi haikuwa kero kwenu.
Napwapongeza tu kwa sababu hamjifichi nyuma ya pazia lolote mkitangaza Udini na Uzanzibar lakini kwa kazi yenu wepesi sana kupachika wengine pia udhaifu wa chama chenu. Nawajua fika mkuu wangu kazi yenu kubwa ni kutafuta kuitumia dini na Uzanzibar ili mpate nafasi ndani ya uongozi kwani kwa unafiki huo hamkuanza leo..
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.
Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.
Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.
Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.
Lazima tujiulize kwa nini chadema wameunda kambi bila kuwashirikisha vyama vingine hii sio sawa wako CUF,TLP,UDP na NSSR
Je hii ni ubinafsi wa Mbowe na wenzake?