Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Ahsante kwa taarifa, lakini mdaharo ungefaa awepo mwakilishi kutoka chama tawala dhidi ya wapinzani. Vinginevyo kama Hamadi awajibie hoja zao
Hamad si atakuwepo au unataka CCM wawe wawili.
 
Quinine
ningepata agenda labda nisingekuwa frustrated...but for this moment I'm confused sure I don't know the rationale behind this move please guide me..
 
cdm tupeni majibu ya nn kinaendelea kuhusu uchakachuaji wa kura za urais? na sio midaharo na vibonde kama HR.
 
Pretty weird! Sidhani kama Mbowe anawezi kuwa mpuuzi namna hiyo. Hatuhitaji mdahalo sasa ila labda wa mabadiliko ya katiba na Tume ya Uchaguzi etc
 
Kuna tetezi ya kuwa mbali na kuwepo mawaziri vivuli watakaoteuliwa na chama kinachounda kammbi rasmi ya upinzani, yaani chadema, kutakuwepo pia mawazili maruhani, watakaoteuliwa kutoka vyama vinginevyo vya upinzani vyenye wabunge. Tofauti na mawaziri vivuli, majina ya mawaziri hao yatabakia kuwa siri lakini yatakuwa yanajulikana kwa uongozi wote wa chama tawala na vyombo vyake. Kutokana na hayo, kauli za mawaziri hao zitapewa umuimu mkubwa na vyombo hivyo kuliko zile za mawaziri vivuli.
mkubwa hii itakuwa kiboko, na inawezekana sana kwa mfumo wa sasa uliopo, lakini hiyo itakuwa ndiyo kujimaliza kwa ccm. watajifunga goli jingine hapo
 
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.


- Chadema wangejiepusha na midahalo ya namna hii at this political time and moment, I mean umemsusia Rais wa Jamhuri kwamba humtambui, chama cha Rais CCM kimekataa mdahalo wowote na wewe, lakini leo chama kinachoshirkiana kutawala na CCM kinataka mdahalo na wewe Chadema na unakubali!

- Huko Chadema vipi jamani au ndio mgema akisifiwa basi tembo atalikoroga, maana sasa mnalikoroga itakapokuja time ya kulinywa mtatafutana sana!, sasa kwa huu mdahalo ni kwamba mnakubali kwamba CUF tu ndio size yenu kama alivyosema Mh. Kinana wakati flani,

- To my loongtime friend Mh. Freeman Mbowe, this is a waste of a political status gained through this elections, stop it now!
The time is not right kuanza midahalo na wapambe badala ya kusubiri kwanza for the big elephant maana the history ni kwamba huwa ana tabia ya kuji-tripple mwenyewe with time, kinachotakiwa hapa ni subira brother!

William.
 
Hizi ni zama a ukweli na uwazi. Wapinzani wakweli wataonekana na wapinzani feki wanaobadilikabadilika kama vinyonga pia watajulikana . Chadema haina cha kuifundisha cuf.
 
kaka hawa wamesha vuta chao kubomoa upinzani huoni walivyojikomba kwa jk kabla na baada ya kuapishwa?
hakuna kitu hawa, CHADEMA TU NDIYO UPINZANI MREMA WA TLP KAPEWA NA JK 300M WEWE UNAJUA HIYO? NA SASA ANA VX V8 YA 120M UNAJUA? NINAYO MENGI SIONGEI.
 
Dhumuni la huo mdahalo ni nini? It could have make sense if ingekuwa ni MBOWE AU RASHID OR BOTH VS CCM na sio wenyewe kwa wenyewe..Huo sio mdahalo kwa maana halisi ya mdahalo....Otherwise CCM inawatumia hawa jamaa ili wajichanganye wenyewe...Opposition parts,we have to be very carefully with this MAKAMBAs CCM.Ni mzee wa fitna haswa...Na fitna hazina masters wala phd....
 
Nahisi kama amelengeshwa tu na hajastukia kuwa kalengeshwa. Sioni la msingi alilonalo la kulumbana na huyo jamaa. Sidhani kama kuna lolote wanaweza kukubaliana toka moyoni maana sidhani kama wanaaminiana. Wanapoteza muda tu. Miaka mitano ni michache sana...wanapaswa waitumie kuimarisha chama badala ya kukibomoa...
 
Haya saa, tutauangalia wengine wapenzi wa upinzani...ama kweli tunasumbiri mabadiliko bungeni kutoka kambi ya upinzani na sio malumbano. Vyama pinzani vinatakiwa viwe na umoja against ruling party.
 
Aggggggggggrrrrrrrrrrr!!!!!!!!! jamani huu MDAHALO for WHAT???????????

Mbona CDM inataka kuwapa credit hawa mamluki wa CCM????
 
Back
Top Bottom