Mdahalo ITV Bila Profesa Lipumba Na Wengine, Kwanini?

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,
Jana tumesikiliza mdahalo, au labda mazungumzo au mahojiano kati ya Dr Slaa ( CHADEMA) na Rosemary Mwakitwange. Mahojiano yaliyoruhusu wengine kuchangia kwa njia ya simu pia.
Tunawapongeza walioshiriki kufanya jitihada zile. Ilitoa fursa kwa sisi wapiga kura kumsikiliza Dr Slaa. Hata hivyo, pungufu kubwa kabisa lililoonekana ni namna waandaaji walivyoandaa mdahalo wa upande mmoja bila kuwashirikisha wagombea wengine wa Urais waliopitishwa na NEC. Maana, ni vema pia tukatofautisha maana ya mdahalo na mahojiano. Kama yale ya jana yalikuwa ni mahojiano tu, hakuna tatizo kwa mgombea mmoja tu kuhojiwa. Lakini kama unaitwa mdahalo, basi, tujadili maana ya mdahalo.

Kama ni mdahalo, basi, ingekuwa ni vema na busara kwa wagombea wengine wa Urais kushiriki. Bila shaka, wagombea wengine nao wana haki za msingi za kupewa nafasi ya kuelezea sera zao na kujibu maswali ya wapiga kura. Hata kama chama tawala, CCM kimeweka wazi kuwa mgombea wao hatashiriki mdahalo, lakini hatujasikia vyama vingine vitoa misimamo kama hiyo.

Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali. Kungetoa fursa ya wagombea hao kushindana kwa hoja pia. Labda kama kuna maelezo ya kuwa wagombea hao walialikwa lakini hawakuitikia mwaliko wa kwenda studioni. Au kuwa gharama za muda wa kurusha hewani mdahalo ziligharamiwa na chama cha mgombea aliyefika kwenye mdahalo/mahojiano. Kama sivyo, basi, waandaaji watakuwa hawakuwatendea haki wagombea na wapiga kura kwa ujumla wao.

Maana, tukianza sasa kujenga tabia ya kubagua wagombea itakuwa ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, tangu Uchaguzi Mkuu wa 1995, tulianza kujenga misingi mizuri ya wagombea kupewa fursa sawa. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 wagombea wote wa Urais walialikwa kwenye mdahalo uliofanyika kwenye iliyokuwa Kilimanjaro Hotel. Kama inavyoonekana pichani, kulikuwa na Profesa Lipumba, Augustino Mrema, Benjamin Mkapa na Bwana Cheyo. Historia ni mwalimu mzuri. Tujifunze.

Maggid,
Iringa, Jumapili, Oktoba, 24, 2010
 
Maggid,

Good observation! Ki-ukweli kuita kile kilichofanyika jana mdahalo ni misnomer - haukuwa mdahalo. Sifahamu sababu za lipumba kutokuwepo lakini hata kama angekuwepo value added isingekuwa worth the effort. Iko wazi kuwa mpambano wa uraisi sasa umebaki kuwa wa watu wawili Dr. Slaa na Raisi Kikwete na kwa kuwa kikwete kapigwa marufuku na makamba kushiriki midahalo hakukuwa na uwezekano wa kumpata so waandaaji wakaamua kufanya walichokifanya. Unaweza ukawa unaamini kuwa Kina Dovutwa na mzee Rungwe pia walitakiwa washirikishwe, I beg to differ. Mimi naamini ubora wa mdahalo unapimwa na uwezo wake wa ku-influence outcome ya election na sio idadi ya washiriki. Nimalizie kwa kusisitiza kuwa mdahalo ambao utaamua mshindi wa uraisi ungekuwa kati ya kikwete na slaa; we both know that that debate will never be held!!!!

Asante.
denis_79tz.
 
Yaani badala ya kuuliza JK in bold unauliza Prof. Lipumba? By the way taarifa kuhusu mdhalo huu mbona zilikuwepo kwenye vyombo vya habari na JF kama siku nne hivi na ikaelezwa namna itakavyokuwa??
 
Nikushukuru ndugu yangu kwwa angalizo hili,
Mimi binafsi nakukubali kuwa kama tutaita mdahalo basi unaweza kuhusisha wagombea mbalimbali lakini ni set up ya mdahalo wenyewe na waandaaji nami siwezikusema sana kuwa ilikuwa imeandaliwa na Mgombea au Media lakini labda nirekebishwe kuwa mdahalo unaweza kuhusisha watu wawili au wengi zaidi kulingana na mpangilio fulani. Na ndiyo maana hata kama wangefika wagombea wengine, pengine wasingekuwa wote,
Lakini pia kuwa labda kwa ile ya jana tuite kuwa ilikuwa fursa ya Dr. Slaa kuzieleza sera zake na kujadiliana na wapiga kura/ au wakereketwa wake.

Yote hii inategemea na maandalizi, kama taasisi itaandaa set up ya aina hii, basi iantegemea who pays for it, kumbuka kwa mfano tunaona maelezo kibao Star tv, ITV, Ch 10 pamoja na maredio recorded programmes za JK (CCM) akinadi sera na kutangaza utekelezaji wa Ilani zake na kunadi sera mpya.
Hivyo mdahalo wa jana ni mipangilio tu, na haizuii wengine pia kufanya kitu kama hicho
 
u r right BUT, Dr Slaa ndie anaonekana kuwa na chance kubwa ya kuleta ukombozi. siku zimekwisha hakuna muda wa kupoteza, huu uchaguzi umesha julikana ngoma ni kikwete au Dr Slaa, sasa kama kikwete hanafyata mdahalo yanini kuleta wengine walio na 5% na siku zimebaki 6? nikukandamiza kwa Dr tuu. wagombea wengine wakauke tu time is up and they r still way behind. BIG UP ITV FOR A GREAT BROADCAST
 
Nikushukuru ndugu yangu kwwa angalizo hili,
Mimi binafsi nakukubali kuwa kama tutaita mdahalo basi unaweza kuhusisha wagombea mbalimbali lakini ni set up ya mdahalo wenyewe na waandaaji nami siwezikusema sana kuwa ilikuwa imeandaliwa na Mgombea au Media lakini labda nirekebishwe kuwa mdahalo unaweza kuhusisha watu wawili au wengi zaidi kulingana na mpangilio fulani. Na ndiyo maana hata kama wangefika wagombea wengine, pengine wasingekuwa wote,
Lakini pia kuwa labda kwa ile ya jana tuite kuwa ilikuwa fursa ya Dr. Slaa kuzieleza sera zake na kujadiliana na wapiga kura/ au wakereketwa wake.

Yote hii inategemea na maandalizi, kama taasisi itaandaa set up ya aina hii, basi iantegemea who pays for it, kumbuka kwa mfano tunaona maelezo kibao Star tv, ITV, Ch 10 pamoja na maredio recorded programmes za JK (CCM) akinadi sera na kutangaza utekelezaji wa Ilani zake na kunadi sera mpya.
Hivyo mdahalo wa jana ni mipangilio tu, na haizuii wengine pia kufanya kitu kama hicho
Whatever you call mdahalo au majadiliano. swala tunaloangalia ni vipi Dr. Slaa ameweza kufikisha ujumbe kwa ufasaha kwa wapiga kura.
 
Zaidi ya hiyo ndiye aliyewazi na sera zake na yuko tayari zaidi kuzieleza. Na pia ndiye watu wanamtegemea kama masihi wao kwa sasa na hii hali ya Tanzania
 
Ndugu Zangu,
Jana tumesikiliza mdahalo, au labda mazungumzo au mahojiano kati ya Dr Slaa ( CHADEMA) na Rosemary Mwakitwange. Mahojiano yaliyoruhusu wengine kuchangia kwa njia ya simu pia.
Tunawapongeza walioshiriki kufanya jitihada zile. Ilitoa fursa kwa sisi wapiga kura kumsikiliza Dr Slaa. Hata hivyo, pungufu kubwa kabisa lililoonekana ni namna waandaaji walivyoandaa mdahalo wa upande mmoja bila kuwashirikisha wagombea wengine wa Urais waliopitishwa na NEC. Maana, ni vema pia tukatofautisha maana ya mdahalo na mahojiano. Kama yale ya jana yalikuwa ni mahojiano tu, hakuna tatizo kwa mgombea mmoja tu kuhojiwa. Lakini kama unaitwa mdahalo, basi, tujadili maana ya mdahalo.

Kama ni mdahalo, basi, ingekuwa ni vema na busara kwa wagombea wengine wa Urais kushiriki. Bila shaka, wagombea wengine nao wana haki za msingi za kupewa nafasi ya kuelezea sera zao na kujibu maswali ya wapiga kura. Hata kama chama tawala, CCM kimeweka wazi kuwa mgombea wao hatashiriki mdahalo, lakini hatujasikia vyama vingine vitoa misimamo kama hiyo.

Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali. Kungetoa fursa ya wagombea hao kushindana kwa hoja pia. Labda kama kuna maelezo ya kuwa wagombea hao walialikwa lakini hawakuitikia mwaliko wa kwenda studioni. Au kuwa gharama za muda wa kurusha hewani mdahalo ziligharamiwa na chama cha mgombea aliyefika kwenye mdahalo/mahojiano. Kama sivyo, basi, waandaaji watakuwa hawakuwatendea haki wagombea na wapiga kura kwa ujumla wao.

Maana, tukianza sasa kujenga tabia ya kubagua wagombea itakuwa ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, tangu Uchaguzi Mkuu wa 1995, tulianza kujenga misingi mizuri ya wagombea kupewa fursa sawa. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 wagombea wote wa Urais walialikwa kwenye mdahalo uliofanyika kwenye iliyokuwa Kilimanjaro Hotel. Kama inavyoonekana pichani, kulikuwa na Profesa Lipumba, Augustino Mrema, Benjamin Mkapa na Bwana Cheyo. Historia ni mwalimu mzuri. Tujifunze.

Maggid,
Iringa, Jumapili, Oktoba, 24, 2010
CRAP!
Kama kawaida yako.
Hoja zilizoongelewa siyo za msingi mpaka lipumba awepo?
Unatuuliza sisi hapa jukwaani kwani ndio tulioandaa huo mdahalo?
MAGGID umefilisika unasahau hata namna ya kusaka chanzo cha taarifa. watafute walioandaa uwaulize huo upupu wako kisha uje hapa jukwaani kueleza walivyokujibu.
Mbona husemi kwamba kwa nini kila siku kwenye channel ten kunakuwa na nusu saa ya kumnadi KIKWETE baada ya taarifa ya habari? hiyo kwako sio ishu bali ishu ni Dr. Slaa kuandaliwa mdahalo?
Wewe ni mvivu wa kufikiri na nilishasema kwamba HUNA UTAIFA na ni MTU HATARI SANA KWA USALAMA WA NCHI. naongea kwa nia njema na si kuwa nakuchukia bali nachukia the way ulivyo MTUMWA wa watawala wasio na uwezo wa kuongoza nchi.

Lakini muda haujaisha, andaa mdahalo kwa wagombea wengine tusikilize wanavyonadi sera zao. chukua hatua unapoona mambo hayaendi sawa siyo unabaki kulalama kama chekechea

Kaka Majid,lakini si nimesikia kwamba wagombea wengine wataitwa pia ili KUMWAGA sera zao,manake ule sio MDAHALO ki ukweli,lakin fursa nzuri kwa wagombea kusikika watatufanyia nini, Jana mwanawane Dr. WAUKWELI katema vitu mpaka nikawa naona muda hautoshi,acha tumsikie Dr. KINANA nae atawaambia nini wananchi ikifika zamu yake.
 
Unajua hawa jamaa hawajipendei, ila kila wakifikiria kuwa waite watu kwa mjadala wanakutana na maswali kibao yatakayowatia aibu na kupoteza wapiga kura kibao (Yaani wale waliobaki)
sasa inawauma sana lakini kwa kifupi hawana la kusema. DR. KINANA na JK wote wanaweza kumudu recorded air time au ile ya kusikiliza bila kuruhusu maswali.
Otherwise watampa 100% credit Dr. Slaa
 
Ndugu majjid ule haukuwa mdahalo ni nafasi ya chadema na raisi wake kutangaza mikakati atakapoingia ikulu mdahalo kikwete kagoma, na kuhusu maraisi wengine wanaweza mbona kufanya kitu kama kile pia lakini frankly ule haukuwa mdahalo na unaonekana uko bias "ETI kama mdahalo mbona lipumba na wengine hawakuwepo"kwa nini usiulize mbona kikweke hakuwepo
ishu ni kwamba si mdahalo ni mahojiano
 
Profesa Lipumba yeye zamu yake ni ijumaa ijayo tarehe 29/10/2010. Kwa hiyo naye atapata nafasi ya kunadi sera zake kwenye huo sijui mdahalo au mahojiano(waandishi mnajua zaidi tofauti za mdahalo na mahojiano). Pia nasikia siku hiyo Kikwete naye atakuwa na mdahalo, sasa sijui ni TBC au ITV tutapata taarifa zaidi.
 
Sawa Maggid, ule sio mdahalo kwa maana ilikuwa ni upande mmoja kuulizwa na kujieleza. Ila ninavyojua Lipumba atakuwa pale kikaangoni 29 na JK tarehe fulani!

Mimi nadhani tusiwe ni watu wakulalamika tu, tuone fahari kwamba baadhi yetu wamo wanaothamini utu na heshima yetu, kwa kumweka tunayemtegemea kuwa kiongozi wetu kwenye mahojiano ili tuweze kuona kama kweli anatufaa au la. Tuwashukuru hawa waandaaji. Hizi lawama hazijengi. Na nathubutu kusema Kikwete ndiye ambaye anajificha, hataki tumjue zaidi ya tulivyokwisha mjua. Yeye angeona fahari kufika pale na kudai maswali ayajibu. Yeye ndiye ana historia ya utekelezaji, anagetusaidia sana angejitokeza ili tuweze kupima kama anastahili kuendelea kutuhudumia au tumchukue mwingine.
 
Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali.

Hivi hao wengi mwenzetu umewajuaje? Au nafsi yako na matashi yako binafsi sasa unayageuza kuwa ni ya wengi? Maggid stop being hyperbolic man...........

Mdahalo kwa kiingereza ni debate ambayo tafsiri yake ni " to deliberate upon something"....kwa hiyo huhitaji wagombea wengine... to deliberate upon something but you need an audience to do so..................

Hivyo tafsiri yako siyo sahihi hata kidogo kuwa lazima wawepo wagombea wengine ili kukamilisha mdahalo..........

Kuhusu kuwatendea haki nalo umechemsha sana hapo......la muhimu kwetu ni wale wenye nafasi ya kuwa Raisi ndiyo wa muhimu na wala siyo wasindikizaji..... ni Dr. Slaa na Jk ambao wana sifa hizo hao wengine ni kutupotezea muda tu......baada ya JK kuning'inia mitini na CCM yake Dr. Slaa tu alitosha na kadamnasi ya waalikwa kukamilisha mdahalo.......pitia tena tafsiri ya mdahalo........hata marekani wagombea ni wengi lakini mdahalo huwa ni kwa wenye mwelekeo wa kushinda tu na wala siyo vinginevyo...........Yaani wagombea wa democrat and Republican....that is all.

Hakuna swala la kutomtendea mtu haki.....yeye ndiyo anatakiwa ajitendee haki kwa kuweka mazingira ya ushindi na wala siyo kubebwa tu.............
 
Sijui mwenzetu unaishi nchi gani mpaka hujui kwamba Kikwete alishakataliwa na chama chake na makamba kushiriki katika midahalo kwa sababu ameshakubaliwa na wananchi. Kama Kikwete hataingia mitini basi mdahalo wa October 29 thithiem wamruhusu Rais Mtarajiwa Dr Slaa ashiriki na hapo ndiyo wanathithiem wengi nchini watakavyoona mgombea wao jinsi alivyo bomu. GO! CHADEMA GO!

Ushahidi wa CCM kumzuia Kikwete kushiriki mdahalo huu hapa chini, walijua angefanywa vibaya na Rais Mtarajiwa Dr Slaa.
http://www.mwananchi.co.tz/mwananch...ili/4652-ccm-yazuia-jk-kushiriki-mdahalo.html
 
Sawa Maggid, ule sio mdahalo kwa maana ilikuwa ni upande mmoja kuulizwa na kujieleza. Ila ninavyojua Lipumba atakuwa pale kikaangoni 29 na JK tarehe fulani!

Mimi nadhani tusiwe ni watu wakulalamika tu, tuone fahari kwamba baadhi yetu wamo wanaothamini utu na heshima yetu, kwa kumweka tunayemtegemea kuwa kiongozi wetu kwenye mahojiano ili tuweze kuona kama kweli anatufaa au la. Tuwashukuru hawa waandaaji. Hizi lawama hazijengi. Na nathubutu kusema Kikwete ndiye ambaye anajificha, hataki tumjue zaidi ya tulivyokwisha mjua. Yeye angeona fahari kufika pale na kudai maswali ayajibu. Yeye ndiye ana historia ya utekelezaji, anagetusaidia sana angejitokeza ili tuweze kupima kama anastahili kuendelea kutuhudumia au tumchukue mwingine.

Njilembera na Wengine,

Nimechokoza mjadala huu kwa nia njema kabisa. Tuwekane sawa, kwamba kuna tofauti ya embe na chungwa, kwa mwonekano na ladha pia. Kilichokuwa kikitangazwa kabla ya jana ni " Mdahalo". Tulichokiona si mdahalo, na sisi ni watu wazima. Wasije wajukuu zetu wakaja kutushangaa watakaposoma historia. Watahoji upeo wetu wa kufikiri . Kinachoonekana hapa ni ukweli, kuwa wa jana haukuwa mdahalo. Swali linabaki, jana tuliona nini? Mazungumzo, mahojiano au PR? Hivi set up ya mahojiano inatakiwa iweje ili yaitwe mahojiano? Na kwanini aliyeendesha shughuli ile alitambulishwa kama ' Mwenyekiti wa Mdahalo?". Hebu 'Great Thinkers ' tuumize vichwa tuweke hili sawa.
 
mengi in nature mbaguzi na hakuna sumu mbaya kwa taifa kuliko ubaguzi

Nikisoma post zako zote, naona wewe ndie mbaguzi. Huwezi kuona hata jema dogo upande fulani.

Ni uchaguzi wako, lakini wengi saaaaaaaaaaaaaana wanatofautiana nawe.

Pole, haujazoea kuzidiwa nguvu, utazoea sasa.
 
Ndugu Zangu,
Jana tumesikiliza mdahalo, au labda mazungumzo au mahojiano kati ya Dr Slaa ( CHADEMA) na Rosemary Mwakitwange. Mahojiano yaliyoruhusu wengine kuchangia kwa njia ya simu pia.
Tunawapongeza walioshiriki kufanya jitihada zile. Ilitoa fursa kwa sisi wapiga kura kumsikiliza Dr Slaa. Hata hivyo, pungufu kubwa kabisa lililoonekana ni namna waandaaji walivyoandaa mdahalo wa upande mmoja bila kuwashirikisha wagombea wengine wa Urais waliopitishwa na NEC. Maana, ni vema pia tukatofautisha maana ya mdahalo na mahojiano. Kama yale ya jana yalikuwa ni mahojiano tu, hakuna tatizo kwa mgombea mmoja tu kuhojiwa. Lakini kama unaitwa mdahalo, basi, tujadili maana ya mdahalo.

Kama ni mdahalo, basi, ingekuwa ni vema na busara kwa wagombea wengine wa Urais kushiriki. Bila shaka, wagombea wengine nao wana haki za msingi za kupewa nafasi ya kuelezea sera zao na kujibu maswali ya wapiga kura. Hata kama chama tawala, CCM kimeweka wazi kuwa mgombea wao hatashiriki mdahalo, lakini hatujasikia vyama vingine vitoa misimamo kama hiyo.

Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali. Kungetoa fursa ya wagombea hao kushindana kwa hoja pia. Labda kama kuna maelezo ya kuwa wagombea hao walialikwa lakini hawakuitikia mwaliko wa kwenda studioni. Au kuwa gharama za muda wa kurusha hewani mdahalo ziligharamiwa na chama cha mgombea aliyefika kwenye mdahalo/mahojiano. Kama sivyo, basi, waandaaji watakuwa hawakuwatendea haki wagombea na wapiga kura kwa ujumla wao.

Maana, tukianza sasa kujenga tabia ya kubagua wagombea itakuwa ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, tangu Uchaguzi Mkuu wa 1995, tulianza kujenga misingi mizuri ya wagombea kupewa fursa sawa. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 wagombea wote wa Urais walialikwa kwenye mdahalo uliofanyika kwenye iliyokuwa Kilimanjaro Hotel. Kama inavyoonekana pichani, kulikuwa na Profesa Lipumba, Augustino Mrema, Benjamin Mkapa na Bwana Cheyo. Historia ni mwalimu mzuri. Tujifunze.

Maggid,
Iringa, Jumapili, Oktoba, 24, 2010

Kabla ya kuandika makala hii ungefanya utafiti zaidi, nadhani usingeandika ulivyoandika.
 
Maggid ni ni miongoni mwa watu wenye mawazo ya kipumbavu sana....nenda kwenye blog yako nod ukaaandika haya mauharo yako
 
Back
Top Bottom