TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 24,893
- 11,290
ule ulikua mdahalo...Jamani tusimlaumu wala kumtukana Maggid, yuko Sahihi anaposema kuwa ule SIYO MDAHALO, na kwa kusema vile hamaanishi kwamba Slaa hakuongea mambo ya msingi, mdahalo ni baina ya pande mbili au zaidi ambazo zinapambana kwa hoja, sasa ukiangalia setup ile, ni dhahiri kwamba yale ni mahojiano.
Tusivikwe na upofu wa Mapenzi kwa Slaa hata tukasahau ukweli wa mambo na matumizi ya kweli ya maneno, kama kitu ni tunakiita mdahalo, basi kiwe mdahalo kweli, kama ni Mahojiano basi tuyaite mahojiano, otherwise tutaonekana hatukijui Kiswahili chetu vizuri halafu tuendelee kutamba kuwa ni lugha ya taifa.
Maggid ana hoja pale. tusimchukie kwa sababu ya kasumba tu ambayo tumeishaijenga hapa JF.
Watu wanaweza kudhani kwamba hili si jambo la msingi. lakini Matumizi ya maneno sahihi ni muhimu sana.