Mdahalo ITV Bila Profesa Lipumba Na Wengine, Kwanini?

Mdahalo ITV Bila Profesa Lipumba Na Wengine, Kwanini?

Ni kweli mkuu, wagombea wasiojiamini wanataka wapate majibu kabla, lazima tubadilike hatuwezi kushabikia watumia majuche watuongoze! wataletaje maendeleo wakati hawana uwezo wa kufikiri? watanzania tubadilikeni! mimi nawapongeza walioandaa mdahalo/mahojiano kwani tunaweza kuona nani anauwezo na nani mwoga,
 
Kwa maneno hayo kwenye red, hata kama Magid ni Mchmia tumbo namba moja, atatokwa machozi. Haya maneno ndiyo yaliyomfanya Yuda ajinyonge, baada ya kugundua kuwa, pesa si kila kitu. Baada ya kuona mtu wake aliyekuwa anampenda kweli kweli anasulubiwa kwa vipande thelathini vya fedha.
Maggid Pesa si kila kitu. Wala ufuasi was dini haukufanyi uwe mtakatifu. Ni ukweli tu ndiyo utakufanya uishi huru, kwenye jamii ya watu huru, ambao wanakuona wewe ni mwenzao. Jina la Nyerere litaishi milele, lakini sijui kama jina la Kingunge Ngombare Mwiru litadumu hata mwezi mmoja ndani ya masikio ya Watanzania siku Mungu akimchukua!
Usiuze utu, kwa ushabiki na pesa kwa vile tu umelipwa talanta mia. Maisha ni zaidi ya fedha!

Nyumbu,
Alichoandika Gottee na wewe ukanukuu nami nimekisoma. Ameandika yasiyo na msingi, ndio maana sikupoteza muda wangu kumjibu. Sasa nawe umemnukuu, nakujibu maana hayo uliyoyapigia rangi nyekundu hayanisumbui hata kidogo. Ni ya kijinga.

Huyo Gottee aliwahi kuandika haya pia;


"Kwenye Blogu yake Maggid ameshaandika mkataba wake wa kazi anayofanya sasa unaisha mwezi wa 12 mwaka huu. Maggid hata kama unafukuzia 'u DC' ndugu yangu macho yako yawe na aibu! Kuna faida gani kushusha Integrity na credibility yako kwa vivyeo vya 'kipuuzi'


Kuna mwingine aliandika kinachofanana na hicho nikamjibu humu ukumbini. Msikilize;

Quote Originally Posted by Sir R View Post
JK akishinda Mjengwa utakuwa DC



Majibu yangu niliyotoa kwa Sir R;

"Hata nikipewa dhamana ya U-RC nitasema; " Mheshimiwa, asante sana, lakini HAPANA kwa sasa". Ndio, nina mke na watoto wanaonihitaji zaidi katika makuzi yao. Kibarua ninachokifanya sasa na kipato changu, japo kidogo, kinaniwezesha kujikimu. Mimi ni Mjamaa, na kamwe sijawahi kuupenda ubepari. Tatizo letu Watanzania ni hulka yetu ya kuangalia ' vyeo' na vyote vyenye kuambatana na vyeo hivyo, kama vile gari la fahari, safari za ndani na nje na posho. Badala ya kuangalia zaidi dhamana inayoendana na vyeo hivyo.

Ni ujinga pia, kudhani kila mtu anayefikiri tofauti , basi, ni fisadi au kanunuliwa na mafisadi." Mwisho wa kujinukuu.

Nyongeza hapa. Masuala ya mkataba wa kazi yangu hayamhusu aliyetoa hoja hiyo. Si mara yangu ya kwanza kumaliza mkataba wa kazi. Mimi ni mwalimu kitaaluma. Kazi hiyo naipenda sana. Na hakuna kwa sasa uhaba wa ajira ya ualimu hapa Tanzania. Naweza pia kufanya kazi nyingine za kwenye vumbi. Nitaishi tu, nikiwa mtu huru, kama nilivyoishi siku zote, hadi hii leo.
 
Maggid Mjengwa said:
Ndugu Zangu,

Kwanza kabisa , niweke wazi, kwamba kwa staili yangu nilichokoza kwa makusudi mjadala ili kutengeneza mwelekeo wa mjadala ambao ungetusaidia kuyafanya mawili haya;
Mosi, kuumiza vichwa vyetu kujadili nini haswa maana ya mdahalo na hususan mdahalo wenye kuhusu masuala ya msingi ya kitaifa. Kufanya kazi ya kuitafuta tofauti ya kimsingi kati ya mdahalo na mahojiano. Hilo nilijaribu kuliandika kwa msisitizo katika majibu yangu katika baadhi ya posti zenu.
Pili, nilitarajia, baada ya kukaikamilisha kazi hiyo ya kwanza, wengi wetu tungejikita kwenye kujadili issues zilizozungumwa na Dr Slaa usiku ule wa Jumamosi. Nilishangaa, kuwa wengi wakaelekea kwenye kuniachia mimi niifanye kazi hiyo. Sikufanya hivyo, kwa makusudi kabisa. Ningefanya hivyo, mjadala huu ungemalizika jana usiku kwa watu kuandika ‘ thanks’ zao. Tusingejifunza mengi.

Tukija kwenye issues, Dr Slaa alipata fursa nzuri sana ya kujieleza. ( Niligusia hilo kwenye moja ya majibu yangu ya posti ). Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, Dr Slaa angefanya vema zaidi kama angepambanishwa na mtu kama Profesa Lipumba. Na hapo, umma ungeweza kumpa alama za ziada. Na laiti JK naye angeingiza timu, basi, tungeshuhudia ‘ mdahalo wa karne’ kati ya Profesa Lipumba, Jakaya Kikwete , Dr Slaa na akina Hashim Rungwe na wenzake. Ni katika hali kama hizo, wapiga kura tunasaidiwa kupeperusha pumba na kubaki na mchele. Niliandika, kuwa ni mkakati wa kimakosa kwa CCM kuamua kutoshiriki midahalo. Maana, huko twendako wataihitaji na kuna watakaowashangaa watakapoonyesha hitaji hilo.
Sababu kubwa ya kuwepo walau wagombea wawili kwenye mdahalo ni ukweli, kuwa wapiga kura tungepata fursa ya kusikia sera mbili tofauti au majibu mawili tofauti kwa swali moja. Hapo, tungeweza kujua nani bora zaidi.

Format ya maswali ingekuwa ni yale maswali magumu yanayohusu most controversial issues of our time. Issues kama uharibifu wa mazingira, ufisadi, mikataba mikubwa ya uwekezaji,. Rasilimali za nchi kama madini, Uongozi bora na maadili ya viongozi( Tuna mfano wa Rais aliyefungua kampuni binafsi na kwa kutumia anwani ya Ikulu)
Tuna issues kama za kuwepo au kutokuwepo kwa wagombea binafsi, Katiba, Uraia wa nchi mbili, upigaji kura kwa Watanzania walio nje, mishahara ya Wafanyakazi, nafasi ya wakulima katika uchumi wan chi (Kilimo kwanza), maradhi (UKIMWI na Malaria). Bila kusahau Kushuka kwa elimu na utitiri wa international schools na academies zilizo chini ya viwango. Na mengineyo mengi.
Kuna pia maswali ambayo hayakuulizwa usiku ule. Moja ni hili la itikadi. Mathalan, Dr Slaa na CHADEMA wanasimama katika itikadi gani kwa sasa katika kutekeleza sera zao? Na kama Jakaya Kikwete, Profesa Lipumba na wengine wangekuwapo, nao wangeulizwa swali hilo.
Mwisho, nasikitika kuwa huenda wagombea wengine wa Urais mbali ya Profesa Lipumba , hawatapata nafasi ya kufanya mahojiano kama wenzao wa CHADEMA, CUF na labda CCM. Nafikiri hawatendewi haki akina Hashim Rungwe , Kuga Mziray na mwenzao Muta wa TLP kama nao hawatapata hata robo saa tu ya mahojiano.
Huko twendako, tuwe na matayarisho ya mapema ya midahalo ya kitaifa inapofikia wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu au masuala mengine makubwa ya kitaifa, kama vile Katiba mpya. Kuwepo na taasisi huru na zenye kuaminika na umma zitakazoratibu midahalo hiyo. Kuwepo na kalenda ya midahalo. Mgombea atakayeshindwa kuhudhuria katika tarehe husika ilihali amepewa mwaliko, basi, huyo itakuwa ‘ imekula kwake’ kama wanavyosema mitaani siku hizi.

Nihitimishe kwa kuwashukuru nyote. Nimesoma kila kilichoingizwa kwenye mjadala huu. Kuna mlionishambulia kwa matusi, nimeyasoma matusi yenu, mengine yamenivunja mbavu. Kuna mliotoka nje ya mada na kunishambulia mimi binafsi badala ya kuikabili hoja iliyowasilishwa. Hilo nalo ni pungufu la kawaida. Na kwa kuchokoza mjadala huu kuna wanaojisikia nimewakwaza, basi, haikuwa dhamira yangu. Sijaufunga mjadala.

Ahsanteni Sana.
Iringa,
Jumatatu, Oktoba, 25, 2010

Maggid,

..nadhani tatizo limetokana na Kikwete kukataa kwenda kwenye mdahalo.

..huyu bwana inaelekea hapendi midagalo. hata mwaka 2005 ambapo ilikuwa dhahiri atashinda hakutaka kufanya mdahalo.

..Raisi alikuwa na muda wa kwenda kuangalia mechi ya Taifa Stars, na kuserebuka kwenye birthday la kukata na shoka lakini hana muda wa mdahalo.

..tukubaliane tu kwamba Raisi tuliyenaye hapendi kabisa mahojiano na majadiliano ya kisomi-kisomi. kama kweli ungekuwa genuine basi ungeelekeza lawama zako kwa Kikwete.

..nakubaliana na wewe kuhusu kuanzishwa kwa taasisi "huru na zinazoheshimika" zitakazoweza kuandaa midahalo huko mbeleni. we could have started na hawa waliojaribu kuandaa mdahalo na Kikwete akaupinga. tungeweza kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuboresha huko mbele ya safari.

..hata kwenye nchi zinazoendelea kuna kuwepo na midahalo iliyoandaliwa na conservative groups, liberal groups, etc etc. wagombea hujitahidi kushiriki ktk midahalo hata kama imeandaliwa na taasisi wasizokubaliana nazo, kwa sababu wagombea hao wanajiamini in the power of their ideas.

NB:

..CCM sasa hivi ni chama cha mizengwe-mizengwe mno. hawataki kabisa majadiliano yoyote yale ya kisomi, yanayohitaji tafakuri za kina. suala hilo linajidhihirisha na jinsi Raisi Kikwete anavyoandamana na makundi ya wanamuziki ili kuwalainisha na kuwahadaa wananchi kabla hajatumbukiza uongo wake.
 
Alichokisahau Maggid Mjengwa ni kuleta Wagombea wenza watatu wa CCM , CUF na CHADEMA kujieleza kwa Watanzania na kujulikana kuwa chama chao kitakaposhinda watu hawa ndio watakua wasaidizi wa Rais au kuwa na Marais pindi Rais akiwa Mgomnjwa au akifariki hii ingekua ni plus kwa Mgombea kuonekana amechagua mtu makini kuwa msaidizi wake.
 
Maggid, unapaondika pumba zako kaa chini utafakari unachoandika, acheni kuwa waandishi uchwara, mnatumia viblog vyenu kuganga njaa, unataka kutueleza hujui ccm ndio waliokataa mdahalo? Lipumba anaeleweka ni ccm B anachojaribu kufanya ni kugawanya kuwa za upinzani ili aisaidie ccm kupata ushindi Jaribu kuwaelemisha ccm na vibaraka wake nini maana ya mdahalo usitupotezee muda kusoma pumba ndefu ambazo hazina maana yoyote.
 
Back
Top Bottom