MCL: DPP kurudisha fedha za 'plea bargain' kwa waliodhulumiwa

Maisha yapo kasi, nasikia kizunguzungu!
Serikali ya utawala onevu iliumiza watu ile!
Dola inakuwa jambazi dhulumati! Mbaya

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Duuh, huyu "SHUJAA WA AFRIKA" alikuwa kiboko balaa....!!

Huyu shujaa gani aliyekuwa anahusudu dhuluma to that extent..?

Shujaa aliyedhulumu mpaka uhai wa watu. Hawa nao warudishiwe uhai wao..!!
 
“Waathirika” watarudi kudai kwamba walikiri under pressure?

Huyu DPP anapaswa kuchunga kauli zake na ajiepushe na siasa. Juzi kati tu hapa Singasinga nae kaminywa, akakiri na akabargain kulipa bilioni 26. Hii nayo itaangaliwa upya?!
 
Hakika awamu ya Mwendazake ilijaa dhuluma na unyanyasaji mwingi sana.

View attachment 1823783
Hata Kiswahili hujui mkuu amesema walioathirika yaani kama kuna Mtz alikuwa part wa kesi husika then analipwa pesa kiasi fulani na serikali inachukua kinachobaki. Someni sheria inayohusika na plea bargaining. DPP hana uwezo wa kuwarudishia watuhumia wakati hiyo ni hukumu ya Mahakama mkuu!
 
Wengi hii habari hamjaielewa mnakurupuka tu. Wataorudishiwa ni wale ambao wameathiriwa na hao waliofanya na kukiri makosa. Zingine zitabaki serikalini.
Mfano ulidhulumu watu, ukapelekwa mahakamani ukakiri kosa. Hivyo pesa itarudishwa kwa waliodhulumiwa
Hawa makamanda uchwara wametelekeza akili zao pale ufipa. Wao kila kitu hivi sasa ni kushangilia tu hata bila kufikiri.
 
Back
Top Bottom