Mchungaji Mtikila ashinda kesi ya kumkashifu rais Kikwete

Hivi hii serikali imewahi kushinda kesi gani vile...... ndio maana mamikataba yetu ya hovyo, wanasheria wa hovyo, wanafundishwa na walimu wa....., majaji wanateuliwa na rais wa.........
 
Ni kigeugeu,wanajuwa hana madhara makubwa kwa serikali,lakini anayo madhara kwa upinzani kwasababu anatumika kuzigawa kura za upinzani na hatimaye ccm kushinda.Shida ni kwamba haaminiki huyu,na anapenda sana pesa kuliko hata hayo ya kuwakomboa watanzania,yeye anapiga kelele ili mkono uende kinywani,rejea ile issue ya RA,kule Mara kwenye uchaguzi wakati wa kifo cha Wangwe pamoja na ile kesi aliyoifunguwa eti amekamatwa makalio yake.Huyu ni pesa tu zinamzidia hata uzalendo.

usikute hata pesa za mawakili kapewa na rostitamu
 
Serikali ya majuha. wastage of Tanznian money. They new what they wanted but just to frustrate the Dp leader not to proceed with his compagn.
 
usikute hata pesa za mawakili kapewa na rostitamu
Very possible,huyu tatizo lake ni mbinafsi,its all about him,na ndiyo maana ameshindwa kushirikiana na wenzake kuiondoa ccm.

RA alimpa pesa halafu akaweka ushahidi wa documents,jamaa akaufyata,sasa imagine keshachukuwa ngapi na wapi?

Serikali huwa inamjengea legitimacy ya kuonekana kuwa ni mpinzani haswa,lakini mimi huwa nadhani ni divide and rule ya ccm na serikali yake.
 
Yesu "alidesa" hiyo hukumu ? nyie watu mna utani mbaya !
wewe vipi wewe.....aliyesema hiyo ni WATU au Mtikila?...muulize Mtikila.

Usikubali kuwa mtumwa wa fikra.....ukiambiwa kitu kilicholetwa na jahazi, changanya na kilicholetwa na bed ford.
 
hivi hii serikali imewahi kushinda kesi gani vile...... Ndio maana mamikataba yetu ya hovyo, wanasheria wa hovyo, wanafundishwa na walimu wa....., majaji wanateuliwa na rais wa.........

iliwahi kushinda kesi ya babu seya dhidi ya jamuhuri
 
Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka timbwili lingine baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja. Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.
 
unapoandika hakikisha umetulia, manake badala ya kuelekeza ndio umeharibu kabisaaaaa!

nimejikuta nacheka hadi abiria wenzangu wananishangaa,kiherehere cha kuandika hadi maneno yanapandana.
 
.


Mchungaji Christopher Mtikila akipunga mkono baada ya kutoka na ushindi katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili katika mahakama ya Kisutu jiji Dar es Salaam leo.
Ambapo amesema kwamba alikuwa anajua kwamba hakuwa na kosa na kuwa maandiko yamesema ‘isimamie imani yako' na ndivyo alivyofanya, na kuwa ametekeleza maagizo ya Biblia na haki yake ya kuiamini na kuitetea iko katika katiba ya Jamhuri na katiba hiyo imesema ‘asiingiliwe'

Mchungaji Mtikila akinong'onezana jambo na mtu wake wa karibu mahakamani hapo wakati akisubiri hatma ya kesi yake.

Akitoka mahakamani kwa kicheko baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.

Mchungaji Mtikila akizungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema katika nchi hii atamshangaa mtu asiyeguswa na kutetemeka katika masuala yanayomhusu Mwenyezi Mungu. Hivyo lazima tumuombee hakimu wa kesi yake na mahakimu wengine wote inapofika katika jambo linalomhusu Mungu.



Na. MO BLOG TEAM.

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa akikabiliwa na kesi ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

Mtikila anadaiwa kati ya Januari 2009 na Aprili 17- 2010 jijini Dar es Salaam kwa nia ya uchochezi alisambaza kwa umma nyaraka za uchochezi.


Na katika Shitaka la pili, anadaiwa Aprili 16, 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka huo wa uchochezi kwa jamii.

Picha na maelezo kwa hisani ya Mo Blog
 
Kwa hiyo aliye shindwa kesi ameambiwa afanye nini na mahakama?
 

Huyu Jamaa anashinda kesi zake... ubaya sijui kwanini asigombee UBUNGE; Uraisi hawezi kuupata
 
Back
Top Bottom