Mchungaji Mtikila ashinda kesi ya kumkashifu rais Kikwete

Kesi zote alizoshinda ni zile ambazo yeye ni mshtakiwa. Nasubiri nione kesi ambayo yeye atakuwa upande wa mashtaka!
 
Tangu nianze kusikia huyu mchungaji ana kesi na serikali sijawahi kusikia serikali imemshinda
 
Hakukuwa na ushahidi wa kumweka hatiani.
Hii inaonesha jinsi ma lawyer wa serikali walivyo wataalamu wa kukurupuka!
 
Tatizo lake amewaweka watu ambao hawajui kutafuta evidence!
Hii kesi angenipa mimi hakika ningempa ushindi.

JK bana angekuwa anaingilia uhuru wa mahakama saizi Mtikila angekuwa Segerea.
 
JK bana angekuwa anaingilia uhuru wa mahakama saizi Mtikila angekuwa Segerea.

Mtikila hana madhara yoyote kwa ccm na serikali yake. Kwa lugha nyepesi mtikila ni swahiba wa fisadi mkuu rostam aziz kwahiyo hana guts za kuikamata uchawi serikali.
 
Imekuwaje tena na Mokiwa mkuu?

soma hapo chini

Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi kumshitaki Askofu Dk. Valentino Mokiwa wa Anglican.

Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.

Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo ufisadi wa au wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Iringa.

Mtikila alivyoitwa na Askofu kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nocholas, usiku wa saa 03:00.

Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti, kazi ambayo aliifanya yeye baada ya kufunga mlango.

Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.


"Mlalamikiwa alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna aliyebisha.

Alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipepesa sehemu za siri za mlalamikaji".

Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha. Madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo

Kesi inataarifiwa kuwa kwenye Mahakama
ya Kisutu, chini ya Hakimu Mchome.

SOURCE: AMANI
DATE: TODAY
PAGE: 02,03
MHARIRI: 0714-895555, 0655-207520, 022-2773357
 
Ha ha haa, Mti- Killer ni noma, hawajawahi kumtia hatiani wakati kila mara wanamshtaki!
 
Haaa! Haaa! Kaaa! Kwa hiyo kutoka mahakamani wametibitisha kuwa Baba mwanaasha ni mhuni, aise! Hii imenifurahisha.
 
Mtikila kanifurahisha mwishon alipomwambia askari mmoja kuwa hana cheo kinachotosha kum-arest. Askari kawa mdogo kama piriton:
 
Nimeona itv baada ya kushinda kesi akataka kudakwa tena kwa kesi nyingine ila akagoma kisa askari anayetaka kum arrest ana cheo kidogo
 
Back
Top Bottom