Mchungaji Mtikila ashinda kesi ya kumkashifu rais Kikwete

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,941
Husika na kichwa habari hapo juu mchungaji mtikila ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili kwa 'kumkashifu' rais Kikwete

Source: ITV

Kwa maelezo zaidi ili watu waelewe maelezo haya:

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.

Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.

Akizungumza na mtandao huu baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema "Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu".

mtikila.jpg


Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Part(DP), Mchungaji Christopher Mtikila ana kesi ya kujibu katika kesi ya kuchapisha na kuusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.


Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo ikiwa ni siku chache baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake baada ya kuwaleta mashahidi watano kutoa ushahidi wao.

Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi wa upande wa Jamhuri,amefikia uamuzi wa kumuona Mtikila ana kesi ya kujibu na kwamba maana hiyo Mtikila atatakiwa na mahakaa hiyo kupanda kizimbani Aprili 11 mwaka huu kwaajili ya kuanza kujitetea.


Baada ya Hakimu Fimbo kutoa uamuzi huo, Mtikila alidai kuwa anatarajia kuleta mashahidi 10.

Februali mwaka huu, Mtikila alikiri maelezo aliyochukuliwa na afisa wa polisi ni yake na kwamba hana pingamizi nayo na hivyo mahakama iliyapokea kama kielezo cha upande wa jamhuri.Mtikila katika maelezo hayo ya onyo alikiri kuwa ni kweli aliuandaa waraka huo na kuusambaza ila akakanusha waraka huo si wa uchochezi ila unahusu maneno ya mungu.

Mtikila alikiri maelezo hayo yaliyosomwa na kutolewa mahakamani kama kielelezo baada ya shahidi wa Jamhuri, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Ibeleze Mrema (54) kudai kwamba Aprili 15, mwaka 2010 akiwa kituo cha polisi kikuu jijini Dar es Salaam, aliitwa na mkuu wake wa kazi na kumpa kazi ya kumhoji Mtikila kuhusu tuhuma za kukutwa na waraka wa uchochezi.

Alidai kuwa wakati akimhoji mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na nyaraka hizo na kwamba alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuokoa wakristo na alisaini yeye waraka huo.

"Mtikila alikiri kuhusika kuandaa waraka huo kama mwenyekiti alisaini kwa niaba ya wengine … nilipomhji walichapisha wapi mtikila hakupenda kusema bali alidai kuwa zilikuwa nyaraka 100,000 ambazo zilisema kwamba Rais Kikwete anaangamiza ukristo na amekuwa jasiri kuingiza uislamu katika katiba ya Jamhuri" alidai Mrema kupitia maelezo hayo yaliyotolewa na Mtikila.


Mrema aliendelea kudai kupitia maelezo hayo kwamba, Mtikila alikuwa anahamasisha wakristo wajitoe mhanga kukomesha ugaidi na wamuweke rais mkristo Ikulu.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari mwaka 2009 na Aprili 17, mwaka 2010 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya uchochezi mshitakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema 'Kikwete kuuangamiza ukristo', 'wakristo waungane kuweka mtu Ikulu' alinukuliwa Mtikila.

Katika shitaka la pili, Aprili 16, mwaka 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka wenye uchochezi kwa jamii.Na katika kesi hii Mtikila hana wakili wa kumtetea na anajitetea mwenyewe.


=================
UKUMBUSHO
=================

Hapa chini ni habari na sababu ya kukamatwa kwake iliyokuwa imepostiwa siku za nyuma; Ilipostiwa tarehe 03/11/2007 katika uzi huu - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-akamatwa-na-polisi-kwa-kumkashifu-rais.html

Polisi wa upelelezi (CID) kutoka makao makuu ya CID Dar es Salaam walimkamata Mchungaji Christopher Mtikila, jana saa 11 jioni (1700hrs) saa za Afrika Mashariki na kufanya naye mahojiano hadi saa 3.30 usiku (2100hrs) walipomuachia kabla ya kumkamata tena leo baada ya kumfanyia upekuzi nyumbani kwake Ilala flats, Block F 4 namba A 8, pale pale karibu na TBL, na sasa wamemshikilia Central Police station, hadi Jumatatu atakapopelekwa mahakamani.

Miongoni mwa matamshi aliyoyatoa ni pamoja na kumuita Rais Gaidi na mhuni. Katika mahojiano yote, Mtikila amekiri kusema maneno hayo na hakukataa hata neno moja na mengine makali zaidi na aliyahalalisha kwa kurejea maandiko mbalimbali
 
Ile Kesi yake ya Uchochezi,,Mahakama imemwona hAna Hatia ..kutoka na Ushahidi ulioletwa na JMT...

*Nakumbuka Bwana mdogo wangu mmoja anasema Hajawahi Kushindwa Kesi na SErikali..

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Husika na kichwa habari juu mchungaji mtikila ameshinda kesia ilikuwa inamkabili ya kumkashifu Jk

source: ITV

Hebu tukumbushe kdg,au dadavua kiundani kdg,ni kesi ipi,japo maelezo ya kesi kwa ufupi
 
Husika na kichwa habari juu mchungaji mtikila ameshinda kesia ilikuwa inamkabili ya kumkashifu Jk

source: ITV
kumbe aliyoyazungumza kuhusu Kikwete yalikuwa ya kweli!!!! Kwahiyo serikali inapaswa kumlipa Mtikila na kumwajibisha aliyeshindwa
 
andika zaid kama hivi watu wakaelewa:

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.

Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.

Akizungumza na mtandao huu baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema "Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu".



 
Mkuu remote
ulihisi kuna kesi hapo ..ilikuwa ni upungufu wa akili wa serikali yetu easy ..nenda sikiliza majibu ya hakimu akitoa hukumu utajua uko na serikali ya aina gani
 
Husika na kichwa habari hapo juu mchungaji mtikila ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili baada ya kumkashifu rais Kikwete

source: ITV
Asante kwa taarifa ungebadilisha kidogo ili isomeke " kesi iliyokuwa inamkabili ya tumuhuma za kumkashifu JK"
 
Mkuu remote
ulihisi kuna kesi hapo ..ilikuwa ni upungufu wa akili wa serikali yetu easy ..nenda sikiliza majibu ya hakimu akitoa hukumu utajua uko na serikali ya aina gani

Mtikila kashinda kesi ndio, lakini haki yetu ya kutoa maoni ii wapi, haki ya kuwasema viongozi wabovu ii wapi.

Sheria aliyoshitakiwa nayo ni sheria ya kidhalimu sana ambayo inabidi iondolewe katika vitabu vya sheria.

Haiwezekani eti kuichambua serikali kunaweza kuleta uvunjifu wa amani
 
Ile Kesi yake ya Uchochezi,,Mahakama imemwona hAna Hatia ..kutoka na Ushahidi ulioletwa na JMT...
*Nakumbuka Bwana mdogo wangu mmoja anasema Hajawahi Kushindwa Kesi na SErikali..

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Mbona ameshawahi kula mvua moja gerezani kwa kumkashifu Mwalimu Nyerere!
 
huyu mtikila ni jembe lakini nashindwa kuelewa ni kwa nini inakuwa ngumu sana kumwingiza kwenye mapambanao na makamanda wenzake,jamaa anafaa sana kutetea anachokiamini,wapi Kayinga msaidizi wake,nakumbuka enzi zile alikuwa mchungaji pale shule ya uhuru Kayinga alikuwa habanduki ubavuni mwake
 
Back
Top Bottom