Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mmezoea viongozi wanafiki kama kina mkatoliki, wao hata kama ina madoa wanasema ni Clean,clean ...absolute clean
Tumewachoka viongozi wanafi sasa ni zama za kusema ukweli na ndicho afanyacho Gwajima
Gwajima ni tapeli kama matapeli wengine.

Ukweli utabaki kuwa ukweli chuki na roho yake ya visasi si funzo kwa wakristu tunaofuata mafundisho ya Bwana YETU YESU KRISTU.
 
We unadhani asiposemea pale UFUFUO NA UZIMA chombo kipi kingine watamruhusu aseme? TUNAHITAHITAJI WATU WASI
 
Hata mimi nina mashaka nae..Ila adui wa adui yako ni rafiki yako sometimes..Twende kazi baba askofu
 
Utumishi wake kwa Mungu atajua yeye na Mungu wake. Haturuhusiwi kujudge imani ya mtu.
Hapa BASHITE tu, kila mtu na Mungu wake!
 
Say he goes against God! Ideally you are right, but because the system has decided to remain silent over all the awkward events about Bashite, I think God has chosen Gwajima to speak on behalf of the oppressed and Tanzania in general.live long Gwajima.
I presume,,,,,,,,,,,,,,,I salute toooo
 
Nina shaka na uaskofu wa Gwajima! Kuandika hivi sina nia mbaya....narudia tena sina nia mbaya na wala sipo upande wa mtu yeyote yaani sipo kwa Gwajima wala Bashite.......

Kwa mtazamo wangu kiimani naona kwamba "reactions" za huyu baba askofu kwa Makonda hazisadiki dhamana kubwa alinayo kama askofu mbele za mwenyezi Mungu! The fact that we are not perfect, we can't use it as an excuse! If God is only what we have then God is only what we need..

Haina haja ya kujikweza na kujionesha ni jinsi gani tulivyo wasafi na waungwana mbele za binadamu kwa kupitia madhaifu ya adui zetu isipokua maandiko yanasisitiza tuwaombee adui zetu na kuwasamehe wanaotuudhi....!!!

Ninaamini kuwa unyenyekevu ni kati ya nguzo muhimu sana kwa wafuasi wa Mungu! Bila shaka kuna ndugu zangu wengine mtakua mmenielewa......

Thanks for your attention and may God bless you abundantly!!!
All I can say is let's pray for our country!

Una mashaka na "uaskofu" wa Gwajima? Basi na wewe anzisha kanisa lako ujiite "Askofu" ili na sisi tuwe na mashaka na wewe!

[HASHTAG]#UsitafuteKikiKwaGwajima[/HASHTAG]
 
Ukweli uache ujidhihiri wenyewe, askofu huyu magumashi analazimisha ukweli kwa visasi na roho ya chuki na kujaza waumini kuamini kuwa kisasi ni njia pekee ya kumkomoa adui.
Dunia uwanja wa vita ukiwa legelege watu watakuzushia kila jambo
 
Bila kujali kuwa Gwajima ni nabii wa uongo au ukweli...ukweli utabakia kuwa ukiwa unamtumikia MUNGU wewe ni zaidi ya raisi. Mungu anasema, yeye ni Mfalme wa Wafalme, ni Bwana wa Majeshi, ukiwa unamtumikia yeye unakuwa ni zaidi ya mkuu wa majeshi ya nchi.
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tuu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajims ni muumni wake mtiifu, koss ls Makonds ni lipi?!.

Jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kuume mgeuzie na la kushoto. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.

Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
Jumatatu Njema.
Paskali
Huyu mchungaji ni ajenti wa IBILISI, na kila anaemuamini na kumfuata, ataishia MOTONI, mwenye masikio na asikie !
 
k

kwangu mimi gwajima si mchungaji sahihi wa mungu namaanisha amejiita kwenye uchungaji hakuitwa na mungu muchungaji yoyote hawezi kuwa na kisasi hata siku moja muchungajki aliyeitwa na mungu hawezi toa tatizo kwa mutu na kulipeleka kwa mtu mwingine akidai ni adui yake hapana kabisa huyo ni mchungaji wa misukule tu
 
Back
Top Bottom