Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais... | Page 57 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 27, 2017.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,710
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
  Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

  Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
  Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

  Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

  Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tuu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajima kuwa anajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, sio Mkuu wa Mkoa, Makonda, bali ni muumini wake mtiifu, ambaye nimemtaja hapa chini na alichokisema!, sasa kosa la Makonda ni lipi?!.

  Jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alivyotufundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto, mgeuzie na la kuume!. Yesu ametufundisha "adui mpende". Yesu ametufundisha "samehe hata saba mara sabini". Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo?! .
  Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
  Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
  Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
  Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
  Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.
  Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.

  Jumatatu Njema.
  Paskali
   
 2. demi

  demi JF-Expert Member

  #1121
  Mar 20, 2017
  Joined: Nov 22, 2016
  Messages: 8,003
  Likes Received: 14,764
  Trophy Points: 280
  Utumishi wake kwa Mungu atajua yeye na Mungu wake. Haturuhusiwi kujudge imani ya mtu.
  Hapa BASHITE tu, kila mtu na Mungu wake!
   
 3. balibabambonahi

  balibabambonahi JF-Expert Member

  #1122
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 5, 2015
  Messages: 6,082
  Likes Received: 3,748
  Trophy Points: 280
  Alikwambia nani? Mbona Daud alimchukua mke wa ndugu yake na mtoto aliyezaliwa ndo mfalme Suleiman?
   
 4. balibabambonahi

  balibabambonahi JF-Expert Member

  #1123
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 5, 2015
  Messages: 6,082
  Likes Received: 3,748
  Trophy Points: 280
  I presume,,,,,,,,,,,,,,,I salute toooo
   
 5. Mr Alola

  Mr Alola JF-Expert Member

  #1124
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 11, 2016
  Messages: 478
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 180
  Kukaa kimya ni jibu kwa mjinga , wakatoliki si watu wa kupayukapayuka na kuendekeza majungu nakujaza waumini roho ya visasi. Huwa tunaacha ukweli ujidhihiri, hata kama utachelewa kufika.

  Gwajima ni mtu wa visasi na roho ya kwanini.
   
 6. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1125
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 145

  Una mashaka na "uaskofu" wa Gwajima? Basi na wewe anzisha kanisa lako ujiite "Askofu" ili na sisi tuwe na mashaka na wewe!

  #UsitafuteKikiKwaGwajima
   
 7. Malilambwiga

  Malilambwiga JF-Expert Member

  #1126
  Mar 20, 2017
  Joined: Jul 19, 2015
  Messages: 461
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Kanisa lake limeongezeka waumini baada ya kuacha kuhubiri injili na badala yake kuanza mipasho
   
 8. k

  kiatu kipya JF-Expert Member

  #1127
  Mar 20, 2017
  Joined: Dec 4, 2016
  Messages: 3,257
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Dunia uwanja wa vita ukiwa legelege watu watakuzushia kila jambo
   
 9. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #1128
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,719
  Likes Received: 30,975
  Trophy Points: 280
  mkuu woga ndiyo adui yetu mkubwa
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1129
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,285
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Bila kujali kuwa Gwajima ni nabii wa uongo au ukweli...ukweli utabakia kuwa ukiwa unamtumikia MUNGU wewe ni zaidi ya raisi. Mungu anasema, yeye ni Mfalme wa Wafalme, ni Bwana wa Majeshi, ukiwa unamtumikia yeye unakuwa ni zaidi ya mkuu wa majeshi ya nchi.
   
 11. L

  LuSilk JF-Expert Member

  #1130
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 14, 2016
  Messages: 784
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 80
  Huyu mchungaji ni ajenti wa IBILISI, na kila anaemuamini na kumfuata, ataishia MOTONI, mwenye masikio na asikie !
   
 12. Bashite og

  Bashite og Senior Member

  #1131
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 15, 2017
  Messages: 173
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  k
  kwangu mimi gwajima si mchungaji sahihi wa mungu namaanisha amejiita kwenye uchungaji hakuitwa na mungu muchungaji yoyote hawezi kuwa na kisasi hata siku moja muchungajki aliyeitwa na mungu hawezi toa tatizo kwa mutu na kulipeleka kwa mtu mwingine akidai ni adui yake hapana kabisa huyo ni mchungaji wa misukule tu
   
 13. Bashite og

  Bashite og Senior Member

  #1132
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 15, 2017
  Messages: 173
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  anamtumikia mungu yupi
   
 14. roboka kafwekamo

  roboka kafwekamo JF-Expert Member

  #1133
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 12, 2017
  Messages: 828
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 80
  Gwajima kavunjiwa heshima na lazima ajitetee kwa alivyoona yeye inafaa
   
 15. Bashite og

  Bashite og Senior Member

  #1134
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 15, 2017
  Messages: 173
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  kw
  kwa mtumishi wa mungu yupi kama ni gwajima hapana
   
 16. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #1135
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,827
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kweli yeye ni zaidi ya Rais katika madhabahu/familia yake, kama wewe ulivyo zaidi kwa mkeo/mmeo.
   
 17. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #1136
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,491
  Likes Received: 3,791
  Trophy Points: 280
  Kwa maana nyingine waumini wanapenda ushilawadu.
   
 18. Bashite og

  Bashite og Senior Member

  #1137
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 15, 2017
  Messages: 173
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  point tupo
   
 19. King Adolfo Osaka

  King Adolfo Osaka Member

  #1138
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 15, 2017
  Messages: 44
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 25
  Duuuh!
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1139
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 41,816
  Likes Received: 24,644
  Trophy Points: 280
  Jamaa anamiss sana bahasha za Lowasa
   
 21. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1140
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 39,072
  Likes Received: 30,844
  Trophy Points: 280
  I culudu be the IGP
   
Loading...