Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais... | Page 58 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 27, 2017.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,764
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
  Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

  Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
  Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

  Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

  Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tuu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajima kuwa anajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, sio Mkuu wa Mkoa, Makonda, bali ni muumini wake mtiifu, ambaye nimemtaja hapa chini na alichokisema!, sasa kosa la Makonda ni lipi?!.

  Jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alivyotufundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto, mgeuzie na la kuume!. Yesu ametufundisha "adui mpende". Yesu ametufundisha "samehe hata saba mara sabini". Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo?! .
  Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
  Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
  Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
  Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
  Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.
  Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.

  Jumatatu Njema.
  Paskali
   
 2. Konsciouz

  Konsciouz JF-Expert Member

  #1141
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 12, 2015
  Messages: 4,344
  Likes Received: 4,946
  Trophy Points: 280
  Dogo jifunze kua na akiba ya maneno...
  Unaingilia kazi ya Mungu kuhusu nani aende peponi na nani aingie MOTONI.
  We ni mkristo I hope hebu fanya kupitia
  James 3:3-6
  Proverbs 18:21
  Soma kitabu chenu you'll learn a lot.
  Ni kweli vitabu vimetuonya kuhusu manabii wa uongo...Lakini yatupasa kua makini unapo mtuhumu mtumishi wa neno la Mungu.
  Simemi Gwajima ni mtumishi wa Mungu au sio.
  Ninacho emphasize hapa ni bora ujitenge na kukashifu hawa watu maana hata vitabu vinasema hivyo rejea
  Psalms 105:15
   
 3. LadyAJ

  LadyAJ JF-Expert Member

  #1142
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 21, 2015
  Messages: 6,935
  Likes Received: 8,888
  Trophy Points: 280
  We nae ni wale wale tu
   
 4. Mr Alola

  Mr Alola JF-Expert Member

  #1143
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 11, 2016
  Messages: 478
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 180
  Dunia uwanja vita lakini mwisho wetu ni chini mavumbini.
   
 5. Mr Alola

  Mr Alola JF-Expert Member

  #1144
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 11, 2016
  Messages: 478
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 180
  Wale wale wakina nani?

  Kama wewe ni mpagani utaona sawa na kushabikia , kama wewe ni muislamu ni utashangila maneno yake huyu Gwajima , lakini kwa Mkristu aijuaye vema mafundisho ya Kristu Yesu ni dhahiri atapingana na baadhi ya maneno ya kichonganishi na ya kufitinisha anayoyatoa Huyu Mchungaji.
   
 6. p

  pilipili kichaa JF-Expert Member

  #1145
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 3, 2013
  Messages: 7,415
  Likes Received: 2,845
  Trophy Points: 280
  Kwanza niseme kuwa Gwajima hajawahi kumfufua mtu, na kama aliwahi kudai hivyo atakuwa muongo mkubwa.Gwajima hajawahi kumponya kilema na kama anadai hivyo ni muongo mkubwa.
  Mwenye uthibitisho atoe humu. halafu nitakuja na ukweli.
   
 7. c

  chifu77 JF-Expert Member

  #1146
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 2, 2014
  Messages: 911
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 180
  Mkuu kumbe kuna baadhi ya mada upo shallow sana, jitahidi kujikita zaidi kwenye mada ambazo una uelewa mpana. Hii ya kumwita gwajima nabii wa uwongo umepotoka na utaishia kushusha heshima yako.

  Unadai gwaji kamwita 'huyu kiumbe'. Kumbuka Yesu alimwambia petro "rudi nyuma shetani".. huyo ni Yesu anamuita Mtume petro shetani kwa wakati huo. Leo gwaji kasema huyu kiumbe unashangaa nini.

  Pia, kumbuka Martin Luther King alikuwa Askofu na bado alipambana dhidi ya uonevu, manyanyasa na ubaguzi na alishinda. Askofu Desmond Tutu wa afrika kusini naye alikuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanyonge.

  Hakuna tatizo kwa gwajii kuumbua mtu mwenye cheti feki au anayetumia cheti cha mtu mwingine. angalia sasa anayoyafanya huyo Rc ya kuvamia wanahabari. Na bado unathubutu kumtetea. Ajabu sana.

  Nakukumbusha, sio lazima uandike kila kitu. Dili na yale machache unayoyajua na kuyaweza. Ya kolomije waachie wengine.
   
 8. p

  pilipili kichaa JF-Expert Member

  #1147
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 3, 2013
  Messages: 7,415
  Likes Received: 2,845
  Trophy Points: 280
  Ni kiumbe ndio na wote sie ni viumbe! kumbe ni nani ndugu? tena likitumika makanisani ndo mahali pake, japo sina hakika kama lile la Gwajima ni kanisa! nahisi hao jamaa wanasali kwa Gwajima na sio kanisani
   
 9. eddy mhando

  eddy mhando JF-Expert Member

  #1148
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 25, 2014
  Messages: 1,728
  Likes Received: 1,469
  Trophy Points: 280
  AISEEE...tatizo wazee wetu wameturithisha...hayo....wametufanya tunakosa ujasiri wa kuthubutu...maana enzi hizo tulikatazwa tusi wakosoe watu wazima...
   
 10. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #1149
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,718
  Likes Received: 30,983
  Trophy Points: 280
  kabisa laikini si jambo nzuri
   
 11. k

  kiatu kipya JF-Expert Member

  #1150
  Mar 20, 2017
  Joined: Dec 4, 2016
  Messages: 3,296
  Likes Received: 1,917
  Trophy Points: 280
  Hakika tutarudi mavumbini pia unatakiwa kuzielewa tabia za watu ,wanasema tabia ni kama ngozi huwezi ikimbia ni vyema kuskiliza Maneno na kuheshimu maamuzi ya mtu
   
 12. ILAN RAMON

  ILAN RAMON JF-Expert Member

  #1151
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 6,598
  Likes Received: 1,537
  Trophy Points: 280
  Magufuli na makonda wanafanana
   
 13. mirror01

  mirror01 JF-Expert Member

  #1152
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 682
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 80
   
 14. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #1153
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,635
  Likes Received: 2,287
  Trophy Points: 280
  Paskali umesoma kweli uandishi wa habari?
  Kwa nini unamtetea mtu ambaye ana elements za uharifu?
   
 15. djzm70

  djzm70 JF-Expert Member

  #1154
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 16, 2014
  Messages: 4,123
  Likes Received: 1,891
  Trophy Points: 280
  Gwajima ni nani kwanza

  Sent from my CAM-L21 using JamiiForums mobile app
   
 16. God iz bae

  God iz bae JF-Expert Member

  #1155
  Mar 21, 2017
  Joined: Mar 19, 2017
  Messages: 524
  Likes Received: 1,027
  Trophy Points: 180
  Mkuu, ni kweli humjui?
   
 17. J

  Jenerali Ambamba JF-Expert Member

  #1156
  Mar 21, 2017
  Joined: Sep 8, 2014
  Messages: 3,314
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Nimevumilia sana lakini sasa nimechoka, yaan ni wiki ya tatu sasa kila nikienda kanisani kusikiliza neno la Mungu katika Kanisa la Ufufuo na uzima ila baada ya kusikiliza neno la Mungu nasikiliza majungu, umbeya na udaku wa mtu anayeitwa Bashite, halafu muda wa sadaka ukifika naambiwa tutoe sadaka, sitakubali tena jumapili hii kufanya hili swala, nitatoa sadaka kama nitasikiliza neno la Mungu mwanzo mwisho, sio majungu, yaan mtu anahubiri majungu tu kila jumapili? sasa, sijui neno la Mungu tutaanza kuhubiriwa lini?


  Naomba sana mchungaji husika, jumapili uhubiri neno la Mungu, tunataka kusikiliza neno la Mungu, au basi ongelea Bashite huku ukihusianisha na neno la Mungu na biblia.
   
 18. Shindu Namwaka

  Shindu Namwaka JF-Expert Member

  #1157
  Mar 21, 2017
  Joined: Sep 22, 2014
  Messages: 4,825
  Likes Received: 2,936
  Trophy Points: 280
  Unaonaje Ukianzisha Kanisa Lako?
   
 19. Econometrician

  Econometrician JF-Expert Member

  #1158
  Mar 21, 2017
  Joined: Oct 25, 2013
  Messages: 8,534
  Likes Received: 7,683
  Trophy Points: 280
  Unataka kuongoza na huna vyeti-what do you expect
   
 20. dlnobby

  dlnobby JF-Expert Member

  #1159
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 30, 2014
  Messages: 2,178
  Likes Received: 2,350
  Trophy Points: 280
  Vyeti vinawatesa si mtoe tu jaman
   
 21. Laface77

  Laface77 JF-Expert Member

  #1160
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 1,403
  Likes Received: 1,521
  Trophy Points: 280
  Nafikiri wewe usije tu kimyakimya na wala usitoe sadaka. Tulio wengi tutaenda na tutatoa sadaka! Nakuhakikishia Jumapili ijayo tutakuwa wengi zaidi kuliko Jumapili iliyopita.

  Halafu nina uhakika kama unatoa sadaka kubwa sana basi unatoa TZS 10,000/- ambayo si kitu kwa mtu anayemiliki Helicopter! You can as well die and go to hell, bado sisi tutakuwa church pale Ufufuo na Uzima tukiendelea na ibada while your a***ss is burning in hell!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...