Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 27, 2017.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,715
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
  Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

  Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
  Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

  Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

  Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tuu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajima kuwa anajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, sio Mkuu wa Mkoa, Makonda, bali ni muumini wake mtiifu, ambaye nimemtaja hapa chini na alichokisema!, sasa kosa la Makonda ni lipi?!.

  Jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alivyotufundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto, mgeuzie na la kuume!. Yesu ametufundisha "adui mpende". Yesu ametufundisha "samehe hata saba mara sabini". Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo?! .
  Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
  Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
  Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
  Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
  Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.
  Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.

  Jumatatu Njema.
  Paskali
   
 2. MUSSA ALLAN

  MUSSA ALLAN JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2017
  Joined: Oct 13, 2013
  Messages: 18,960
  Likes Received: 7,722
  Trophy Points: 280
  Nadhani anayo matokeo ya shule aliyosoma BASHITE akapata zero, Pamoja na vyeti vya MAKONDA.

  Hawa ni watu wawili tofauti.
   
 3. Askari Muoga

  Askari Muoga JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2017
  Joined: Oct 22, 2015
  Messages: 6,057
  Likes Received: 4,461
  Trophy Points: 280
  Ni kweli utumishi wa Mungu ni zaidi ya Rais
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,715
  Trophy Points: 280
  Hajasema ana matokeo, amesema ana vyeti mezani kwake, hivi kweli kuna cheti cha divisheni 0 ya miaka hiyo?.

  Paskali
   
 5. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2017
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  Ile pikipiki yako ambayo ipo "moja" tu Tanzania nzima umeshaitengeneza??!!!
   
 6. Castr

  Castr JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2017
  Joined: Apr 5, 2014
  Messages: 7,896
  Likes Received: 13,086
  Trophy Points: 280
  Binadamu ni kiumbe, tunaposema kiumbe hai hatujatenga kua digidigi na kicheche ndiyo wanastahili jina kiumbe.

  Zamani hata mtu akifeli alipata cheti lakini hata result slip itaonesha matokeo pia, pengine ana result slip.

  Imeandikwa kua 'Ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga' kama maisha yako unayaendesha kinafiki subiri ukutane na wanafiki wenzako.
   
 7. Askari Muoga

  Askari Muoga JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2017
  Joined: Oct 22, 2015
  Messages: 6,057
  Likes Received: 4,461
  Trophy Points: 280
  ujue ww paska may all a sijui ndio kundi LA waandishi vipanga sasa unauliza Gwajima kasema yeye ni zaidi ya Raise harafu unatuuliza ni uongo
   
 8. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2017
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,676
  Likes Received: 2,752
  Trophy Points: 280
  YANI UMAJITAHIDI KABISA SIJUI KWA KUSUDI GANI KUTETEA VITU USIVYOKUWA NA USHAHIDI NAVYO. KAMA GWAJIMA ANASEMA UONGO WAKAMSHTAKI. HAYO YA UNABII WA UONGO MI HAYANIHUSU MAANA SIJAAMBIWA NIMEAMBIWA NISIHUKUMU.
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2017
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 26,520
  Likes Received: 13,980
  Trophy Points: 280
  ndio
   
 10. Castr

  Castr JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2017
  Joined: Apr 5, 2014
  Messages: 7,896
  Likes Received: 13,086
  Trophy Points: 280
  Kwa uongozi wa nyakati hizi, Kama hiki kitu alichosema Gwajima ni uongo, tarajia kusikia kesi ya kumdhalilisha mkuu au kuwekwa ndani saa 48 usiposikia hivyo jua kua kilichosemwa ni legit.
   
 11. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2017
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,881
  Likes Received: 2,616
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona Lowassa na Maalim Seif wanaulilia sana urais? Kwa nini wasiwe wachungaji?
   
 12. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #12
  Feb 27, 2017
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,515
  Likes Received: 899
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani amuite Mkuu wa Mkoa kiumbe...ni kosa kubwa sana
   
 13. S

  Swelana JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2017
  Joined: Sep 24, 2016
  Messages: 236
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 180
  Aisee kumbe wengine mmesoma kw kukariri,kwani akiwa na result slip si ni cheti pia?
  Nyinyi mnawajua watumishi wote wanaosali kwa gwajima je kama wamempelekea ushahidi huo wa kuprint hata kama ni document sio cheti?pascally wewe nina wasi wasi utakuwa ni mhanga kama daudi bashite.
   
 14. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2017
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,491
  Likes Received: 3,791
  Trophy Points: 280
  Nimegundua kitu, kwenye mahubiri yake anatumia jina la Mh rais kama ngao. kama vile anampamba, lakini anakua anam-snich.

  Hapo hajamtaja kwa jina, ili akijakuulizwa aseme hakumtaja makonda
   
 15. fakalava

  fakalava JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2017
  Joined: Jul 16, 2015
  Messages: 4,238
  Likes Received: 5,391
  Trophy Points: 280
  Kuhubiri neno ni pamoja na kukemea Maovu.
   
 16. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2017
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,122
  Likes Received: 45,930
  Trophy Points: 280
  Daudi Bashite
   
 17. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2017
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,122
  Likes Received: 45,930
  Trophy Points: 280
  Kwani sio kiumbe?
   
 18. c

  chotera JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2017
  Joined: May 19, 2016
  Messages: 1,108
  Likes Received: 1,565
  Trophy Points: 280
  Nchi hii ni ngumu sana , nilikua najiuliza kwa nini Kagame anaseaze watu kumbe ni watu kama gwajima na halafu amemnanga Raisi kiujanja ujanja kua hatompiga rais lakini atampiga makonda.
   
 19. Denis denny

  Denis denny JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2017
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 5,748
  Likes Received: 7,547
  Trophy Points: 280
  Safari hii mliopewa hela mmsafishe Makonda mtaumbuka sana.
  Gwajima huwa anapiga panapouma siku zote na aliyepigwa huwa haachi kuweweseka
   
 20. I

  IFRS JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2017
  Joined: Dec 19, 2014
  Messages: 1,722
  Likes Received: 1,059
  Trophy Points: 280
  Ni rahisi sana muumini wa kawaida kuingia mbinguni kuliko mchungaji kuingia mbinguni. Trust me
   
Loading...