Habari kwenu wanajamiiforus!
Awali yote napenda niseme kuwa Mimi ni Miongoni mwa watu ambao bado wanamkubali na kumuunga mkono Ndugu Rais Magufuli na nasema hili ili ieleweke kuwa sio tu wale wanaotizamwa kama hawamkubali Rais ndio wanaotafakari na kufurahi Haki na usawa ukitamalaki, leo na mimi nimeona niandike kuhusiana na suala la Vyeti feki, na hoja ya mtumishi wa umma kuwa amevunja sheria na bado akiwa Kazini.
Hoja yangu ni kuhusu namna Serikali inavyolichukulia suala la hoja ya mkuu Wa mkoa wa Dar Es Salaam kuwa alitumia cheti cha mtu cha kidato cha nne, Masikitiko yangu makubwa ni kuwa:-
1. Rais amekuwa siku zote ni mtu wa maamuzi ya haraka na kwa wakati, lakini katika hili amechelewa sana sana kulichukulia uamuzi unaostahili, watumishi wengi sana sana waliacha kazi na wengine kukamatwa kwa kutumia vyeti feki na Kwa sasa wanashangaa kuona kwa nini Rais na Viongozi wengine sio wakali na kujiuliza kama Serikali huangalia vyeo katika kufanya maamuzi.
http://m.ippmedia.com/sw/habari/kiama-wenye-vyeti-kuwa-mwezi-huu
2. Kuanza kuzuka kwa taarifa mbalimbali kuhusu kutumika kwa jeshi la polisi katika kuadhibiti watu au mtu anayeonekana kutaka kuonyesha unaodaiwa kuwa ni ukweli kuhusu vyeti vya Mkuu Wa mkoa wa Dar Es Salaam, kitu ambacho kimeanza au kitaanza kuichafua Serikali na taasisi zake.
3. Kuanza kudharaulika kwa taasisi ambazo huhusika na kutafuta, kuchakata na kutoa taarifa kuhusiana na mtu anayeweza kuwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.
4. Kuibuka hisia za ukabila na ukanda kwa watu wanaotajwa yaani mamlaka ya kuteua na kuteuliwa kwa kuwa ni wa kabila na ukanda mmoja, Jambo hili limeanza kuhuzunisha watu na hata wengine wanaona kama ndio sababu ya mamlaka kuchelea kufanya maamuzi kwa wakati.
5. Kuibuka kwa hoja ya kupuuzwa kwa Wapiga kura na wananchi ambao Rais amekua akisema wamemtuma kuwafanzia kazi, Mamlaka imeonwa imekuwa nzito sana sana.
Kwa hoja hizo za masikitiko yangu napenda kuiomba mamlaka ya uteuzi kutosita na kuona kuwa labda ikichukua hatua za kuhusu vyeti itadharauliwa na watoa hoja, nikimaliziamalizia napenda kuisisitiza Sana Serikali ichukue hatua za kumsimamisha kazi mkuu huyo wa mkoa ili uchunguzi ufanyike(utaratibu wa kawaida).lakini pia wale watafutaji na wachakataji wa taarifa wasione aibu labda ya kuonekana labda hawakuchakata na kuchunguza vizuri kuhusu Ndugu tajwa na huwenda labda walitajiwa tuu na marehemu wakaona anafaa bila hata ya kujiridhisha. Kwa sasa nawashauri wachukue hatua kulingana Sheria.
Mkuu wa mkoa pisha uchunguzi uheshimike na Serikali ionekane haiangalii vyeo katika maamuzi.
Wako katika hapa kazi tu.
Hmjamii