Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Uwakiki ulikuwa kwa walimu tu na manesi hao ndowalikiona chamtemakuni wamehakiki zaidi ya maranne watu waliacha kazi ndani ya masaa 24 wengine wamekula kona kimya kimya ilikuwa zaidi ya noma.hao wauko juu hawakuguswa
Waambie hao.Na tunataka ma RC nao uhakiki ufanyike
 
akifungua kesi itabidi aje na ushaidi wa kuonesha yeye si daudi bashite
 
Na Bashite aliyetangaza kupitia Live TV Coverage kwamba Gwajima anajihusisha na dawa za kulevya kwako wewe ni sawa sio?! Au unadhani kwavile yeye ni RC ndo ana haki ya kuchafua watu hadharani kupitia Live TV Coverage?!!

Wangapi amewataja kwamba wanauza unga wakati hana ushahidi wowote?! Wangekuwa baba zako wale, au mama zako, au kaka zako au dada zako ungefurahia kuchafuliwa hadharani?!!

Shame on y'all !!!
Na huu ndo ukweli. Et anataja majina hovyo tu wakati hana ushahidi.
Safi Gwajima na NECTA wawajibike na wizara pia.
 
Mchungaji Dr.Josephat Gwajima, leo kanisani kwake mbele ya umati wa waumini akiwaita wanafamilia wake, ametoa maelezo yakinifu juu ya tuhuma zinazomkabili ndg. Paul Makonda na katika clip inayosambaa kwa kasi mitandaoni.

Askofu Gwajima amedai anaoushahidi wa kutosha kua ndg. Makonda alitumia vyeti visivyo vyake.

Katika clip hiyo mchungaji Gwajima amesema ana vyeti vinavyotoa ushahidi kua Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine.

Swali: Je, Rais atamwacha Makonda na kulifumbia macho hilo suala?



=======

PAUL MAKONDA:

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).

18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.

Why amshitaki si aweke vyeti vyake kuondoa huu uzushi? Gwajima huenda alimaanisha anamatokeo yake sio vyeti so why waste time and resources kumshitaki Gwajima badala ya kuonyesha vyeti and clear the bad wind
 
Hakuna mtu ambaye hajuwi kuwa pili pili inawsha hawezi jimwagia maji ya pili pili machoni akifungua kesi ndio kajimaliza!
 
Mnataka walio na ushahidi kuwa mh. Paul Makonda hajatumia vyeti wa mtu,,mmesahau kuwa ni punde tu tulihakikiwa vyeti vyetu tena mara kadhaa na vyombo mbalimbali vya serikali bila mtu ushahidi wowote kutoka kwa raia?
Mmesahau kuwa Paul Makonda ni mtumishi wa umma na kwamba na yeye alishahakikiwa vyeti vyake? Kama mnakumbuka,sasa badala ya kutaka kumsaidia kuchepusha mjadala,kwanini nguvu hizo hamzielekezi kwa taasisi za serikali zenye majibu ya uhakiki wa vyeti vyake? Au mnataka kutuambia kuwa ule uhakiki ulikuwa kwa watumishi flani flani pekee?
Mods,mkiona vema msiunganishe uzi huu maana una dhima tofauti.
cc.Nyani Ngabu na Paskali Mayalla

Mbona Mimi huku simiyu ni mteule ila sikufikiwa uhakiki
 
Namuona NNappee akiwa mkuu wa mkoa wa DDaarr na baadaye afisa tawala wa mkoa wa maeneo ya katavi.
 
Baada ya kusikiliza sauti ya Baba akiongea na wanawe. Alizungumzia juu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda na akadai amefoji VYETI na jina Hilo si la kweka. Katika Hilo sina la kusema.

Turudi kwa MCHUNGAJI kwa kumbukumbu zangu, mchungaji ni mkaz wa Mwanza na nilianza kumfahamu pale alipomtusi Cardinal Pengo. Nilifatilia zaidi nikagundua kuwa naye alisoma pamba sekondari na alikua kiongoz wa ukwata na form four pia alipata *** kama anabisha alete cheti hadharani na ndalichako ahakiki.
Muhimu::: TUNAOMBA VYETI VYAKO MCHUNGAJI


Kweli ndugu Wanga, mtu akilaumu na yeye atalaumiwa, akihukumu na yeye atahukumiwa. Makonda yeye alishughulikia madawa ya kulevya na sasa watu wanamsakama kwa yanayodaiwa kuwa ni kasoro katika vyeti vyake. Hivi asingesema neno juu ya madawa ya kulevya haya tungeyasikia? Kwa hiyo viongozi wetu wafumbe vinywa vyao waache kuufanya uongozi kwa kuwa wakisema neno nao watasemwa? Makonda angekuwa anatumia madwa ya kulevya ingeeleweka kama watu wangemshutumu kwa shughuli hiyo? Lakini hatuna habari kama anatumia. Hata kama hana vyeti sahihi (mimi sijui ukweli upo wapi), basi asihukumiwe kwa sababu alijaribu kusema kitu juu ya madawa ya kulevya na hatima ya vijana wetu nchini.

Mr. Wanga umechukua mkondo unaofaa kurekebisha mtiriririko wa shutuma kwa Ndugu Makonda. Nimekuelewa kuwa unataka watu wanaomlaumu wawe "fair". Ni kama umewauliza hao wanaomtuhumu kuhusu vyeti vyao wenyewe vikoje? Hata kama vyeti vya mtu ni vizuri lakini sijui kama ni sawa kuvishambulia vyeti vya mtu mwingine kwa kuwa tu amesema kitu juu ya madawa ya kulevya. Ikiwa mheshimiwa atavitoa vyeti nadhifu vya taaluma zake hawa wanaosema sana watakuwa na lililobaki la kusema?

Nakumbuka shauri la Rais mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama alivomaliza kejeli za kuzaliwa kwake baada ya kutoa cheti sahihi cha kuthibitisha kuwa yeye alizaliwa Marekani; na ni Mmarekani kwa maana hiyo na hivyo kustahili kuwa Rais wa Marekani. Utendaji wa Obama leo unalinganishwa na ule wa mkosoaji wake mkuu Mhe. Donald Trump (Rais wa sasa wa Marekani) na unaonekana ulikuwa bora hadi kipindi hiki pamoja na kushutumiwa juu ya cheti chake cha kuzaliwa. Nisingependa kumsisitiza Mhe Makonda kutoa vyeti vyake vinavyozungumziwa, hiyo itakuwa ni kuicheza ngoma ya wakosoaji wake. Yeye achape kazi kwani anajua ni nani alimweka hapo na kwamba mpaka anaipata nafasi hiyo utaratibu unaotakiwa ulifuatwa.
 
Kwa haya yanayoendelea kati ya mh Paul Makonda na Mchungaji Gwajima ni dhahiri shairi ni udhalilishaji na kuchafuliana majina tu!

Kitendo cha Gwajima kuzusha habari za kumchafua mkuu wa mkoa ukweli si nzuri na hii kosa kabisa

Hivyo namshauri mkuu Makonda achukue hatua zaidi alifikishe hili kwenye sheria, ili Gwajima apishe faini!
Hii ni udharilishaji hasa kwa mtu mkubwa kama Rc wa Dar es salaam!
3323477e79f3110effa8ce31b85ff4cb.jpg
fb2d38dd921d6c3704e5c4dcaab2aac2.jpg
243f00494f311413b12f008c26140baf.jpg
 
Wahenga walinena "Ngoma ikivuma sana haikawii kup

...ka".Hayo ni malipo yake
 
Duh, kweli anaemaliza ndie huonekana Mbaya, yeye alipochafuliwa ulileta uzi humu?

Hata hivyo nafurahi hawezi kwenda mahakamani maana hii issue ni nzito kuliko kawaida, ngoja wageni wawasili kanisani juma 5.
Sababu ya police kuzingira nyumba ya Gwajima leo.
 
Bashite kajisahau anajiona na yeye kawa mtoto wa Dasalamu kwa kula chipsi kuku. Kumbe wana kijiji wenziwe akina Gwajima wanamjua dadeki zake.


Ndukiiiii
 
Back
Top Bottom