Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Wanasiasa si wa kuamini bila uthibitisho,kuna watu waliwahi kumchafua lowasa hadi tukawaamini wakamkosesha ikulu...sasa wanaona aibu hata kumuomba msamaha.
 
Daudi Bashite Hakusoma UDSM Mkuu. Alisoma MUCCOBS ambapo inasemekana alidisco mara tatu na baadae akatoka na cheti kwahiyo kuna uwezekano chuo cha MUCCOBS walimuuzia Paul Makonda cheti cha degree. haiwezekani mtu adisco mara tatu katika chuo hicho hicho baadae eti anatoka na cheti cha kumaliza masomo. Huyu daudi alishajijengea tabia ya kufoji elimu.
 
Light kama angekuwa wa chadema nakwambia angeshahukumiwa. Ila nakwambia hata watetee Ila Makonda hana sifa tena za kuwa mkuu wa mkoa wa dar. atasema nn sasa mbele ya wasomi.
 
Tatizo hakuna ushahidi juu ya hayo mnayotulazimisha tuyaamini,kama haujui siasa ni mchezo mchafu sana,ili tuamini hayo madai yenu tuleteeni huyo aliyemuuzia vyeti kuthibitisha vinginevyo ni hila tu na chuki zisizo za msingi.
Sasa hapo ndio bwana makonda anatakiwa atoke kifua mbele na vyeti vyake halali kuanzia kile cha kuzaliwa hadi cha ubatizo na kuwaziba midomo hao wenye chuki nao..

Mbona ni kazi rahisi sana, tena mji utanyamaza kimyaa kwa aibu!

Sio kwenda kulia kanisani
 
Tupo kwenye vita ya madawa.mtuache kwanza.na madai yenu ya vyeti ebo?
 
Nikakumbuka wimbo "Jambo gani lililo gumu la kumshinda Mungu baba" Jambo gani rahisi kati ya kulia na kuonyesha vyeti?
 
Yaani ndio hapo, habari moto kama hii

Mimi ningekuwa hao wanaomsingizia, ningesaka habari nipige pesa ndefu sana juu yake. Na ilivyo na wa madawa etc

Yaani ndefu hadi ningejenga mjengo wa maofisi mjini, tena na hivi ni habari moto la hasha cocochanel mngenijua sura yangu kwa kuniona lwa kumaliza utata ambao ni historia nchini.

Makonda oyeeeeeee
 
Hao hao wana ccm wanasema tuangalie utendaji wake sio makaratasi. Pumbavu ingekuwa hivyo msinge wafukuza wanafunzi na msinge komaa na ukaguzi miaka mi2 bila kulipa wafanyakazi stahiki zao na kutoa ajira kwa watu mlowasomesha
Mwanasisiemu ni popo.... Likigusa kwake anatetea likigusa kwingine anakomalia.
Sawa bashite ana maisha yake mazuri na yule ni msukuma anapenda uongozi kama kweli ana uchaji wa Mungu asingefanya hayo. Direct angetoa tuu vyeti mambo yaishe.
 
Kinachomsaidia tuu Makonda ni ofisi kuu Magogoni kwani anakubalika huko na mwamvuli unamkinga. Ingekuwa hayo yako kwa Simbachawene au mwingine ambaye hana upepo mzuri na muzee, zamaaaani tungesha sahau single hii
 
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia...
 
Tatizo hakuna ushahidi juu ya hayo mnayotulazimisha tuyaamini,kama haujui siasa ni mchezo mchafu sana,ili tuamini hayo madai yenu tuleteeni huyo aliyemuuzia vyeti kuthibitisha vinginevyo ni hila tu na chuki zisizo za msingi.
Ushahidi umewekwa kama mhusika anaona anachafuliwa ashitaki wanaomchafua, serikali ilipohakiki vyeti haikulazimika kutafuta wamiliki halali wa vyeti ilitafuta watu ambao wamejipachika sifa ambazo sio zao. Waziri wa Elimu ajiandae na swali hili la nyongeza juu ya uhalali wa vyeti na ninavyomjua atasimama kwenye ukweli, baadhi ya watu hutumia vyeti vya watu ambao wameshafariki hivyo sio rahisi kumpata mhusika kuja kutoa ushahidi nafikiri hata ushahidi mwingine unaweza kutumika kuthibitisha.
 
Mkuu hebu rejea nyuma na kuangalia viongozi wote waliotuumiwa kwa kesi kama hivi walitoa ushahidi wao?, mm nadhani hili litaisha kama kwa wengine wa awali ambao waliandikwa kwenye kitabu cha "mafisadi wa elimu' au wengineo wa juzi juzi hapa
 
Kama huyo mtuhumiwa hajakana mashitaka mpaka leo ni kwann hatua zingine zisitumike kama ambavyo nimependekeza ili kuumaliza huu utata na watanzania wote tukajua mbivu au mbichi juu ya hili swala.
 
Mjini shule,mwacheni ajifunze.Aliingia kichwa kichwa.
 
Shida siyo kukubali au kutokubali kuhusiana na swala. Issue iko hivi kama mshtakiwa hataki kutoa majibu sahihi ili kuweka mambo wazi ni kwann watu ambao wanaushaidi kuhusiana na swala hili wasijitokeze na kukitia kimbutua mchanga na watu wakajua?. Maana tukiendelea hivi mwisho wa siku naona itakuja kama kipindi kile cha " mafisadi wa elimu" ilivyokuwaga na hatukuwa na ushahidi kama ni kweli watu walichukua majina ya watu au la?
 
Mkuu wa mkoa anaweza kuwaita wanahabari muda wowote na wakafika..

Kwanini asiwaite ili awamwagie mavyeti yake yote ili kuwanyamazisha hao anaodhani ni wauza unga wanaomsakama?

Mbona ni rahisi tu? Nusu saa inatosha kuwaziba watu midomo na mji ukatulia kama maji katika chungu!
 
Daudi Bashite ana bahati Ben Saanane alishapotea.........
 
Hii movie itaisha vizuri pale bunge litakapomweka kitimoto na kuchambua makosa yake yote, na kumwachie rais aamue. Kwa sasa aachwe azunguke nyumba zote za ibada huku akilia kama alivyokuwa akiliza binadamu wenzake.
Mi sidhani kama bunge litajadili kuhusiana na swala la mtu kufoji vyeti maana itahitaji ushahidi wa kina ili kudhibitisha hili. Pia tukumbuke kama yeye ni kweli alifanya hilo swala basi kuna haja ya kuwafanyia uchunguzi mpaka wale wengine waliobadi na kukili kwa sababu nao watakuwa wamefanya makosa.
Pia na wale viongozi walitajwa kwenye kitabu cha "mafisadi wa elimu" nao wanapaswa kujadiliwa kama huyu jamaa.
 
Wadau

Nadhani nnakumbuka hadithi ya Charles Kitwanga na Kashfa ya Lugumi akiwa waziri wa mashauri ya ndani ya nchi.

Katika lile sakata Mh Rais alikuwa akisemewa kuwa hawezi kumtema ndugu yule kwa kuwa ni 'home boy' tena in classmate wake.....wengi waliumbuka kumuona Magufuli akimpiga chini rafiki yake aliyefanya kosa la ' kiufundi'.

Sasa kwa huyu Mkuu WA mkoa Daudi Bashite wengi mnamsemea Mh Rais kuwa atakaa kimya, hapana.

Bashite alipendwa kwa utendaji wake mzuri ila Magufuli hakujua yaliyotokea kwamba huyu MTU ana dosari.. hapa ndio Magu hujidhihirisha uzuri wake.. soon mtaniambia.

Kumbukeni sakata la Kihiyo.. Katibu mkuu wa CCM wakati huo Laurence Gama na Sekretarieti hawakujua fojari ya vyeti na hawakutaka kuingilia Uhuru WA mahakama kuzuia aibu ndani ya chama baadae.

Tafakari..Magufuli soon atajidhihirisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…