Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,180
- 138,474
Invisible na Mods wote tuseme ukweli huu uzi una mahusino gani na huku mlipouleta.Clouds Media kupitia kipindi cha Take One kilichokuwa kinaendeshwa na Zamaradi kiliwahi kuweka Video ya mahojiano ya Zamaradi na Wazazi wa Mh.Makonda katika mtandao wa You Tube........katika video hiyo ya You Tube moja kati ya wachangiaji katika video hiyo kwenye mtandao wa You Tube walikuwa Mahimana Joyce. Mama huyu ni mama yake mdogo wa Mh.Makonda. Katika comment yake kwenye video ya Clouds Media aliandika ''Barikiwa sana familia ya Bashite na pia dada Suzan pole sana Daangu. Mungu atukuzwe sana.kweli amekuinua''
Katika hali ya kushangaza Clouds Media Group ambao ndio walionweka video hiyo wamefuta ujumbe huo uliowekwa miezi nane iliyopita.
View attachment 477185
Wachangia wameilaumu Clouds kwa kufuta ujumbe huo kitendo kinachoamsha hasira katika kupambana na matumizi ya vyeti feki
Kwa maelezo zaidi tembelea You Tube
Kwani kuonyesha vyeti kunatumia dakika ngapi......si nusu dakika tuHii ni aibu ya karne...
Lijamaa linalia lia kinafiki tu!
Angekuwa na hivyo vyeti si angetoa tu yakaisha...
Daud Bashite!
Eti wanadai tunamuonea wivu, hata akiondoka wala hatuufikirii huo u-RC, sisi tunataka mtu mwaminifu aliye na vyeti vya kweli.Bashite must go.. tusiwe wajinga ndugu zangu watanzania
Nani amuonee wivu uyo ziro.. yani kweli shule inaumuhimu mkubwa sana kwa mtu.. angekuwa kapita shule angeweza kujitambua na kujua namna ya kuongoza.. kitendo cha kumpiga Warioba bado sielewi uyu dogo alikuwa na nini kwenye mawazo yake..Eti wanadai tunamuonea wivu, hata akiondoka wala hatuufikirii huo u-RC, sisi tunataka mtu mwaminifu aliye na vyeti vya kweli.
Si ndio hapo mkuu..Kwani kuonyesha vyeti kunatumia dakika ngapi......si nusu dakika tu
HUYU GWAJIMA MBONA ANA VISASI VYA KIJINGA ? TANGU ATAJWE KWENYE TUHUMA ZA UNGA KILA SIKU MAHUBILI YAKE, MAKONDA,MAKONDA!? VYETI,VYETI, UNABOA BWANAA !!Mchungaji Dr.Josephat Gwajima, leo kanisani kwake mbele ya umati wa waumini akiwaita wanafamilia wake, ametoa maelezo yakinifu juu ya tuhuma zinazomkabili ndg. Paul Makonda na katika clip inayosambaa kwa kasi mitandaoni.
Askofu Gwajima amedai anaoushahidi wa kutosha kua ndg. Makonda alitumia vyeti visivyo vyake.
Katika clip hiyo mchungaji Gwajima amesema ana vyeti vinavyotoa ushahidi kua Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine.
Swali: Je, Rais atamwacha Makonda na kulifumbia macho hilo suala?
=======
PAUL MAKONDA:
1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite
3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.
4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).
5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.
6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.
7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).
8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.
9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.
10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.
11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.
12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.
13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).
14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).
15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.
16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.
17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).
18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite
19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.
20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
Pambafuwewe mbuzi tu tena unafaa kwa mchuzi
Wewe huna kaziKwa mtazamo wangu yafuatayo yanaweza kuwa madhara ya kufumbia maccho jambo hili.
1.Waliokuwa wamebakiza imani ndogo kwa Mkuu wa Kaya sasa wamebakiza imani "zero" kwake
2.Waliokuwa bado wanamuamini sasa imani yao kwake nayo imeanza kushuka
3.Imani ya wananchi kwa chama tawala inazidi kushuka
4.Chama tawala kitapoteza viti vingi vya ubunge hasa katika jiji la Dar-es-laama na majiji mengine makubwa ya nchi hii.
5.Zoezi zima la uhakiki limepoteza maana na limedharaulika.
6.Mazoezi mengine yoyote yatakayofuta watu watayadharau
7.Waliokuwa bado wanavutiwa na hotuba zake sasa wataacha kumsikiliza.
8.Ni mfano mbaya kwa wanafunzi walioko mashuleni.
9.Vijana wengi wataamini mafanikio katika maisha ni ujanja wako tu na kwamba kusoma sio issue.
10.Ukijuana na wakubwa wewe ni utouchable.
11.Baadhi ya vijana watakuwa insipired kufuata nyayo za RC huyu kufikia hapo alipo bila kujali hatari inayowakabili.
12.Baadhi ya watu hawatakuwa comfortable kuumpa mtuhumiwa heshima yake kama kiongozi na wengine hawatajisikia amani kuhudumiwa na mtuhumiwa.
13Mthumiwa nae hatakuwa comfortable kupokea heshima anayopewa na atajihisi hastahili tena heshima hiyo.
14.Hadhi ya jiji husika na watu wake kushuka thamani.
15.Mtuhumiwa kujihisi kusemwa na kila mtu hasa pale anapoona watu walio karibu yake au anaofanya nao kazi ofisi moja wanapiga story katika vikundi na hata wawapo maofisini...
16.Athari za kisaikolojia kwa muhusika katika siku za baadae.
17.Ajenda na turufu ya upinzani mwaka 2020
This is more than serious !!!!Gazeti la MwanaHALISI kumuanika Paul Makonda
Nyumba aliyokulia Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (Daudi Bashite)
KILA pembe ya kijiji cha Koromije, Wilaya ya Misungwi, pamoja na viunga vya jiji la Mwanza Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anatajwa na kufahamika kama Daudi Albert Bashite, wanaandika Waandishi Wetu.
Wanaomtaja kwa jina hilo ni wanakijiji, ndugu zake, wanafunzi aliowahi kusoma nao pamoja na watu waliowahi kumshuhudia akifanya kazi kama kondakta.
Gazeti la MwanaHALISI baada ya uchunguzi wake wa kina uliohusishwa kutuma timu ya maripota wake jijini Mwanza, wanakuletea habari kamili inayofichua ukweli wa sakata hilo huku mama na baba wa Makonda, shangazi yake na wanafunzi waliowahi kusoma naye wakiwa wamehojiwa.
Shule ya Msingi aliyosoma Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Chanzo: Mwanahalisi