Kwa mtazamo wangu yafuatayo yanaweza kuwa madhara ya kufumbia maccho jambo hili.
1.Waliokuwa wamebakiza imani ndogo kwa Mkuu wa Kaya sasa wamebakiza imani "zero" kwake
2.Waliokuwa bado wanamuamini sasa imani yao kwake nayo imeanza kushuka
3.Imani ya wananchi kwa chama tawala inazidi kushuka
4.Chama tawala kitapoteza viti vingi vya ubunge hasa katika jiji la Dar-es-laama na majiji mengine makubwa ya nchi hii.
5.Zoezi zima la uhakiki limepoteza maana na limedharaulika.
6.Mazoezi mengine yoyote yatakayofuta watu watayadharau
7.Waliokuwa bado wanavutiwa na hotuba zake sasa wataacha kumsikiliza.
8.Ni mfano mbaya kwa wanafunzi walioko mashuleni.
9.Vijana wengi wataamini mafanikio katika maisha ni ujanja wako tu na kwamba kusoma sio issue.
10.Ukijuana na wakubwa wewe ni utouchable.
11.Baadhi ya vijana watakuwa insipired kufuata nyayo za RC huyu kufikia hapo alipo bila kujali hatari inayowakabili.
12.Baadhi ya watu hawatakuwa comfortable kuumpa mtuhumiwa heshima yake kama kiongozi na wengine hawatajisikia amani kuhudumiwa na mtuhumiwa.
13Mthumiwa nae hatakuwa comfortable kupokea heshima anayopewa na atajihisi hastahili tena heshima hiyo.
14.Hadhi ya jiji husika na watu wake kushuka thamani.
15.Mtuhumiwa kujihisi kusemwa na kila mtu hasa pale anapoona watu walio karibu yake au anaofanya nao kazi ofisi moja wanapiga story katika vikundi na hata wawapo maofisini...
16.Athari za kisaikolojia kwa muhusika katika siku za baadae.
17.Ajenda na turufu ya upinzani mwaka 2020