Mchungaji Gwajima acha kupotosha, huwezi sema Maalim Seif muda wake wa kuishi umetosha, binadamu anaweza kuishi miaka zaidi ya 100

field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
771
1,000
Nimesikiliza clip ya Mchungaji Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima akijaribu kuhalalisha kifo cha makamu wa pili wa rais wa Zanzibar kuwa ameshafika miaka 70 hivyo hata akifa ni sawa kwa sababu binadamu tuliumbwa kuishi miaka 70.

Naomba nimfahamishe huyo Gwajima ambaye binafsi siamini kama ni mchungaji kweli kutokana na matendo yake mabovu kwenye jamii na pia wizi wake wa kura uliompa ubunge feki, kuwa umri wa kuishi watu si miaka 70 tu, kwenye nchi zilizoendelea wastani wa kuishi ni miaka 84 au zaidi lakini kuna watu wakitunzwa vizuri wanafika miaka 100 kama alivyofikia babu yangu na bibi yangu miaka 96.

Gwajima huyu feki aliyedai anafufua wafu na asiyejua hata maana ya Covid-19, anasema ni Corona virus december 2019 ndiye anayetupangia nani afe au asife au anayeshabikia watu kufa wakiwa na umri wa miaka 70?

Ni aibu sana kwa huyo Gwajima aliyesambaza makaratasi kuwa watu wawamalize wanaompinga Magufuli na kutaka kueneza USUKUMA, it is shame to have this kind of imbecile church leader.

Scandal yake ya vijambo alivyofanya bado ipo mbichi anataka kuipotezea kwa kurukia rukia vitu vingine visivyomhusu.

Ushauri ahangaike na kanisa lake, hatuwezi kupangiwa miaka ya kuishi na huyo Gwajima, awe basi angalau na uwezo wa kufikiri sawasawa aache mihemuko, yeye anatukataza kuvaa masks ni nani nchi hii? Anawakataza waumini wake kuvaa masks je anajua athari za kutokuvaa masks?
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,766
2,000
Duh mkuu hili povu akilipata muumini wake huu uzi sijui tu

giphy.gif
 

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
933
1,000
Gwajima alikuwa sahihi. Kwa mujibu wa biblia binadamu kuishi ni miaka sabini.

Mtu unatakiwa kujiuliza swali hapa: Je,Maalim Seif angefariki tarehe ile kama Mungu hakupenda afariki?

Ajabu na wewe umehamia kwenye mipango badala ya kutoa hoja za maana.
 

field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
771
1,000
Ameambukizwa COVID-19 alivyokwenda Chattle, Hatuongozwi na hisia za watu. Asingepata Covid-19 asingekufa. Watu wanaishi miaka 100 wewe unaongea nini? Ali Hassan Mwinyi anayo miaka 94, wewe unatuambia miaka 75 na kitu ni mingi? EBU ACHA HIZO
 

donbeny

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
3,566
2,000
Askofu Gwajima ni tapeli ,kama ilivyo mzee wa upako na matapeli wengine wenye makanisa ya kitapeli wanakula sadaka na wake zao/mahawara huku waumini wao wakizidi kuwa wachovu hawa ni manabii wa uongo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom