Nini hatima ya kanisa la Mlima wa moto A.G baada ya Mama Getrude Lwakatare (Mchungaji na mbunge) kufariki dunia?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,681
2,000
Ni wengi ambao wangetaka kupata majibu yake lakini kidogo corona inawaweka busy..

Kiasili Mama Getrude sio Mhaya kama wengi wanavyodhani... Huyu ni Mpogoro wa Morogoro Ifakara huko... Mumewe ambaye pia ni marehemu ndio Mhaya wa Bukoba Kanyigo nadhani...

Kupanda kimafanikio kwa Mama Getrude kunaanzia miaka ile ya 2000 alipofungua shule ya kwanza ya mkondo wa kiingereza Tabata karibu na mawenzi akiwa na mshirika wake mmoja anayesemekana ni mnaija

Shule iliitwa St. Mary's English medium academy ikafanya vizuri na kupanuka kwa haraka hata kuwa na matawi... Huyu mnaija ndio alimpa connection ya Marekani ambapo alipewa mbinu ya kusema zaidi ya kuwa na shule lakini pia anajihusisha na watoto yatima ambao hawa husoma bure kwenye shule yake.

Wazungu wakahadaika na kummwagia fungu la maana ambapo alijenga shule kubwa huko huko Tabata bima nadhani

Ili kuwaaminisha wazungu akachukua kweli wachache na kuwaingiza kwenye shule yake.. Na akawa anawapiga picha pamoja na wanafunzi wengine na kuzituma ulaya... Kwa mbinu ya kwamba wote hao ni yatima.. Waliosoma St Mary's miaka ile ni mashuhuda wa hili

Shule zikachanganya sana kwakuwa tayari alikuwa na ufadhili wa wazungu lakini vile vile akaenda Kenya na kuwachukua Vijana wa Kikenya kibao ambao ni graduates. Hawa wakaletwa kufundisha lugha ya kiingereza na shule zikaongezeka na kupata mafanikio makubwa

Katikati ya mafanikio makubwa zikaanza skendo na tuhuma za Walimu wake kutokuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Walimu wake wengi kutokuwa na vigezo hafifu vya kuwa walimu. Wanafunzi kuwa na uwezo mdogo kwenye masomo mengine tuhuma za kuiba mitihani.

Siku ambayo serikali imejiandaa kwenda kufanya ambush mama akawa ameshatonywa na hivyo kuwakimbiza walimu wote Wakenya kwa mabus ya kukodi mpaka mpakani.. Ushahidi ukakosekana lakini shule zikayumba sana kwa sababu ya kudhibitiwa na serikali kwenye swala la ajira ya walimu

Hilo lilienda sambamba na wafadhili kupata taarifa kuwa yatima wanaowachangia kila wakati sehemu kubwa ni uongo hivyo wakakata kamba

Kipindi hicho ndio mama alipoona awekeze zaidi kwenye kituo chake cha maombi kilichokuja kuwa kanisa kubwa la Assemblies of God Mikocheni Mlima wa moto.

Huku kwenye kanisa ufuatiliaji wa serikali haukuwa mkubwa kama kwenye shule na hata running cost zilikuwa chini sana kulingananisha na kwenye elimu.


Income ya kanisa ikawa super na inayopatikana kwa wepesi kuliko kwenye shule zake... Hivyo akapunguza nguvu kwenye shule na kuwekeza zaidi kwenye dini.

Dini ikamkuza na kumfanya awe maarufu maradufu huku akiwa ni mmojawapo wa wafadhili na mwanachama matiifu wa CCM.. Hili lilimpelekea kupewa ubunge wa kuteuliwa.. Kwahiyo sasa akawa sio mama Getrude Mchungaji tuu bali na mheshimiwa mbunge pia... Akawa sasa ametimiza cycle ya msingi ya matamanio ya binadamu wengi

- Umaarufu
- Utajiri
- Heshima
- Fame, wealth and respect (status)

Sehemu ya pili
Kwenye maisha yake ya kutafuta alikuwa na nyakati ngumu pia na mojawapo kazi ya hizo ni kutengana na mumewe Mzee Lwakatare. Kugombana na mshirika wake kibiashara kwenye shule kusitishiwa misaada ya watoto yatima.

Kuzuiwa kuajiri walimu wageni. Kuingia kwenye kashfa ya kununua kiwanga cha Mangula Moro kilichokuwa na eneo kubwa sana na kubalidili matumizi yake huku mashine akiziuza chuma chakavu.

Umaarufu wa kanisa lake ukawavutia na matajiri wengine walioficha maovu yao kwa mlango wa dini... Mmoja wao ni mmiliki wa vituo vya mafuta vya Victoria service stations.. Huyu jamaa mwenye background isiyovutia sana hasa nchini Kenya alianzisha kanisa lake pale Victoria lakini baadae akaja akaunda ushirika na mama Getrude Lwakatare.. Na mara nyingi huonekana kwenye ibada za mlima wa moto kwenye vile vipi MUHIMU

Mama Mchungaji Getrude Lwakatare mbunge inasemekana ana mtoto mmoja wa kiume. Mama ni mjasiriamali na tunaweza kusema ni mwekezaji pia akiwa na vitega uchumi lukuki
Katika uwekezaji wake kuna

Shule za St Mary's

- Kuna kituo cha radio (sina hakika na TV online)
- Ana kanisa la Mlima wa moto
- Ana viwanja na ardhi sehemu tofauti tofauti
- Ana uwekezaji mwingine usiojulikana na wengi
- Sehemu kubwa ya uwekezaji wake kwa sasa ana shareholders lakini je vipi pale mlima wa moto alipokuwa amewekeza mpaka moyo wake?
Je, alikuwa na shirika na mtu/ watu wengine?

Je, huyo mtu/hao watu wana maono kama yake?
Je, nafasi ya wanae ni ipi pale mlima wa moto
Huko kwingine je.. Kaweka vizuri kwenye ishu za mikataba ya biashara, umiliki na mirathi?

Mlima wa moto ilikuwa ni taasisi binafsi je ni nani ataweza kuvaa viatu vya mama? Mtoto ataweza?
Mwisho wa yote tunabaki na swali moja muhimu.

Je, ni nini hatima ya kanisa la Mlima wa moto baada ya Mama Getrude Lwakatare mbunge na Mchungaji baada ya kufariki dunia?

Wakati utasema.. Si muda wa kuanza ramli chonganishi.

Jr

Jr
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,681
2,000
Sehemu ya pili
Kwenye maisha yake ya kutafuta alikuwa na nyakati ngumu pia na mojawapo kazi ya hizo ni
Kutengana na mumewe mzee Lwakatare.

Kugombana na mshirika wake kibiashara kwenye shule. Kusitishiwa misaada ya watoto yatima
Kuzuiwa kuajiri walimu wageni.

Kuingia kwenye kashfa ya kununua kiwanga cha Mangula Moro kilichokuwa na eneo kubwa sana na kubalidili matumizi yake huku mashine akiziuza chuma chakavu.

Umaarufu wa kanisa lake ukawavutia na matajiri wengine walioficha maovu yao kwa mlango wa dini... Mmoja wao ni mmiliki wa vituo vya mafuta vya Victoria service stations.. Huyu jamaa mwenye background isiyovutia sana hasa nchini Kenya alianzisha kanisa lake pale Victoria lakini baadae akaja akaunda ushirika na mama Getrude Lwakatare.. Na mara nyingi huonekana kwenye ibada za mlima wa moto kwenye vile vipi MUHIMU

Mama Mchungaji Getrude Lwakatare mbunge inasemekana ana mtoto mmoja wa kiume. Mama ni mjasiriamali na tunaweza kusema ni mwekezaji pia akiwa na vitega uchumi lukuki.

Katika uwekezaji wake kuna
Shule za St Mary's
Kuna kituo cha radio (sina hakika na TV online)
Ana kanisa la Mlima wa moto
Ana viwanja na ardhi sehemu tofauti tofauti
Ana uwekezaji mwingine usiojulikana na wengi
Sehemu kubwa ya uwekezaji wake kwa sasa ana shareholders lakini je vipi pale mlima wa moto alipokuwa amewekeza mpaka moyo wake?
Je alikuwa na shirika na mtu/ watu wengine?
Je huyo mtu/hao watu wana maono kama yake?
Je nafasi ya mwanae ni ipi pale mlima wa moto
Huko kwingine je.. Kaweka vizuri kwenye ishu za mikataba ya biashara, umiliki na mirathi?
Mlima wa moto ilikuwa ni taasisi binafsi je ni nani ataweza kuvaa viatu vya mama? Mtoto ataweza?
Mwisho wa yote tunabaki na swali moja muhimu
Je ninini hatima ya kanisa la Mlima wa moto baada ya Mama Getrude Lwakatare mbunge na Mchungaji baada ya kufariki dunia?
Wakati utasema.. Si muda wa kuanza ramli chonganishi

Jr
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,681
2,000
Kuna mwaka ndugu yetu alikuwa yatima . Akapata feva ya kusoma kwenye shule yake ya St. Mary's international school.
Alisoma mwaka mmoja akarudishwa nyumbani kwamba wazamini wamejitoa na kurudi shule za kawaida miaka 2004's.

Je hawa walitumika kama chambo ili apige mkwanja ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yatima hawakuwa wengi kama alivyowaambia wafadhili na sakata la walimu wa Kenya ndio lilifunua mengine yote

Jr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom