Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
Tuwekee video clip mkuu ili tuweze kutoa hukumu ya haki
 
mzee wa upako hatumii vile vitu vya kina chidi na TID kweli
 
Yeye ndio ana upako wa konyagi?angesema ni tapeli mwenzake.
 
Kama anataka pesa ahame nchi, ili wananchi wamfuate alipo.

Lazima ameongea hivi kwasababu anaona wengi wanaenda Nigeria.
 
Kwa hiyo yeye Lusekelo amekuwa Mungu!!? Maana amejipa jukumu la kuhukumu wengine. " Usihukumu usije ukahukumiwa" hii naona wengi imewapita pembeni!
 
Ukiskia mpigaji hataki wenzake wapige ndo hii, wote tapeli tu mtu mishi wa mungu anagonga maji wapi na wapi
 
Binafsi sioni tofauti kati ya Babu wa Loliondo na Tb Joshua kwa kuwa mungu wao ni mmoja wanayetumikia kwa tabiri zao na mengine
 
Hahahaaa.... Yeye mtumishi Wa Mungu kwann adiwataje hao Wa madawa ... Mkuu Wa mkoa asipate tabu kuishi???

Albino waliokuwa wanauawa kila kukicha alikuwa wapi??

Na hii njaa je?? Mbona hatoi unabii usio feki?

Sent from my HUAWEI Y360-U61 using JamiiForums mobile app
 
Moja kati ya watumishi wapuuzi ni huyu mzee wa upako na ninavyomuona imani yake ina shida kwa sababu katika kumtumikia Mungu swala linalo-matter ni imani kwa mfano mtu akija umuombe na ukamwombea asipone akaenda kwa mchungaji mwingine hiyo haikufanyi wewe kuamini kuwa Mungu hayupo, ukimuombea mtu akipona au asipone wewe endelea kuamini kuwa Mungu yupo. Sasa habari ya kutoa utabiri usio sahihi si kitu cha kumfanya Tb Joshua kutokuendelea kumtumikia Mungu. Hakuna mwanadamu aliyefanikiwa kum-exhaust Mungu kwa namna yeyote ile hata Musa licha kuongea naye na kumwona hakufanikiwa kujua tabia zake zote, mwisho Lusekelo elewa kuwa Mungu hana mwisho kama ni somo basi yeye ni somo endelevu sometime utatoa utabiri ambao Mungu mwenyewe anaupindisha ili uelewe kuwa akili zake hazichunguziki na uzidi kumtumainia na kumtafuta. Mhu 7:20 ”Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi”.mzee Lusekelo Mungu si sport sport kama unafikiri, kumbuka sikuzote nyumba haijengwi na kukamilika kwa kumtumia fundi mmoja huyu huyo ajenge msingi , kuta, apige bati, lip, apake rangi, aweke umeme, apitishe mabomba ya maji nk hiyo itakua siyo nyumba labda banda la kuku vivyo hivyo mwili wa Kristo hauiengwi na mchungaji, nabii, mhubiri mmoja lazima washirikiane kulingana na karama zao walizopewa na Mungu mwenyewe
 
KANISA NI MOJA,KANISA NI KATOLIKI,KANISA ASILI YAKE NI MITUME

Hili ni kati ya makanisa yaliyojaa mafundisho ya uongo na kuipotosha biblia ambalo ni neno lenye pumzi ya Mungu

Ni pm nikusaidie kwa kile kidogo nilichojaliwa na Mungu
 
Manabii wa uongo manabii wa uongo!!

Hao manabii wa ukweli wako wapi?kila siku tunasikia story za manabii wa uongo ila manabii wa ukweli hatuwasikii.
 
Wivu tu, hata kibongo bongo hakuna Muhubiri anayemkubali Mwenzake...kila mmoja anaamini Mwenzake kuwa na Wafuasi wengi ndio anapiga pesa zaidi...kwa hiyo roho inauma.
 
Back
Top Bottom