Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
.
Zakaria 13
.
2 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi, nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena; pia nitawafukuza manabii, na roho ya uchafu, watoke katika nchi.

3 Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la BWANA; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii.

4 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba manabii, kila mmoja wao, atayaonea haya maono yake atoapo unabii; wala hawatavaa joho ya nywele ili kudanganya watu;

5 bali atasema, Mimi si nabii kamwe; mimi ni mkulima wa nchi; kwa maana nalifanywa mtumwa tokea ujana wangu.
.
Ni kama dunia tumefikia siku hizo hapo juu. Yaani pia kwa maana kwamba kwa sababu ya kuongezeka maasi upendo wa wengi umepoa. Katika nyumba ya Bwana ndiko kwenye utapeli kushinda mahali pengine popote jambo lililopelekea nafsi za wenye haki kukata tamaa kabisa. Siku hizi mtu akijiita mtumishi wa Bwana watu wanageukiana na kutizamana, kwa ishara kwama 'wale wale...'
Ole, ole, ole!!
 
Hivi huyu mbona hadi leo hajatajwa au yupo kwenye list ya 3 ........
Unauza ngada unakunywa bapa huwezi kuwa mzima kichwani ....
 
Wewe mzee wa bapa na Tb Joshua wote matapeli, utofauti ni kwamba wewe ni tapeli local, mwenzako ni tapeli intaneshno
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
Woote mantanange
 
Ok. Huwa ninakuelewa Ila Boliti ndani ya Jicho lako mzee wa Upako umetoa? na hili lako la kwamba unapiga pombe na wengi wana mashaka hata muonekano wako ni kama wale wapiga bapa kubwa? sijaelewa siku hizi mzee ana matatizo ya macho? au anaficha kitu?
Ila kweli mkuu muonekano wake ni wa kitwanga
 
Hahaha, kweli hizi imani zitatufikisha pabaya. MIMI SIMUAMINI YEYOTE ANAYEJIITA NABII KARNE HII, FULL UTAPELI, MZEE WA UPAKO ANAVIMBA MACHO SAIVI SIJUI SHIDA NI KINYAGI AU NINI. NGOJA TUONE ALISEMA WALIOSEMA ANAKUYWA KONYAGI WATAKUFA MWEZI HUU.

Wizi mtupu.
 
Kiongozi mzuri wa kiroho hatukani viongozi wengine wa kiroho. Yeye hufundisha neno la Mungu kwa ufasaha ili watu wayakubali mafundisho yake. Kuponda na kutukana hata vichaa wanaweza.
Lusekelo amedhihilisha kwamba uwezo wake wa kuhubiri neno ni mdogo na huenda ameanza kupoteza waumini.
 
Back
Top Bottom