Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Waumini wezangu tusimame imara na madhehebu yetu..natumjue mungu muumba wetu atatuongoza katika imani zetu..wachungaji wengi sasaivi wapo kimaslahi
 
Basi usiseme madhabahu haichezewi ilhali hata wewe una mamlaka katika Kristo ya kuivunja madhabahu kama utapata neema ya kuijua madhabahu hiyo.
una maanisha kuwa madhabahu ikichezewa its ok?
na unajua kuwa zipo madhabahu za aina ngapi?
 
una maanisha kuwa madhabahu ikichezewa its ok?
na unajua kuwa zipo madhabahu za aina ngapi?
Swali zuri madhabahu ni pale inapofanyika ibada,Hata shetani ana madhabahu,wachawi wana madhabahu,kwahiyo ukisema madhabahu haichezewi nilikuuliza unaijua madhabahu ya huyo Mtumushi kwamaana madhabahu huwa inataja jina la yule mwenye kiti cha enzi cha madhabahu husika.
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
Kama TB Joshua ni tapeli yy ni nani
 
lini ananda kuuza gongo ? alisema waliomzushia kanywa lucekelo( konyagi) asipokufa ye ataenda uza gongo
 
Sipati picha ange react je kama angetajwa kwenye kashfa ya dawa za kulevya
 
Back
Top Bottom