Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Anashambulia level isiyo yake. Yeye apambane na wamiliki wa makanisa bongo ambao ndio level yake.
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
Neno la kujifunza hapa ni "SHIKA IMANI YAKO".Imani tu ndiyo itakayokuponya.
Kamwe sitokaa nimdharau mtu kwa dini, imani wala dhehebu lake.
 
Sisi hapa tunasubiri tu ule utabiri wa Mzee wa Upako kuhusu Kufa kwa waandishi wote wa habari walioandika lile tukio la yeye kukutwa kalewa chakari huku akiporomosha matusi huku akinyeshewa na mvua.
Mzee wa Upako alijiapiza kuwa kama waandishi hao wa habari kufikia mwezi March mwaka huu hawatakuwa wamekufa basi yeye mzee wa Upako ataacha kuhubiri na kwenda kuuza gongo.

Sisi tupo hapa hapa JF tunasubiri.
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
TB J alipatia kwenye kutabiri alisema Hillary anaonekana kushinda uchaguzi na ni kweli kwan Hillary anamzidi kura 3million Trump sema siasa za marekani wanazijua wenyewe so kwa hapa mzee kachemka
 
Anayebisha TB Joshua hana upako ujue anabisha anafanya hivyo kwa maslahi yake binafsi pia anaogopa kuumbuliwa pia ni mchumia tumbo huyu mzee ws upako hana lolote jipya alilolifanya kama tunavyomuona TB Joshua anvyofanya kwenye makongamano yake Columbia, Mexico au kanisani kwake Nigeria
 
TB Joshua ana tofauti na Babu wa Loliondo kwa upako
 
Back
Top Bottom