Habari waungwana, naomba kusaidiwa kimawazo nifanye nini katika hili.
Nina mchumba wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano kwa takribani miaka miwili na nusu, japo sijawahi kujitambulisha kwao mpango wa utambuzi ulikuwa ni mwezi huu wa November na mipango ilikuwa ishawafikia wazazi.
Hivi majuzi mchumba wangu aliugua gafla tumbo na baada ya vipimo alilazimika kufanyiwa upasuaji uliopelekea kuondoa mfuko wa uzazi ili kunusuru maisha yake.
Ukweli nimechanganyikiwa nini nifanye, hasa ikizingatiwa tunapendana sana.
Lakini nawaza je, ndo hatutapata familia yenye watoto kabisa kama tutaoana? Tafadhali hebu nijengeni kifikra.