Mchumba wangu katolewa kizazi

Mchumba wangu katolewa kizazi

duh,,,, kila mmoja na lake......tambua utakachuamua ndo mustakabali wa maisha yako......pole brother..
 
Habari waungwana, naomba kusaidiwa kimawazo nifanye nini katika hili.

Nina mchumba wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano kwa takribani miaka miwili na nusu, japo sijawahi kujitambulisha kwao mpango wa utambuzi ulikuwa ni mwezi huu wa November na mipango ilikuwa ishawafikia wazazi.

Hivi majuzi mchumba wangu aliugua gafla tumbo na baada ya vipimo alilazimika kufanyiwa upasuaji uliopelekea kuondoa mfuko wa uzazi ili kunusuru maisha yake.

Ukweli nimechanganyikiwa nini nifanye, hasa ikizingatiwa tunapendana sana.

Lakini nawaza je, ndo hatutapata familia yenye watoto kabisa kama tutaoana? Tafadhali hebu nijengeni kifikra.

Dah sema we ni mzinzi sana, miaka 2? Anyway alikuwa mtu na dem wake naona, piga chini
 
unaambiwa kizazi kimetolewa! imani hiyo imani gani yenye kumwezesha.mtu kuzaa pasipo kizazi?

Remote watu wana imani humu jamvini balaa...! Engine imeng'olewa watu wanasema kwa imani gari itapanda mlima kitonga? Aaaah!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa huo mtihani ndugu yangu. Hili suala shirikisha wazazi.
 
Pole kwa yaliyokupata lakini upendo una nguvu kuliko jambo Lolote lile, unaweza owana na mwenye kikaz na bado msipate watoto Kwa maana watoto ni zawadi toka kwa mungu... Kumbuka mwenzio anakuhitaji sana katika kipindi hiki kigumu anachopitia
Imagine tatizo lingekuwa limekupata wewe alafu mwenzio akafikiria kukuacha, ungeumia kiasi gani?

Sikubaliani na wewe! Nyie mnamshauri mtu kwa kufuata natural justice ambayo kiukweli haipo. Huyu jamaa kiukweli akioa huyo dem hataishi nae! Raha ya nyumba ni watoto jamani na raha ya mtoto baba na mama wahenye kulea mimba! Eti mwingine anasema akaadopt sijui? Unamuadopt mtu wewe huwezi kuzaa wako? Shem bana ishakula kwake. Kama ungekuwa kwenye ndoa then augue like a few months later then it is fine japo lazima ujikunje nje upate mtoto! Ingekuwa labda official engagement ishafanyika ningeshawishika ila eti mnakutana Vigwaza maporini kule halafu kaumwa we umepagawa! Dah
 
Najaribu kuvaa viatu vyako lakini nashindwa ku imagine! Huko katika kipindi kigumu sana na kila maamuzi utakayo yafanya Lazima ya muumize mchumba wako!

Ungekuwa na Mtoto wa nje hata mmoja ungekuwa katika nafasi nzuri zaidi!

Kuna Mwingine anaweza akakuruhusu ukazae nje ya ndoa hata kama mkioana lakini unatakiwa kulichukulia hata kwa upande wako ingekuwaje kama mmebakiza mwezi mmoja kufunga ndoa halafu unapata ajali ambayo inapelekea wewe kukatwa miguu itakuwaje kwa upande wake? Ni fair hakikuacha?

Hukupenda kukatwa miguu!
Hakupenda kutolewa kizazi!

Hapa ndipo busara na ujasiri wako utapimwa vyema!
Japo watoto ni muhimu kwenye ndoa lakini ni mpango wa mungu maana anaweza akawa na kizazi na msiwapate!

Jaribu kumuuliza kwanza kwa upande wake anasemaje? Yeye awe wa kwanza kusema chochote!

Pia unatakiwa kujiuliza wewe huko tayari kuishi nae hata kama hawezi kuzaa? Kama akikuruhusu ukazae nje huko tayari kumuoa?
Kwa sababu tuna oa kwaajili ya familia zetu je familia yako inasemaje kuhusu hili swala?

Hiki ni kipindi kigumu kwako..pengine kuliko kipindi kingine!
 
Watoto ni zawadi toka kwa mungu anaweza akakupa au asikupe but uamuzi ni wako kama unaona hutoweza kuvumilia bila kuwa na mtoto basi muache mapema kuliko kuja kumpa maumivu zaidi hapo baadae
 
Look everywhere dunia ina watu...na wengi wao hawana hata pa kuishi, hawana chakula, hawana wa kuwajali na hawaitaki hata dunia yenyewe. We are only human beings. Hatuwezi kumpa mtu maisha wala afya. Tunazaa ndio lakini pumzi ya uhai anaitoa Mungu. Yeye ndiye anayejua ni kwanini wewe una uwezo wa kuzaa na mwingine hana. Anajua ni kwanini leo wewe ukaishi na mwenzio akafa. Ukimtazama yeye Mungu. Nothing on earth will make ur heart down. Using'ang'anie kupata mtoto ilhali hujui destiny yake....
Just know children come from God. Na sababu ya ndoa si watoto.

Acha kumingiza mwenzio kwenye hisia na majibu yasiyo na tija kisayansi... marriage and sex were meant for offspring development and nothing else..... watoto wanakamilisha ndoa..... hizo siasa unazopiga hapo hazina maana..and FYI the successfull organism on Earth is the one which leaves as many off springs as possible, binadamu ni K- selected..
issue ya destiny wazazi(nyie ) ndo hupanga na mtoto akikua anaamua, it has nothing to decide whether to have kids or not........ sasa Circumstance isimforce aache kuzaa kisa sijui love, atakuja juta baadae au atamuumiza mwenzie vibaya sana kwani wote wanataka watoto lakni mmoja ni biologically functionless.. unless they are coming from first class society, bado relatives pressure itakuwa kubwa saana kuhandle....on top of that if he didnt know.. people learn to love with time ndo maana kuna divorce na infidelity, still the choice is his!!!!!
 
Bhaaaas! Namie nimemlima hivi hivi unajua hapa JF watu wanapenda sana kushauri uongo! Uchumba wenyewe haukuwa official fikiria wamekutana Vigwaza huko halafu hata wazazi hawautambua na jamaa yetu eti kadata! Mi nimemwambia piga chini
 
Remote watu wana imani humu jamvini balaa...! Engine imeng'olewa watu wanasema kwa imani gari itapanda mlima kitonga? Aaaah!

Kuna watu wanapenda kufanya mchezo na Mungu! Sasa kwanini wasifikiri Mungu ndio kaamua kitoke kizazi?
 
Last edited by a moderator:
Ukiondolewa kizazi ,huwezi kupata au kuzaa au kushika mimba ,tuwache kukufulu kwa kumsingizia Mungu ,Yeye Mungu ndio alioipanga hiyo njia sasa ukiiondoa bado unamuelekezea Mungu ,none sense ,jaribuni kuwa wawazi ,Mwenyezi Mungu amepanga njia hizo ,hayo ya india ni elimu tu aliyopewa binadamu. Ila kusema umeondolewa kizazi halafu ushike Mimba itakuwa wamekudanganya tu hawajakuondoa kizazi .
 
Back
Top Bottom