Ndukidi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 1,500
- 1,303
Habari waungwana, naomba kusaidiwa kimawazo nifanye nini katika hili.
Nina mchumba wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano kwa takribani miaka miwili na nusu, japo sijawahi kujitambulisha kwao mpango wa utambuzi ulikuwa ni mwezi huu wa November na mipango ilikuwa ishawafikia wazazi.
Hivi majuzi mchumba wangu aliugua gafla tumbo na baada ya vipimo alilazimika kufanyiwa upasuaji uliopelekea kuondoa mfuko wa uzazi ili kunusuru maisha yake.
Ukweli nimechanganyikiwa nini nifanye, hasa ikizingatiwa tunapendana sana.
Lakini nawaza je, ndo hatutapata familia yenye watoto kabisa kama tutaoana? Tafadhali hebu nijengeni kifikra.
Lengo kubwa la kuoana ni kuzaa watoto.
uzuri ni kuwa hili tatizo limetokea bahati nzuri wewe umejua na mchumba wako. Kaeni chini mkubaliane mtafanyaje ikiwa yeye atashindwa kabisa kupata watoto. Naamini kama kweli mnapendana mtapata suluhisho, ikiwa ni pamoja na ku adopt, wewe kuzaa nje na kumleta mtoto mkamlea etc.