Mchumba wangu katolewa kizazi

Mchumba wangu katolewa kizazi

Luhungu

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2013
Posts
817
Reaction score
237
Habari waungwana, naomba kusaidiwa kimawazo nifanye nini katika hili.

Nina mchumba wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano kwa takribani miaka miwili na nusu, japo sijawahi kujitambulisha kwao mpango wa utambuzi ulikuwa ni mwezi huu wa November na mipango ilikuwa ishawafikia wazazi.

Hivi majuzi mchumba wangu aliugua gafla tumbo na baada ya vipimo alilazimika kufanyiwa upasuaji uliopelekea kuondoa mfuko wa uzazi ili kunusuru maisha yake.

Ukweli nimechanganyikiwa nini nifanye, hasa ikizingatiwa tunapendana sana.

Lakini nawaza je, ndo hatutapata familia yenye watoto kabisa kama tutaoana? Tafadhali hebu nijengeni kifikra.
 
pole kwa uwezo wa mungu mtapata watoto
 
angalia lengo la kuoana nae kama ni watoto, chapa lapa ila kama ni furaha ya moyo wako na kama kutokuwa na mtoto haitakusumbua endelea nae.

watoto ni zawadi toka kwa Mungu...unaweza oa mwenye kizazi na asizae vilevile. chamsingi tambua lengo lako katika ndoa
 
muoe huyohuyo, ukimuacha nawe yatakukuta ya kushindwa kusimamisha,
 
Pole mkuu ni changamoto kweli katika kufanya maamuzi hapo.....
 
Watoto ni matokeao tu na.majibu ya ndoa na hua n.mpango wa mungu kama unampenda kweli muoe penye upendo wa dhati hapaingiliwi na.chochote kile
 
Look everywhere dunia ina watu...na wengi wao hawana hata pa kuishi, hawana chakula, hawana wa kuwajali na hawaitaki hata dunia yenyewe. We are only human beings. Hatuwezi kumpa mtu maisha wala afya. Tunazaa ndio lakini pumzi ya uhai anaitoa Mungu. Yeye ndiye anayejua ni kwanini wewe una uwezo wa kuzaa na mwingine hana. Anajua ni kwanini leo wewe ukaishi na mwenzio akafa. Ukimtazama yeye Mungu. Nothing on earth will make ur heart down. Using'ang'anie kupata mtoto ilhali hujui destiny yake....
Just know children come from God. Na sababu ya ndoa si watoto.
 
We unacho kizazi cheyewe!? kama mnahela mnaweza mkapandikiza india!!
 
Mungu ni Muumbaji,na bado anaendwlea na kazi yake,mwamini Mungu aliye mtoaji wa vyote,haijalishi kizazi kimetolewa Mungu anaweza kumwekea kingine na mkapata watoto
 
misingi ya ndoa kwenye akili yako ndiyo itakayo toa majibu sahihi na maamuzi sahihi
 
Back
Top Bottom