Mbona ulimtoa nje kidogo kujadili jambo ambayo lilikuwa gumu kuamua mwenyewe? Mimi nitakupa ushauri gani wakati ni wewe uliyemtongoza mwenyewe, ukampeleka hadi kwenu.
Sikiliza, ndg mtwae huyu mwanamke, awe wako kwa misha yako yoote. Huyu kwanza ni saafi, tayari unajua ni shamba linalo zaa. Mbona wengi tu wana uzuri wa sura na tumbo flat lakini hawana tumbo la uzazi tena? Weshalikausha kwa vidonge vya majira.
Kama unataka watoto, huyu ndiye anakufaa. Ingekuwaje kama ungekutana naye mjini baada ya kuzaa na akakuambia hana mtoto? Acha ushamba, chukua mzigo. Nakuhakikishia huyu atakuwa mwaminifu siku zoote. Hata ungeenda London siku zijazo, huna haja kumwekea mitego. Hatarudia tena.
Kijana chukua mzigo wako, chapa mguu na furushi lake hilo, mwenye mzigo aje akuone kama yeye ni kidume kweli. Lakini kama akija mapema kabla ya kushusha mzigo huo akasema yeye ndiye mhusika na akaomba kuuchukua mapema, mruhusu na muendelee na maisha yenu na mkeo. Kama haji, mtoto ni wako tuuu.