Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,898
Mkuu pole sana. Usitumie hisia katika hili, tumia akili zaidi. Jaribu kufikiria mchakato mzima hadi akapata mimba,inaonekana walianza mbali, kutoka kutongozana,kukubaliana, kuwekeana miadi, kukutana,na hatimae kubadilishana hardware za maungo yao.koooooote huko alikuwa hajui kama ana mchumba?
Imani yangu ni kuwa kwa kipindi chote hicho mlikuwa mnawasiliana na alikuficha, je unadhani ni mtu wa kumuamini tena huyo?
Fahamu kwamba baba wa huyo mtoto atakuwa na haki juu ya mwanawe na pia atakuwa na jukumu la kujadili na kupanga mustakbali wa mwanawe kwa kushirikiana na mama wa mtoto ambaye ni mchumba wako. Je upo tayari kuyabeba hayo katika maisha yako yote? Upo tayari kumkaribisha mume mwenzio sebuleni kwako akija kumuangalia mwanawe?upo tyari kumuacha sebuleni mchumba wako na mume mwenza wakijadili yahusuyo mtoto wao?kaka wanawake wenye sifa za kuwa wake wapo ila inategemea tu namna unavyowatafuta, mrudie mungu akuongoze katika kutafuta mke mwenye sifa sahihi za kuwa mke bora, huyo mama kijacho msahau kabisa.