Mchumba wangu amezaa na mume wa mtu!

Mchumba wangu amezaa na mume wa mtu!

Lumia920

Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
41
Reaction score
10
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.
 
Misongo mingine ya mawazo ya kujitakia, sasa mtu ana mimba ya mwanamme mwenzio wee unasongoka nini?

Kama una kifua beba mwanamke na mtoto wake, kama huuna kifua tafuta mwingine uanze upya.

Afu unawaonea aibu wazazi wako, umekuwa mwali au ulikuwa unawaolea wao? Grow up!

Na kuzaa hakumfanyi huyo dada moja kwa moja asiwe mke mwema, labda alizidiwa na 'ash.ki' tu.
 
Achana nae, tazama mbele. Hicho ni kipimo bora kabisa kwa mustakabali mwema wa maisha yako ya baadae. Hakuna love isiyokuwa na maumivu, hivyo unapitia kipindi hicho cha maumivu, JIEPUSHE.
 
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.
 
Pole sana mkuu. Ningekuwa wewe ningevunja tu huo uchumba, mi kwangu kosa kubwa kabisa la kuvunja uhusiano ni kucheat. Kama ameshindwa kuvumilia huku mwanzoni kwenye ndoa ndo ataweza. Ila mwamuzi ni wewe.
 
Mkuu Kikubwa ni upendio kama unampenda basi samehe na waambie wazazi you are responsible kwa hiyo mimba (Sitaki kutoa mimamo wangu kwa hili)
 
Pole sana Mkuu kwa yaliyokukuta. Wewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho kama unaweza kumsamehe au la ila washirikishe na Wazazi wako pia kabla ya kufanya uamuzi wako. Pole sana.
 
Hakuna kuvunja uchumba kwani kama Mungu amekuandikia wako ni wako
Hivi ingekuwaje kama ingekuwa ni wewe umemtia mimba msichana mwingne??? Je huyo mchumba wako angekusamehe na.angelea mtoto hivyo yakupasa kumsamehe hakuna aliye mkamilifu na muendelee na mipango yenu
 
Ila mpime kwanza afya maana inawezekana ametembea peku pia na watu wengine tofauti.
 
Hakuna haja ya kumsamehe huyo ni nyoka tena ndumila kuwili anajifanya anakupenda kumbe hamna lolote. Ameamua kuzin wakat anajua fika kuwa anamchumba akaona haitosh ameamua kukuletea mimba kamakwambwa ww n bwabwa la kulea mimba na dam za wenzio. Kaka najua umependa lakin sio penyewe........ Mm nakushaur usisikilize chochote mpge chin tu..... Run away....
 
mwache aende zake, wazazi wako watampenda mwingine mwaminifu na anaye kupenda. Mwanamke akipenda mwaume hawezi kusubutu kuiba nje tena hata kama akifanya hivyo basi mpira lazima utumike.

Ila huyu inaelekea alikuwa analala na huyo mwenzake hata kabla haujaenda kusoma na wakazoeana na kulala bila kinga, kwa hiyo embu kimbia mtakie maisha mema.

Ukiwaambia wazazi wako mwenzio amelalwa na amepewa mimba na anaomba umlele mume wa mtu mtoto watakubali?

Ila wanaume wengi wanapenda kung'ang'ania wanawake kama wanawasaidia kimaisha, sasa wewe sijui unasaidiwa maana tunaweza kukushauri humu na ukaendelea tu kujilinda kimaisha. nasema hivi maana ulivyoanza kumshukuru Mungu kuhusu kusoma kama vile ilikuwa haukutegemea...

Pole utapata binti mwingine mwaninifu omba Mungu umsahau huyu, inauma ila imeshatokea. baba mtoto ataendelea kuwepo maishani mwake..utaweza?
 
Wanasema nirudi Igunga maisha yashanishinda.....

cc: lara 1
 
Last edited by a moderator:
What the hell....?!?!

Is she the be-all and end-all of your existence or what? If I were you I'd have dumped her in a heartbeat.

What are you waiting for? Why are you dithering?

Just cut her loose and keep it movin'.
 
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.

Pole sana, Usiwaze lolote juu ya huyo mwanamke si wako. Ukimuoa utapata shida kubwa sana baadaye. Wewe huna hatia yoyote kwake yeye ndiye mwenye hatia kwako. Wajulishe wazazi na umuache. Si wako huyo. Utapata shida baadaye. Pole sana nakuhurumia sana.
 
Sijaelewa unataka tukushauri nini? Kama umuoe akiwa na mimba ama umuachie mume wa mtu aendelee nae?
 
Kuna watu wanawaza hata hili, mbona mna mioyo migumu sana? Binafsi hapo ndio ingekua mwisho wa kuonana, kuwasiliana na kila kitu. Mtu kaanza kutembea na jamaa mwingine hajakwambia, kabeba mimba hajakwambia na bado unawaza kuendelea nae. Vp usingerudi like 3yrs ingekuaje? Angekwambia ukweli kwa simu afu akuombe ukirudi umuoe? BS
 
^^
Itakusumbua mbeleni ukilazimisha..bado kuna hifadhi njema ya mabinti wengine wanaohitaji ndoa.
Be brave,,relax
^^
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom